Kgy26
Member
- Sep 14, 2022
- 6
- 4
Maana ya Uwajibikaji
Ni hali ya kujituma kutimiza majukumu au wajibu fulani kwa wakati, mahali na muda sahihi.
Neno hili katika maadili na utawala linafananishwa na kuwa na jukumu la kujibu, kutegemewa au kutoa hesabu ya kile ulichopewa dhamana ya kukifanya.
Dhana hii imekuwa ikitumika sana katika utawala kwa sababu viongozi hupewa dhamana na kutegemewa kuleta mabadiliko katika jamii iliyowaweka madarakani.
Serikali yoyote iwe inaongozwa na demokrasia au kimabavu ina dhamana kubwa ya kuonyesha uwajibikaji na kuleta manufaa kwa wananchi kwani wao wanasimamia rasilimali zote zitumike kwa weledi ili kuleta ustawi kwa taifa husika.
Uwajibikaji unatoka kwa serikali kwenda kwa wananchi/Jamii na pia wananchi/Jamii kwa serikali
Serikali inao wajibu wa kuwahudumuia wananchi kulingana na sheria, kanuni na sera zilizowekwa kuhakikisha wanafikia hali ya juu kimaisha, kila kiongozi katika wadhifa wowote anao wajibu wa kuwajibika kuhakikisha anatekeleza majukumu yake kulingana na nafasi yake aliyopewa yaani alete matunda ya kazi yake au ajibu kile alichoagizwa kutekeleza au kutatua changamoto na kuvusha taifa au wananchi kutika sehemu moja kwenda nyingine iliyo bora zaidi.
Wananchi/Jamii wanao wajibu wa kuwajibika katika nafasi nyingi kuanzia kufanya kwa ufanisi shughuli zao za kila siku ili kuleta tija kwa taifa, kuhusika katika kupata elimu, kupiga kura, kulea watoto/taifa vizuri. Jamii ina mchango mkubwa sana kwa maendeleo ya taifa fulani kupitia uwajibikaji kwani ndio nguvu kazi ya taifa kwa maana ya wafanyakazi za uzalishaji mali na shughuli nyingine binafsi ambazo hutokana na sera au kanuni au sheria za nchi kwa jamii ambayo ndiye mtekelezaji mkubwa kwa usimamizi wa serikali.
Haya ni baadhi ya mataifa makubwa duniani yaliyo na uwajibikaji mzuri Morway, Finland, New zealand, Switzerland, Netherland(Chanzo Voice and accountability by country, around the world | TheGlobalEconomy.com)
Mifano ya Uwajibikaji wa Serikali
Uwajibikaji huleta matokeo makubwa sana kwa taifa hasa ikiwa kwapande zote yaani jamii/wananchi na serikali
Mataifa yaliyoendelea sasa kama Japani, China na Marekani uwajibikaji ulikuwa wa hali ya juu sana pasina kujali njia zilizotumika kuzalisha mali wengine walitumia watumwa na kushurutisha, lakini dhana hii ya uwajibikaji ndiyo iliyo paisha mataifa haya na kutajwa sana duniani kwa maendeleo makubwa.
Manufaa ya Uwajibikaji wa serikali
Serikali ikiwajibika ipasavyo mambo yafuatayo yanatokea;
Ili taifa lipate manufaa linategemea uwajibikaji pande mbili kwa serikali na jamii/wananchi
Ukichukulia mifano ya nchi zilizo endelea kama china enzi za nyerere walikuwa wakifanya ujamaa dhana iliyochangia sana maendeleo ya taifa hilo kufikia lilipo sasa.
Ukiangalia upande wa teknolojia wako juu ni kwa sababu serikali inachochea ubunifu kwa kufungua vyuo, kulea wabunifu na kuwasaidia kaika mawazo waliyo nayo ya kibunifu ili walete kile ambacho wanakibuni, hii imesaidia sana maana sasa hata watoto wa shule za awali kutengeneza nyenzo ndogondogo kama(Calculator) katika mazoezi yao ya darasani.
Hii inaleta picha kwamba pande zote mbili zinawajibika katika kuchochea ustawi wa nchi
Ni muhimu kujua ya kwamba bila kuwajibika ni vigumu kufikia malengo iwe kwa mtu binafsi, familia, kampuni, shirika na hata taifa. Hivyo ni vyema kurudi katika dhana hii na kutafakari kwa kina dhana hii na kuifanyia kazi tukionyeshwa mfano na nchi zilizoendelea. Tuwajibike kifamilia, ofisini na katika kutumia fursa mbalimbali.
Ni lazima pia kupanda mbegu ya uwajibikaji kwa kizazi kijacho kwa njia za kuwaoneshwa umuhimu wa kufanya kazi kwa kufanya kwa vitendo, kusimamia majukumu waliyo nayo na kuhakikisha wanayamaliza kwa wakati.
Viongozi mbalimbali husisitiza uwajibikaji katika taifa kama kichocheo kikubwa cha maendeleo na ustawi wa nchi, hivyo kuanzia kwa mtu mmoja mmoja, taifa na dunia endapo hii dhana itatiliwa maanani itaondoa baadhi ya changamoto ambazo hazikupaswa kutokea ila kwa kukosa tu uwajibikaji kwa mfano vifo kama wauguzi hawawajibiki, magonjwa kama watu hawawajibiki na afya zao, uongozi mbaya kama wananchi wa kuchagua viongozi sahihi, vita kama mipaka ya nchi haikulindwa vilivyo, wizi kama watu hawawajibiki kuchuma mali halali, uharibifu wa mazingira kama watu hawawajibiki kutunza mazingira, miondombinu hafifu ikiwa viongozi waliopewa dhamana hawakuwajibika ipasavyo au Kilimo duni kama serikali kaikutoa pembejeo za uhakika au mkulima hakuzingatia kuwajibika kufanya kilimo bora.
Madhara makubwa hutokea duniani kwa kukosa kuwajibika zaidi ya yaliyooroheshwa hapo juu ila wajibu namba moja ni Mungu mwenyewe ametuleta duniani kufanya kazi yaani kuwajibika ukirejea maandiko ya dini binadamu wa kwanza adamu alipewa dunia aitunze. Sisi nasi tunapaswa kuwajibika kwa nafasi tulizo nazo ili tulete manufaa au tija katika nafasi hizo iwe ni mtoto, mzazi, kiongozi wa serikali, mwalimu, daktari, askari na nafasi nyingine.

- Kutunga sheria, kanuni na sera ambazo zitaongoza nchi vizuri na kuleta tija
- Kusimamia sheria, kanuni na sera zilizotungwa kwa kuhakikisha zinafuatwa bila ukosefu wa haki au uvunjifu wa amani
- Kufuata kanuni na mifumo ya serikali kama ni ya kidemokrasia au la
- Kuhakikisha wananchi wanalindwa pamoja na mali zao
- Kusimamia utawala bora
- Kuhakikisha rasilimali za taifa husika zimasimamiwa vizuri kwa manufaa ya wananchi na taifa kwa ujumla
- Kuhakikisha chaguzi za viongozi zinakuwa huru na kwa haki
- Kuhakikisha kazi zinafanya na kupata mapato halali kwa ustawi wa taifa
- Kufuata sheria, kanuni na sera za nchi bila kushurutishwa
- Kupiga kura na kuchagua viongozi wawajibikaji
- Kutumia fursa zilizopo ili kustawisha taifa
Uwajibikaji huleta matokeo makubwa sana kwa taifa hasa ikiwa kwapande zote yaani jamii/wananchi na serikali
Mataifa yaliyoendelea sasa kama Japani, China na Marekani uwajibikaji ulikuwa wa hali ya juu sana pasina kujali njia zilizotumika kuzalisha mali wengine walitumia watumwa na kushurutisha, lakini dhana hii ya uwajibikaji ndiyo iliyo paisha mataifa haya na kutajwa sana duniani kwa maendeleo makubwa.
Manufaa ya Uwajibikaji wa serikali
Serikali ikiwajibika ipasavyo mambo yafuatayo yanatokea;
- Haki na ustawi wa taifa kwa sababu sheria na taratibu zimesimamiwa na viongozi waliopewa dhamana wamewajibika ipasavyo
- Wanachi hufurahia na kujivunia taifa lao kutokana na ustawi na kuwa na serikali inayowajibika kwa wananchi.
- Kuvumbua au kuibua mambo mapya kama teknolojia mpya n.k
- Hali nzuri ya maisha
- Ustawi kwa jamii na mtu mmoja mmoja

Upvote
3