SoC02 Uwajibikaji

SoC02 Uwajibikaji

Stories of Change - 2022 Competition
Joined
Sep 2, 2022
Posts
1
Reaction score
0
UWAJIBIKAJI


Uwajibikaji ni hali au kitendo cha kuchukua hatua kutekeleza majukumu mbalimbali uliyo kabidhiwa na watu kimaandishi au kimaneno au kujikabidhi mwenyewe binafsi. Uwajibikaji ni dhana pana kuna uwajibikaji wa mtu yeye binafsi, uwajibikaji kwenye ngazi ya familia, uwajibikaji kwenye ngazi ya jamii na uwajibikaji kwenye ngazi ya Taifa kiujumla.

Watu wengi hususani vijana kwenye nchi zinazo endelea kama vile Tanzania watu wake hususani vijana wamekuwa sio wawajibikaji kwenye ngazi mbalimbali ikiwemo katika ngazi ya familia, jamii na Taifa. Kwa sababu hiyo vijana wame amua kujikita kwenye kulaumu na kulalamika juu ya hali ya uchumi na uongozi uliopo. Pia wana amua paka kudiliki kulaumu hadi wazazi na walezi wao juu ya maisha yao duni. Kumbe kila mtu ana nafasi au wajibu wa kuwa muwajibikaji kwenye mambo mbalimbali pasipo kusimamiwa na mtu.

Vijana wengi nchini Tanzania wamejikita kwenye michezo ya kubahatisha na kamali, uku wakisahau kuwa wana wajibu kwenye kuleta maendeleo chanya ya Taifa. Vijana wanapoteza muda mwingi kwenye kufatilia mambo yasiyo ya msingi wala kuleta tija kwenye maendeleo ya mtu binafsi, mda mwingi wanafatilia umbea na udaku mitandaoni uku ikipelekea kupoteza mda na uwajibikaji kwa ajili ya maendeleo ya jamii na Taifa kiujumla.

Muda mwingi wanao tumia kufanya mambo yasiyo kuwa ya msingi wangetumia kufanya jambo (kuwajibika) kwenye suala fulani ambalo linaleta tija tungefika mbali, bali vijana wengi ni wavivu na sio wawajibikaji kazi yao ni kulaumu na kulalamika. Wanasahau kuwa na wao wana wajibu wa kuleta mabadiliko kwenye jamii. Kazi yao ni kulalamikia uongozi, wakati huo wana wajibu wa kuweza kuwawajibisha viongozi kwa hoja na ujumbe kupitia vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, lakini wajibu huo kwa asilimia kadhaa wana waachia wana siasa.

Mafanikio yoyote katika ngazi ya mtu binafsi, familia, jamii na Taifa kwa ujumla ni uwajibikaji wa mtu mmoja mmoja. Kila mtu akijaza titi kwenye kuwajibika bila kutegemea mtu au kusimamiwa tutafika mbali. Tuache kupoteza mda kwenye mambo yasiyo kuwa na msingi kwa kutumia mitandao ya kijamii vibaya kwenye mambo ambayo hayaleti matokeo chanya kwenye maisha kama vile udaku na umbea. Unakuta kijana anajua historia na maisha ya msanii au mchezaji kuanzia "A" hadi "Z", lakini umri wa bibi yake haujui. Kuwa mwajibikaji kwenye kila nafasi uliyo nayo iwapo serikalini, kazini, kwenye familia na jamii bila kuangalia changamoto mbalimbali.

Ili ufanikiwe lazima uchukue hatua ya kuwajibika kwa asilimia mia moja (100%) bila kuangalia una nini? au hauna nini? , chukua majukumu ya kuwajibika kwenye kuleta mafanikio kwenye Taifa na jamii. Ukifatilia historia ya nabii Musa kwenye vitabu vya Mungu (Biblia na Quaran), Nabii Musa alitaka kutokuwajibika kutokana na visababu sababu kwamba hawezi kuongea na wala hana chochote, ila Mungu alimuuliza una nini mikononi mwako? Akajibu nina fimbo, ile ile fimbo aliyo kuwa nayo alitumia (aliwajibika) kuwakomboa wana wa israel kule Misri. Je, kijana wa Kitanzania una nini?, una elimu, ujuzi, maarifa, ufahamu, akili, afya na Pumzi una tumiaje mambo hayo kwenye kuwajibika?

Hivyo basi vijana na viongozi mbalimbali tutumie vile tulivyo navyo ili tuweze kuwajibika kwenye kuleta mafanikio na maendeleo kwenye familia, jamii na Taifa kwa ujumla. Vijana tupunguze na tuache kabisa sababu sababu zisizo kuwa za msingi, usiangalie nini huna bali angalia nini unacho ili uweze kuwajibika kuleta maendeleo.

Unakuta kijana ana miaka zaidi ya 30 na bado anaishi kwa wazazi ana elimu, akili, na afya lakini achukui hatua kwenye kuwajibika ili kuleta maendeleo ila anakaa na kuanza kulaumu ajira ngumu au hana watu wa kumshika mkono. Ajira ni ngumu sawa ila unatumiaje au unawajibikaje kwenye kuleta au kutengeneza ajira na fursa mbalimbali.

Wazazi wana wajibika ipasavyo kulea watoto na kuwahudumia, tumia mbinu zao basi, mama anapika chapati tumia fursa hiyo kufanya kama yeye ila vijana wengi utakuta wana ona aibu juu ya watu wata mchukuliaje. Ndugu zangu haya maisha usifaanye kitu kwa kumtazama mtu au watu pambania maisha yako, wajibika na maisha yako fanya jambo ambalo unajua auvunji sheria kihalali na inaleta tija kimaendeleo wajibika tu usiangalie nyuma.

Kuna msemo una sema "kama fursa azipigi odi, tengeneza mlango" ikiwa ina maana kama fursa hazipo zitengeneze zako, shida hatutaki kuwajibika.

Kwaiyo kama vijana tuwajibike kwenye kuleta maendeleo kwenye familia zetu tuache kufanya mambo yasiyo ya msingi hususani kutumia mitandao ya kijamii, kuongelea na kufatilia maisha ya watu, udaku na umbea na mambo mengine kadha wa kadha ambayo siyo ya msingi.

Tuache uvivu na tuwajibike kwenye kufanya kazi kwa bidii ili kizazi kinacho kuja kile matunda ya uwajibikaji wetu, tusiwe wabinafsi. Tupunguze visababu ambavyo havina msingi tuwajibike kwa asilimia 100 kwenye kila jambo haijalishi una nini au hauna nini. Tuache kupoteza mda kufatilia maisha ya watu maarufu, tufatilie maisha yetu binafsi tuta yaendeshaje.

Tuache kufatilia habari za wasanii na wana michezo kwa sababu wao wana wajibika kwenye idara na tasnia zao na wewe wajibika kwenye idara na tasnia yako, fatilia maendeleo yako binafsi unakwama wapi na una jikwamuaje kutoka apo ulipo na kwenda juu zaidi, kila kitu kina wezekana cha msingi ni kuamua na kuwajibika.

Viongozi pia wawajibike ipasavyo wawe wazalendo kwa Taifa lao, uwajibikaji wao chanya utaleta hamasa kubwa kwa vijana na wananchi kiujumla kwenye kufanya kazi kwa bidii. Mtu anafanya kazi na kuwajibika kwa bidii na nguvu zote na analipa kodi vizuri ila una kuta viongozi wengine wanatumia kodi izo kwenye mambo yao binafsi na kula na familia zao, hii sio sawa kabisa ina muumiza mtu wa chini hata hamasa ya uwajibikaji ina shuka kwa kiwango kikubwa sana.

Endapo kiongozi au viongozi hawawajibiki ipasavyo wawajibishwe ili kutokomeza tabia chafu. Uwa jibikaji mkubwa kwa viongozi na serikali italeta chachu kwa vijana na wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuwajibika ipasavyo. Kama mwananchi na kijana wa Tanzania natoa ushauri Tuwajibike bila kutegemea chochote wala mtu yeyote Mungu yupo ata tusaidia na kutushika mkono kwenye uwajibikaji wetu, tuwajibike tulete mapinduzi na maendeleo chanya kwenye nyanja mbalimbali. Usimuangalie nani kafanya nini? au nani anasema nini? "kama hawajui kula yako, hawana ujanja kwenye kuuponda utafutaji wako" .

Tusiwe kama wanyama kuongozwa ongozwa au kukumbushwa kumbushwa kila wakati, bali tuchukue jukumu la kuwajibika kwa moyo mmoja. Baba anajua wajibu wake kwenye familia alikadhalika Mama anajua wajibu wake na tuwajibike kisawasawa. Hata wewe unajua wajibu wako je, una wajibika? Tuna jua wajibu wetu kwenye familia, jamii na Taifa na Tuwajibike. " MAISHA YAKO NI WAJIBU WAKO NA UNAO UWEZO WA KUYAJENGA AMA KUYABOMOA WEWE MWENYEWE".
 
Upvote 0
Back
Top Bottom