Uwanja mkubwa wa kisasa wa mpira wa miguu Dodoma upo katika hatua gani?

adriz

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2017
Posts
12,207
Reaction score
26,521
Moja kwa moja..
Miaka kadhaa imepita (toka 2016) tuliposikia kuhusu ujenzi wa uwanja wa kisasa wa mpira wa miguu Dodoma unatarajia kuchukua watazamaji 80,000 na miundombinu mingine. Ikiwa kama ushrikiano wa serikali ya JMT na Morocco huku serikali ya Morocco ikiahidi kutoa fungu kusaidia ujenzi huo

Muda umepita sasa bila kupata habari zozote kuhusu maendeleo ya mpango huo ,je kuna hatua zozote gani serikali imepiga katika ujenzi wa uwanja huo na umefikia wapi?

#UziTayari
 
JPM sanamu yake inahitajika, mwaka mmoja bado anatajwa midomoni mwa watu.
 
Acha tufanye mambo ya maana, mjengewe viwanja ata michuano ya caf tu hamna huwezo wa kushiriki, hatuwezi kuteketeza mabilioni ya pesa kwenye ujinga.
 
Acha tufanye mambo ya maana, mjengewe viwanja ata michuano ya caf tu hamna huwezo wa kushiriki, hatuwezi kuteketeza mabilioni ya pesa kwenye ujinga.
Ahadi ni deni kutekelezwa muhimu
 
Picha inajieleza, tazama walivyobana mikono, walikubali tu yaishe waondoke🤣
 
Haukuhusu huo utakuwa mali ya CCM serikali itarudishiwa uwanja wake uliopo.
 
Inamana Yule mfalme wa Morocco ameshindwa kutekeleza ahad yake
 
Acha tufanye mambo ya maana, mjengewe viwanja ata michuano ya caf tu hamna huwezo wa kushiriki, hatuwezi kuteketeza mabilioni ya pesa kwenye ujinga.
Hazikuwa pesa zetu, ilikuwa msaada.. Labda ungesema hatuna vipaumbele...
 
Hazikuwa pesa zetu, ilikuwa msaada.. Labda ungesema hatuna vipaumbele...
Hizo pesa unazan unapewa na baba yako, hizo pesa za mkopo ni bora tuzielekeze kwenye sgr na bwawa la umeme.
 
Imebaki stori tu.
 
Dah kweli kabsa maana hakuna taarifa
 
Viongozi wa Tanzania ni ma comedian kumzidi hata Rais wa Ukraine. Wepesi wa kuongea mambo ambayo hawana uwezo nao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…