Uwakala wa NMB bila kutumia mashine ya kutolea risiti

Uwakala wa NMB bila kutumia mashine ya kutolea risiti

Mayova

Senior Member
Joined
May 10, 2018
Posts
189
Reaction score
132
Habari za leo wakuu:

Siku hizi mawakala wapya wa NMB wanasajiliwa bila ya kupewa zile mashine za kutolea risiti badala yake wakala anafanya kupitia simu yake ya mkononi hivyo mteja anaondoka na ile risiti moja ambayo ameijaza na wakala atagonga mhuri . Kwa wazoefu hii haileti changamoto kwa wateja?

Naomba kuwasilisha
 
Iko poa tu, shida ni vile wateja hatujazoea huo utaratibu mpya, baada ya muda kila kitu kitazoeleka tu.

Hivi unakumbuka jinsi ilivyokuwa ngumu kuamini kama unaweza kutuma pesa kwa njia ya simu? Yaani unatuma pesa baada ya dakika moja unampigia uliyemtumia pesa na kumwambia kama pesa imeingia kwenye simu yake basi chap chap aende kwa wakala ikaitoe kama kweli itatoka!
 
Mhhhh hii ngumu na kama unalipa fee shule au rent hyo risit c mtasumbuana Sana nao
Maana risit locally rahis Sana kuifoj
 
Hakuna kitu kipya hapo shida n uelewa tuu fikiria ukienda unajaza jina la account, unaweka namba ya simu ya mwenye account unaweka na jina la aliedeposit na namba pia wewe ulieweka pesa unapata e-receipt na aliepokea pesa anapata e-receipt Sasa karatasi la nn hapo?

Ndio maana Mimi huwa sijaz karatas sababu naona napoteza muda tuu, napewa machine naingiza taarifa inakuwa umeisha hyo.

Tutunze mazingira yetu.
 
Huu mfumo unasumbua sana kwani mteja pia hawezi kutoa kwa Kadi ni mfumo mzuri ila mawakala tunakosa ssna biashara
Hapa umenikumbusha . Hivi kama mteja amekuja anataka kutoa pesa itakuwaje?
 
Mhhhh hii ngumu na kama unalipa fee shule au rent hyo risit c mtasumbuana Sana nao
Maana risit locally rahis Sana kuifoj
Taasisi nyingi zikiwemo shule watahamia kweny mfumo wa control number badala ya account number
 
Habari za leo wakuu:

Siku hizi mawakala wapya wa NMB wanasajiliwa bila ya kupewa zile mashine za kutolea risiti badala yake wakala anafanya kupitia simu yake ya mkononi hivyo mteja anaondoka na ile risiti moja ambayo ameijaza na wakala atagonga mhuri . Kwa wazoefu hii haileti changamoto kwa wateja?

Naomba kuwasilisha
teknolojia inachanja mbuga
 
Iko poa tu, shida ni vile wateja hatujazoea huo utaratibu mpya, baada ya muda kila kitu kitazoeleka tu.

Hivi unakumbuka jinsi ilivyokuwa ngumu kuamini kama unaweza kutuma pesa kwa njia ya simu? Yaani unatuma pesa baada ya dakika moja unampigia uliyemtumia pesa na kumwambia kama pesa imeingia kwenye simu yake basi chap chap aende kwa wakala ikaitoe kama kweli itatoka!
Umeongea vzr sema ina mapungufu wakala huwezi mlipia mtejabili wala malipo ya serikali na wateja wengine Elimu ni ndogo wanakomaa wanataka risiti za mashine .
 
Huu mfumo unasumbua sana kwani mteja pia hawezi kutoa kwa Kadi ni mfumo mzuri ila mawakala tunakosa ssna biashara
Upo wa kutoa kwa wakala anapewa token then anampa wakala ni Elimu tu itawafikia
 
Binafsi naitumia ni nzur Sanaa na dunia ndio tunaelekea huko shida ni hawajaipromote public watz wakaiamini unajua tz huduma zipo nyingi nzur ila kama mtu hajaisikia kwenye redio au TV basi anakuwa na hofu ya kuamnin
 
  • Unahitaji kuwa na mtaji wa kazi wa kuanzia Tsh milioni 2 au zaidi ambayo haitapungua kwa muda wote wa uwakala na ada ya uwakala ya Tsh 200,000 isiyorudishwa baada ya wakala kuidhinishwa na kusaini mkataba.
Rurakha Mayova naomba kujua hichi kigezo kipo katika huduma hii mpya ya nmb wakala kwa njia ya simu ya mkononi
 
Back
Top Bottom