Uwanja wa Benjamin Mkapa | Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba SC Vs Plateau United

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Mabingwa wa Nchi Simba SC, Mnyama Mkali Kuliko Wote Mwituni Jumamosi ya leo Disemba 5, 2020 watakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kupapatuana na Plateau United, kutoka nchini Nigeria kwenye mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku Simba SC wakipewa nafasi nzuri ya kushinda kutokana na kupata ushindi ugenini wa bao moja bila majibu kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria kwenye uwanja wa New Jos matokeo ambayo Plateau United wakitaka kuweka rekodi ya kupindua matokeo.

Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck kuelekea mchezo wa leo amesema " Utakuwa mchezo mgumu, na mchezo ambao tumepishana kwa goli moja, hivyo lazima tuwe makini na natarajia mashabiki watajitokeza kwa wingi kushangilia. Timu yao ni nzuri hivyo tunahitaji kila aina ya nguvu ambayo tunayo ili tuweze kupata matokeo mazuri" amesema Vanderbroeck

Kulipewa Mwana... Kulitaka Mwana

Kumbuka mtanange huu wa kombe la Mabingwa Afrika ni kuanzia saa 11:00 jioni. Azam Sports 1 HD Live na Ghazwat na Jopo zima la JF litakuwa hapa Mubashara kukuletea mtanange huu kinagaubaga.

Usikose Ukasimuliwa..

Kikosi cha Simba SC;

Aishi Manula
Shomari Kapombe
Mohamed Hussein
Erasto Nyoni
Pascal Wawa
Jonas Mkude
Hassan Dilunga
Mzamir Yasin
John Bocco
Claotus Chama
Luis Miquissone

Subs;

Kakolanya
Gadiel
Ame
Ndemla
Kahata
Kagere
Morrison




 
Kila la kheri mnyama mkali ushindi ni lazima leo.
Kuna watu wamemis sana match za kimataifa hadi wanavamia za watu kujifanya wakarim sana kwa wageni.
Leo lazima tuwatie aibu kubwa vyura wasaliti wakubwa nyie.
 
Hivi sisi watanzania tuna ugonjwa gani kwani?
Ujue nimewaza sana mbona kule Nigeria tulifanyiwa kila aina ya figisu na sikuwaona wapinzani wa Plateau wale Enyimba wakiwapokea Simba wala kuwapa ushirikiano wowote kuwasaidia?

Inamaana ujinga huu tunaujua sisi tu wabongo? Hakika wanatudharau sana hawa wanigeria kwa hiki wanachokiona hapa.
 
Ni hawa hawa utopolo ndio waliokua wanamwaga maunga kule nigeria

Ule unga mbona ulionekana wazi kua ni wa bahresa
 
Kila la kheri mnyama mkali ushindi ni lazima leo.
Kuna watu wamemis sana match za kimataifa hadi wanavamia za watu kujifanya wakarim sana kwa wageni.
Leo lazima tuwatie aibu kubwa vyura wasaliti wakubwa nyie.
wamewapeleka kwa yule mganga wao ila kamati ya roho mbaya imesharekibisha mambo jamaa wanakufa mapema tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…