Uwanja wa Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL' Yanga SC Vs Namungo FC

Uwanja wa Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL' Yanga SC Vs Namungo FC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL' kuendelea kupigwa leo November 22, 2020 kwa mchezo miwili.

Kwenye Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera, Kagera Sugar inavurumishana na Mwadui FC ambapo timu zote mbili zinahitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujinasua kwenye nafasi ya chini kwenye msimamo wa VPL.

Kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Yanga SC inakwaruna na Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kombe la Shirikisho la Afrika CAF, Namungo FC.

Mchezo huu utakuwa mkali na wa kusisimua Yanga wakihitaji alama tatu ili kukaa kileleni na Namungo FC wakitaka kushinda na kusogea nafasi ya juu kutoka nafasi ya tisa huku wakitaka vilevile kuuthibitishia Umma kweli wanastahiki kuwakilisha Tanzania michuano ya Kimataita sambamba na ujio wa kocha mpya Hemed Morocco ambaye amechukua nafasi ya Thiery Hitimana.

Update;

Yanga SC na Namungo FC wamegawana alama moja moja baada ya kwenda sare ya kufungana kwa bao moja kwa moja kwenye patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League VPL'kunako Uwanja wa Benjamin Mkapa

FT; VPL' Yanga SC 1-1 Namungo FC

Screenshot_20201122-164330.jpg
Screenshot_20201122-163342.jpg
 
Update, VPL

Kagera Sugar 1-0 Mwadui FC, bao la Hassan Mwaterema kunako dakika ya 63'
 
Update..FT, VPL

Kagera Sugar wameweza kuibuka na ushindi wa bao moja bila majibu dhidi ya Mwadui FC, bao la Hassan Mwaterema kunako dakika ya 63'

Kagera Sugar 1-0 Mwadui FC
 
Update, CECAFA U20

Mchezo umemalizika kwa Tanzania kushinda jumla ya 6 kwa 1 dhidi ya Djibouti

FT; Tanzania 6-1 Djibouti
 
Back
Top Bottom