Uwanja Mpya Taifa na Jina Jipya

Uwanja Mpya Taifa na Jina Jipya

Mfumwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2008
Posts
1,455
Reaction score
42
Wakati tunasuburi makabidhiano rasmi, na kama walivyoahidi kuwa watataja jina jipya leo. Nadhani jina sio muhimu sana, matunzo ndio muhimu kwa huu uwanja.

Uwanja wa Taifa kubatizwa kesho
na Nasra Abdallah

HATIMAYE kitendawili cha jina la uwanja mpya wa soka uliopo Temeke, Dar es Salaam, kinatarajiwa kuteguliwa kesho, imefahamika jana jijini Dar es Salaam.

Taarifa zilizopatikana jana kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, zinasema kwamba Serikali ya Tanzania itatangaza jina hilo kesho katika ukumbi wa wizara hiyo.

Habari hizo zinasema kwamba, Serikali ya Tanzania pamoja na China, zimeandaa hafla ya kuzindua jina hilo ndani ya uwanja huo, uliojengwa kwa gharama ya zaidi ya sh milioni 55.

Uwanja mpya wa Tanzania, wenye uwezo wa kubeba watazamaji wasiopungua 65,000, walioketi, ulijengwa kuanzia mapema mwa miaka 2003 na Kampuni ya China, Beijing Construction.

Uwanja huo, umetumika kwa mechi kadhaa za kitaifa na kimataifa lakini kumbukumbu itabaki Septemba mosi, 2007 wakati ambako Stars iliifumua The Cranes ya Uganda katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa.

Mchezaji wa kwanza kufunga bao katika uwanja huo ni Abdi Kassim Babi, aliyepiga bao hilo katika dakika ya 52 kwa shuti la umbali wa mita kama 30.

Ulikuwa ni mchezo wa Stars wa kujipima nguvu kabla ya kuivaa Msumbiji ‘The Black Mambaz’, Septemba 8, mwaka huo ukiwa ni mchezo wa mwisho wa kundi la saba kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (CAN) 2008.

Stars haikufuzu kwani siku hiyo ilipigwa bao 1-0 na Mamba hao. Bao hilo lilifungwa dakika ya kwanza, na mshambuliaji wa kimataifa wa Afrika Kusini, Tico Tico.
Source: Uwanja wa Taifa kubatizwa kesho
 
Wametangaza kwamba Uwanja Mpya utaitwa UWANJA WA TAIFA na wa zamani utaitwa UWANJA WA UHURU.
 
Baba E

Wacha nirusha roho bana, wakati hata ile shule ya Ben Mkapa tumependekeza ibadilishwe jina kuonyesha hatuungi mkono viongozi mafisadi....

Mkuu Msanilo,

Jina Kamili litakuwa "The Benjamin W M National Stadium😡"
 
Wakati tunasuburi makabidhiano rasmi, na kama walivyoahidi kuwa watataja jina jipya leo. Nadhani jina sio muhimu sana, matunzo ndio muhimu kwa huu uwanja.

Uwanja wa Taifa kubatizwa kesho
na Nasra Abdallah

Habari hizo zinasema kwamba, Serikali ya Tanzania pamoja na China, zimeandaa hafla ya kuzindua jina hilo ndani ya uwanja huo, uliojengwa kwa gharama ya zaidi ya sh milioni 55.

Source: Uwanja wa Taifa kubatizwa kesho

Aissee, uwanja bei nafuu sana yaani zaidi ya sh milion 55? Yaani hata nyumba yangu imenicost zaidi ya uwanja???????? kwa nini hatuna vingi????????????????? wachina njooni mtujengee vingine kama hiyo ndio bei
 
Sikujua Nsajigwa Nsalilwe kama nawe ni fisadi ...55 Million tuambie umetoa wapi?
Nadhani typo error should read 55 Mil USD...
 
Sikujua Nsajigwa Nsalilwe kama nawe ni fisadi ...55 Million tuambie umetoa wapi?
Nadhani typo error should read 55 Mil USD...

Nduyu yangu Masalilo si uone mwenyewe magazeti yetu yanavyokosa proof reading?

Kwanini siyo 55 Mill Yen or 55 Mill Euro?

Njimba
 
sasa mbona majina yanayotajwa na inv na masanilo yanatofautiana?
 
Vipi huko mjini, wamesha confirm kwamba hayo ndo majina mapya ya viwanja vyetu?

Mkuu NL, nadhani Invisible katuandikia kuwa wametangaza kuwa Uwanja mpya utaitwa UWANJA WA TAIFA na wa zamani utaitwa UWANJA WA UHURU. Sasa sijui unahitaji cofirmation gani?. Ni kuwa magazeti yaliandika leo ndio watataja jina la uwanja mpya, na Invisible kapata hiyo habari ndio akatuwekea hapa.

Kwa kuwa naona uwanja mpya umechukua jina la uwanja wa zamani "Uwanja wa Taifa", basi ndio maana uwanja wa zamani ukapewa jina jipya "Uwanja wa Uhuru. Na hili jina la uwanja wa zamani ni zuri, manake pale ndio zilifanyika sherehe za kupata Uhuru wetu toka kwa mwingereza.
 
Thanks mkubwa,

Niliona kuna mjumbe mwingine kasema eti kasikia ule mpya utaitwa BEN NKAPA NATIONAL STADIUM...so nikaona kuana confusion hapo!
 
Thanks mkubwa,

Niliona kuna mjumbe mwingine kasema eti kasikia ule mpya utaitwa BEN NKAPA NATIONAL STADIUM...so nikaona kuana confusion hapo!

Mkuu NL, Baba Enock nadhani hajasema amesikia, bali ametoa wazo kuwa "Jina Kamili litakuwa The Benjamin W M National Stadium", nadhani anahisi baadae uwanja utabadilishwa tena jina. Sio ajabu uwanja kuwa na jina halafuukabadilishwa, ni sawa na Barabara hata shule hubadili majina.

Haya Mkuu na wakuu wengine tusubiri kuutunza uwanja wetu.

NB: Hivi Yanga anacheza lini na wacomoro, Amwanga nadhani una hili jibu Mkuu, ama mkuu yoyote?
 
Nafikiri mchezo unatakiwa kurudiwa in two weeks time tangia first leg, so nafikiri itakuwa next week hivi...(sina uhakika na tarehe)!
 
Wametangaza kwamba Uwanja Mpya utaitwa UWANJA WA TAIFA na wa zamani utaitwa UWANJA WA UHURU.

WaTZ bwana, sasa sijui walikuwa wanangojea nini muda wote huo! Jina la uwanja lilitakiwa lijulikane hata kabla ya ujenzi. Wembley mpya, Emirates, majina yalijulikana kabla. Na hata Green Point stadium (Cape Town) bado inajengewa lakini jina lipo.
 
Don't worry hiyo ni staili ya kibongo mkuu!
 
Serikali yapitisha jina la Uwanja wa Taifa Ule wa zamani sasa kuitwa uwanja wa Uhuru Anastazia Anyimike
Daily News; Saturday,February 14, 2009 @20:00

Ikiwa leo uwanja mpya wa kisasa unatarajia kufunguliwa, serikali imetangaza uwanja huo utaitwa kwa jina la Uwanja wa Taifa wakati ule wa zamani utajulikana kama Uwanja wa Uhuru.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo alisema kuwa: “Kuanzia leo (jana) Februari 14, uwanja mpya wa kisasa utajulikana kama Uwanja wa Taifa na ule wa zamani utaitwa uwanja wa Uhuru.

Alisema nia ya sekali kuita uwanja wa zamani kwa jina la Uwanja wa Uhuru ni katika kutunza historia ya Taifa. “ Uwanja wa zamani ulijengwa mwaka 1961 maalumu kwa ajili ya sherehe za Uhuru wa Tanganyika. Rais wa Tanganyika na muasisi wa Taifa letu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikabidhiwa hati za Uhuru wa Tanzania ndani ya uwanja huo Desemba 9, 1961.

Aidha, Mkuchika alisema kuwa serikali imefikia uamuzi huu wa kuzingatia kwamba matukio muhimu ya taifa yamekuwa yakifanyika uwanjani hapo ikiwa ni pamoja na maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania na sherehe za Muungano. “ Pia tukio muhimu na la kihistoria la kuwapa fursa wananchi ya kuaga mwili wa aliyekuwa muasisi wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere lilifanyika uwanjani hapo.

Kwa kuzingatia sifa hizi na nia ya serikali kutunza historia ndiyo maana tumeamua kutoa majina hayo. Akijibu swali ni kwa nini uwanja huo usingepewa jina la Rais Mstaafu wa Awamu wa Tatu, Benjamini William Mkapa kama wadau wengi walivyotaka, Mkuchika alisema: “ Rais mstaafu (Mkapa) amefanya mambo mengi makubwa katika nchi hii na kama tutaenzi kila kazi aliyofanya basi majina yake yatakuwa kila mahali.

“ Hata hivyo, tayari kuna shule ya sekondari iliyopewa jina lake, jengo la Mafuta House limeitwa kwa jina lake na pia daraja kubwa Afrika Mashariki na Kati nalo limeitwa kwa jina lake. Ninachoweza, katika kuheshimu mchango wake, kesho (leo) wakati wa ufunguzi amealikwa na amethibitisha kuhudhuria,” alisema.

Uwanja huo ambao umejengwa na kampuni ya China ya Beijing Construction Engineering Company Limited ulianza kujengwa Januari 2005 kwa ushirikiano wa Serikali ya China na Tanzania. Gharama za ujenzi wa uwanja huo ni dola za Marekani milioni 56.4 (zaidi ya bilioni 56) ambapo Serikali ya Tanzania imetoa dola za Marekani milioni 23 na Serikali ya China imetoa dola za Marekani milioni 33.4.

Aidha, Mkuchika alisema kuwa kwa sasa uwanja huo utaendeshwa na Kamati Maalumu iliyo chini ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo Dk. Florens Turuka baada ya kushindikana kupata mtu mwenye sifa za kuendesha uwanja huo.

“ Tulitoa tangazo kwa watu wanaotaka kuendesha uwanja huo na watu waliojitokeza wamekosa sifa za kupewa kazi hiyo, hivyo tumetangaza tena, lakini kwa sasa utakuwa chini ya usimamizi wa Kamati Maalumu inayoongozwa na Katibu Mkuu”. Uwanja huo unatarajia kufunguliwa leo na Rais wa China Hu Jintao aliyepewa mwaliko na Rais Jakaya Kikwete na kuhudhuriwa na Rais mstaafu Benjamini Mkapa na viongozi wengine wa serikali.
 
Back
Top Bottom