Kupitia mpira wadau wa mpira wilaya ya Misungwi mkoani mwanza wameamua kujenga uwanja mpya wa kisasa zaidi ambao uko nje kidogo na jijini la Mwanza wenye uwezo wa kubeba zaidi ya watazamaji elfu kumi na moja.
Akizungumzia kuhusu ujenzi huo ambao uko katika hatua ya mwisho meneja wa ujenzi Bw.Nyanda Mnyeti amesema kuwa walianza ujenzi kwa na mkandarasi mwingine ambaye alizungushia tofali na baadae wakapata mkandarasi mwingine ambaye alichimba na kuweka udongo ambayo unaofaa kwa ujenzi kama tofauti na awali.
Ameongeza kuwa uwanja huuo ni wa kisasa kwani ujenzi wa uwanja huo wamejifunza kupitia viwanja vya nje ya nchi ambapo maegesho ya magari yatakuwa nje wakati wa mechi huku makazi ya kocha,Viongozi na wachezaji watakuwa wanaishi karibu na uwanja ambapo kuna nyumba (Hostel) zao tayari za kuishi.
(Hii ni kwa mujibu wa tarifa za awali zizonikuliwa toka kwenye magazeti ya michezo)
Lakini leo wakati wa uzinduzi wa uwanja huo meneja Mnyeti ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema uwanja huo umegharimu kiasi cha shilingi 838,000,0000.
Akifafanua chanzo cha fedha killipopatikana kwaajili ya ujenzi huo, Mnyeti amesema alikopa Benki ya CRDB shilingi 300,000,000 kwaajili ya kujenga pitch na kiasi kingine aliuza magari yake binafsi 4, akapata shilingi 300,000,000, pia alisema alimuomba mke wake wauze gari yao ya kutembelea ndipo wakapata kiasi kilicho baki cha kumalizia uwanja huo.
View attachment 1133553View attachment 1133554