Uwanja wa gwambina unamilikiwa na nani?

Uwanja wa gwambina unamilikiwa na nani?

Shauri zako! Endelea na siasa

Kwenye hio habari kuna maneno haya
"Lakini leo wakati wa uzinduzi wa uwanja huo meneja Mnyeti ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema uwanja huo umegharimu kiasi cha shilingi 838,000,0000."

Wewe hujayaona hayo au ni msukuma wewe?
 
Mnakurupuka sana ku-quote minyuzi! Wewe mleta kaandika Bw. Nyanda Mnyeti wewe unamjadili Alexander Mnyeti!

Kuweni makini na maandishi!
Lakini leo wakati wa uzinduzi wa uwanja huo meneja Mnyeti ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema uwanja huo umegharimu kiasi cha shilingi 838,000,0000.
 
Huyu jamaa nasikia ana undugu na mama Jeska,... Ndio maana kabebwa bebwa hadi kufikia hapo,.
Sasa kama Ruangwa umejengwa uwanja,.. Kwann yeye ashindwe kujenga Mwanza,.. Mpaka kuisha miaka kumi, mtayashangaa mengi kama sio Mwanza basi Chato... Hiyo geresha tu, hamna mkopo wala magari...
 
Lakini leo wakati wa uzinduzi wa uwanja huo meneja Mnyeti ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema uwanja huo umegharimu kiasi cha shilingi 838,000,0000.
Inawezekana! Basi kuna shida kwenye uandishi wa mleta uzi! Maana mkuu wa mkoa wa Manyara anaitwa Alexander Mnyeti na si Bw. Nyanda Mnyeti kama mleta uzi alivyomwita!
 
Huyu jamaa nasikia ana undugu na mama Jeska,... Ndio maana kabebwa bebwa hadi kufikia hapo,.
Sasa kama Ruangwa umejengwa uwanja,.. Kwann yeye ashindwe kujenga Mwanza,.. Mpaka kuisha miaka kumi, mtayashangaa mengi kama sio Mwanza basi Chato... Hiyo geresha tu, hamna mkopo wala magari...
Ni kweli ni ndugu kabisa na Mama jen
 
Hongera sana Mnyeti lakini usitufanue wajinga.

Huko kukopa CRDB ni geresha tu na wanasiasa karibu wote huwa mnafanya hicho kiini macho.

Pili unauza magari manne unapata milion 300,000,000 hayo ni magari ya aina gani uliyokuwa ukimili Mnyeti mpaka used magar manne upate hiyo pesa?

Mnyeti biashara ya madiwani kule Arumeru ilikulipa sana lakini tunashukuru umewekeze kwenye jamii.
Mkuu, neno milioni linachukua nafasi ya sufuri sita; hivyo, sahihi ni milioni 300
 
Kupitia mpira wadau wa mpira wilaya ya Misungwi mkoani mwanza wameamua kujenga uwanja mpya wa kisasa zaidi ambao uko nje kidogo na jijini la Mwanza wenye uwezo wa kubeba zaidi ya watazamaji elfu kumi na moja.

Akizungumzia kuhusu ujenzi huo ambao uko katika hatua ya mwisho meneja wa ujenzi Bw.Nyanda Mnyeti amesema kuwa walianza ujenzi kwa na mkandarasi mwingine ambaye alizungushia tofali na baadae wakapata mkandarasi mwingine ambaye alichimba na kuweka udongo ambayo unaofaa kwa ujenzi kama tofauti na awali.

Ameongeza kuwa uwanja huuo ni wa kisasa kwani ujenzi wa uwanja huo wamejifunza kupitia viwanja vya nje ya nchi ambapo maegesho ya magari yatakuwa nje wakati wa mechi huku makazi ya kocha,Viongozi na wachezaji watakuwa wanaishi karibu na uwanja ambapo kuna nyumba (Hostel) zao tayari za kuishi.
(Hii ni kwa mujibu wa tarifa za awali zizonikuliwa toka kwenye magazeti ya michezo)

Lakini leo wakati wa uzinduzi wa uwanja huo meneja Mnyeti ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Manyara amesema uwanja huo umegharimu kiasi cha shilingi 838,000,0000.

Akifafanua chanzo cha fedha killipopatikana kwaajili ya ujenzi huo, Mnyeti amesema alikopa Benki ya CRDB shilingi 300,000,000 kwaajili ya kujenga pitch na kiasi kingine aliuza magari yake binafsi 4, akapata shilingi 300,000,000, pia alisema alimuomba mke wake wauze gari yao ya kutembelea ndipo wakapata kiasi kilicho baki cha kumalizia uwanja huo.

View attachment 1133553View attachment 1133554
Uongo uongo hausaidii, huwezi kopa hela benki kwa riba then ukaizike uwanjani. Mradi huo siyo kabisa au zero ROI.
 
Back
Top Bottom