Wakati tunasuburi makabidhiano rasmi, na kama walivyoahidi kuwa watataja jina jipya leo. Nadhani jina sio muhimu sana, matunzo ndio muhimu kwa huu uwanja.
Uwanja wa Taifa kubatizwa kesho
na Nasra Abdallah
HATIMAYE kitendawili cha jina la uwanja mpya wa soka uliopo Temeke, Dar es Salaam, kinatarajiwa kuteguliwa kesho, imefahamika jana jijini Dar es Salaam.
Taarifa zilizopatikana jana kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, zinasema kwamba Serikali ya Tanzania itatangaza jina hilo kesho katika ukumbi wa wizara hiyo.
Habari hizo zinasema kwamba, Serikali ya Tanzania pamoja na China, zimeandaa hafla ya kuzindua jina hilo ndani ya uwanja huo, uliojengwa kwa gharama ya zaidi ya sh milioni 55.
Uwanja mpya wa Tanzania, wenye uwezo wa kubeba watazamaji wasiopungua 65,000, walioketi, ulijengwa kuanzia mapema mwa miaka 2003 na Kampuni ya China, Beijing Construction.
Uwanja huo, umetumika kwa mechi kadhaa za kitaifa na kimataifa lakini kumbukumbu itabaki Septemba mosi, 2007 wakati ambako Stars iliifumua The Cranes ya Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.
Mchezaji wa kwanza kufunga bao katika uwanja huo ni Abdi Kassim Babi, aliyepiga bao hilo katika dakika ya 52 kwa shuti la umbali wa mita kama 30.
Ulikuwa ni mchezo wa Stars wa kujipima nguvu kabla ya kuivaa Msumbiji The Black Mambaz, Septemba 8, mwaka huo ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kundi la saba kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) 2008.
Stars haikufuzu kwani siku hiyo ilipigwa bao 1-0 na Mamba hao. Bao hilo lilifungwa dakika ya kwanza, na mshambuliaji wa kimataifa wa Afrika Kusini, Tico Tico.
Source: Uwanja wa Taifa kubatizwa kesho