Godwin Matiko
New Member
- Jul 28, 2022
- 3
- 2
UWAJIBIKAJI NA MAENDELEO
Palikuwa na kazi ya muhimu kufanyika na kilamtu aliamini kwamba mtu fulani angeliweza kuifanya. Mtu yoyote angeliweza kuifanya, lakini hapakuwa na mtu aliyeifanya. Mtu mmoja akapata kufadhaika kwa kazi kutokufanyika, kwasababu ilikuwa ni kazi ya kilamtu.
Kilamtu alifikiri mtu yeyote angeliweza kuifanya kazi, lakini hapakuwa na mtu aliyefikiri kwamba kila mtu asingeliweza kuifanya kazi. Hitimisho lilikuwa kwamba kilamtu alimlaumu mwingine wakati hakuna yeyote aliyeifanya kazi ambayo kila mtu angeliweza kuifanya. Fasihi hii andishi iliandikwa na mshairi anayefahamika kwa jina Charles Osgood.
Uwajibikaji ni msiba wenye kilio kisicho na sauti lakini una tafuna familia, jamii na taifa letu la Tanzania katika maeneo yote ya kijamii, kiuchumi, kiutawala na kisiasa. Uwajibikaji ni hatua ya makusudi katika kuhakikisha kilamtu anatimiza majukumu yake katika nafasi aliyopo binafsi, kifamilia, kijamii na kitaifa kwa ujumla.
Changamoto na matatizo mengi yanayotokea kwetu binafsi, familia zetu, jamii zetu na taifa letu kwa kiwango kikubwa ni watu kushindwa kutimiza majukumu yao kwa ufanisi. Uwajibikiaji ni msingi muhimu wa maendeleo katika maeneo yote maisha.
Shabaha ya andiko hili ni kutusaidia kutambua, kutenda na kuongeza juhudi katika kutimiza wajibu wetu tulionao kwetu binafsi, familia zetu, jamii yetu na taifa letu kama ifuatavyo;
Wajibu wetu binafsi
Maendeleo ya familia, jamii na taifa huanzia kwa mtu mmoja mmoja. Uwajibikaji katika ngazi ya mtu binafsi ni hatua muhimu zaidi maana ndiyo inayoamua maendeleo ya ngazi zingine. Changamoto zinazowakumbwa watu binafsi zinazokwamisha juhudi za uwajibikaji zimekuwa nyingi kiasi kwamba bahati ndio imebaki tumaini kuu la kufanikiwa.
Kutojiwekea malengo, kutokuwa na ndoto ya maisha, kuridhika katika mazingira tuliyopo, kutokuwa na watu sahihi wa kutushauri, mafanikio ya haraka, tamaduni za kigeni, malezi ya kisasa na yanayofanana na hayo ni vikwazo vikubwa vya uwajibikaji na maendeleo endelevu. Msingi wa uwajibikaji umejikita kwenye kutimiza majukumu tuliyonayo na pia kuwa wabunifu katika kutimiza wajibu wetu, kutengeneza na kutumia fursa zinazotokana na kuwajibika kwetu.
Tukiweza kuvishinda vikwanzo vinavyotukwamisha kutimiza majukumu yetu hakina tutakuwa na maendeleo makubwa katika ngazi ya mtu mmoja mmoja. Shabaha ya wajibu wetu binafsi ni kuhakikisha tunawajibika katika maeneo yetu ya kazi, kuongeza ufanisi na kutumia fursa zilizopo ili tuweze kuwa na msingi mzuri wa maendeleo ya familia, jamii na taifa.
Tukishindwa kuwajibika tutabaki kulaumiana sisi wenyewe na serikali kila kukicha wakati tuna nafasi ya kuwajibika katika yale yaliyo ndani ya uwezo wetu na hatuwajibiki ipasavyo. Fasihi hii andishi itusaidie kuwajibika kwenye shughuli zetu za kila siku.
Maswali ya msingi;

- Wajibu wangu ni upi katika shughuli zangu za kila siku?
- Je, natimiza wajibu wangu ipasavyo?
- Nifanye nini nizidi kuongeza ufanisi katika kuwajibika kwangu?
Wajibu katika familia
Familia kwa aina zake ni msingi mzuri wa maendeleo ya jamii na taifa. Katika kushinikiza uwajibikaji katika ngazi ya familia ni vema kila mtu kwenye familia akatimiza majukumu yake ili familia izidi kuwa bora na kuwa na maendeleo. Yeyote anayeshindwa kutimiza majukumu yake katika familia lazima ajua anachangia kwa kiwango kikubwa kushuka kwa maendeleo ya familia na kuchochea matatizo. Baba, Mama na watoto kila mtu ana wajibu wake. Familia ambazo baba anakimbia majukumu zinapitia kipindi kigumu sana.
Familia ambazo mama anakwepa majukumu ni hakika kizazi cha nyoka kitakuzwa. Watoto wanaposhindwa kutimiza majukumu ya familia ndio inatoa picha mbaya zaidi ya vizazi vijavyo kwa maana watoto ndio wazazi wa baadae.
Familia bora ni msingi wa maendeleo. Kuna changamoto kubwa ya ongezeko la famila za mama na watoto pekee pamoja na baba na watoto pekee. Matatizo au maendeleo ya familia athari zake huonekana kwenye jamii na taifa. Kwa sasa ni swala la kwaida kusikia ndugu wameuana kisa kugombea mali, ndugu wa familia kujiua, watoto wametelekezwa, baba kakimbia familia, mama kakimbia familia. Fasihi hii itukumbushe kila mmoja wetu kwenye ngazi ya familia kutambua tuna wajibu wa kufanya katika familia zetu.

- Nini wajibu wangu katika familia ?
- Je, ninatimiza wajibu wangu katika familia ?
- Nifanye nini niongeze ufanisi katika kutimiza majukumu ya familia ?
Wajibu katika jamii
Jamii ni muunganiko wa familia. Familia zetu zikiwa na watu wenye kutimiza majikumu yao vizuri hakika jamii zetu zitakuwa bora sana na zenye maendeleo. Tuna changamoto nyingi zinazoikabili jamii kama vile ukosefu wa maadili, rushwa, viongozi wabinafsi, kupungua kwa utu, kuongezeka kwa watoto wa mitaani, unyanyasaji kwa aina zake na mambo yanayofanana na hayo.
Msimgi wa changamoto zote hizo zinaweza kutatuliwa katika ngazi ya familia endapo kila mtu atatimiza wajibu wake. Shabaha ya andiko hili ni kuikumbusha jamii kuwa changamoto nyingi zipo ndani ya uwezo wetu katika ngazi ya familia na binafsi, kama tutaamua kuwajibika hakika changamoto nyingi za kijamii zitapungua sana kama sio kuisha kabisa. Kila mmoja wetu ana nafasi ya kusaidia katika kutatua changamoto za kijamii, yawezakuwa kupitia kuelimisha jamii, kutoa misaada na mambo yanayofanana na hayo.

- Nini wajibu wangu kwa jamii inayonizunguka ?
- Je, natekeleza wajibu wangu ?
- Nifanye nini ili niweze kutekeleza wajibu wangu kwa jamii ?
Wajibu katika taifa letu
Taifa ni muunganiko wa jamii mbalimbali. Katika kutatua changamoto zetu binafsi na zile za jamii, tuna nafasi ya kuwajibika katika taifa letu ili tuweze kuchochea maendeleo. Tunapaswa kuwa wazalendo na kuondokana na ubinafsi katika matumizi ya rasilimali za taifa zikiwemo mali za umma, wananchi na kutengeneza fursa nyingi zitakazowasaidia watu kuongeza kipato, ujuzi na maarifa zaidi.
Tanzania ni yetu sote basi tupambane kuijenga kwa hali na mali. Viongozi wetu wana nafasi kubwa ya kuhakikisha yale mambo ambayo yapo nje ya uwezo wa wananchi hayawi kikwazo cha maendeleo ya jamii lakini pia maamuzi ya viongozi hayaongezi matatizo zaidi katika jamii bali, yaongeze unafuu wa maisha na kupunguza urasimu hasa kwenye eneo la biashara na shughuli nyingine za kijamii.

- Nini wajibu wangu kwa taifa langu ?
- Je, nina timiza wajibu wangu kwa taifa ?
- Nifanye nini kuongeza ufanisi wa kutekeleza wajibu wangu kwa taifa ?
Mwisho
Asanteni kwa kusoma andiko hili lenye shabaha ya kufufua uwajibikaji kuanzia ngazi ya mtu binafsi mpaka ngazi ya taifa. Kila mtu ana wajibu wa kufanya ili taifa letu liwe na maendeleo endelevu. Karibuni kwa michango.

Upvote
2