Uwakilishi mpana wa watoto wanaobeba maua kupokea wageni wa kitaifa uzingatiwe

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Katika mapokezi ya kumpokea makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris nimeona watoto wawili(2) wa kumpokea kwa maua uwanja wa ndege, lakini nasikitika kusema itifaki haikuzingatia uwakilisho mzuri na mpana wa taifa letu.

La jana limepita ila kwa wageni wakubwa watakaofuata tena baadaye napendekeza watoto watatu(3). Mmoja wa kiume mweusi kama wa leo akiwa na suti, mmoja wa kike Mwarabu au Muhindi akiwa na hijabu na mmoja wa kike tena mweusi bila hijabu.

Hii itaonyesha uwakilishi mzuri wa makundi mbalimbali katika nchi yetu hata kama sio timilifu sana. Katika haya mapokezi ya Kamala ingewekwa hivi ingependeza na kuzidi kutuheshimisha zaidi kwa sababu Wamarekani ni watu wanaopenda sana "diversity".
 
Wageni wengine huwa wanafikia mchana, pia hawa inawezekana walila mchana.
Kwa nini kuwaweka macho watoto mpaka saa 6 usiku?
Hatuwatendei haki kabisa,huo ni utumwa mamboleo.
 
Weka picha basi
 
Umeanzisha thread over a very minor thing...which seems to bother you
 
Wakati wa JPM walikuwa watoto Aina gani? kulinganisha na sasa?
Haikuwahi kukusumbua then? Why ikusumbue now??
 
Wakristo walalamishi sana sijui kwa nini?yaani hii miaka 2 mnataka kupasuka sababu ya hijabu?kwani mkristo hawezi kuvaa hijabu?
 
picha
 
maji hufuata mkondo kaka, mengine ni ya kunyamaza tu siku ipite.
 
Kama uwakilishi haukuwa mzuri kipindi hicho pia kuna shida tukifanya maboresho awamu hii??
Wakati wa JPM walikuwa watoto Aina gani? kulinganisha na sasa?
Haikuwahi kukusumbua then? Why ikusumbue now??
 
Wakristo walalamishi sana sijui kwa nini?yaani hii miaka 2 mnataka kupasuka sababu ya hijabu?kwani mkristo hawezi kuvaa hijabu?
Umejikita kwenye dini tu, hujaona hilo pendekezo la Mwarabu, Muhindi au hata Msomali?!
 
Yoda, this is too low for you. Usijishushe kiasi hicho kwa kanzisha trivial threads.
 
Wakristo walalamishi sana sijui kwa nini?yaani hii miaka 2 mnataka kupasuka sababu ya hijabu?kwani mkristo hawezi kuvaa hijabu?

Kwanza mtu akivaa hijab anawakilisha uislam??mbona kuna wakristo Wengi wanavaa hijab??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…