Kastori Kalito
Member
- Jul 31, 2022
- 17
- 13
Swali kubwa linaloibuwa mijadala miongoni mwa jamii ni kwa namna gani inawezekana kukidhi mahitaji ya muhimu ya ki-jamii bila kuathiri uwezo wa vizazi vijavyo kukidhi mahitaji yao wenyewe. Katika miaka ya hivi karibuni kumeshudiwa uharibifu mkubwa wa mazingira asilia katika nchi ukilinganisha na miaka 40 iliyopita, hali imezidi kuwa mbaya kila mwaka kwa sababu ya kuongeeka kwa shughuli za kibinadamu kama vile kilimo cha kisasa na ukataji miti hovyo na kuongezeka kwa idadi ya watu. Hivyo ili kunusuru mazingira yetu ambayo ndiyo msingi wa uhai wa taifa letu na pia kuelekea maendeleo endelevu tunapaswa kuyatumia maeneo ya uwanja wa mbele na nyuma ya nyumba katika njia bora.
Uwanja wa mbele na nyuma ya nyumba ni nini ?
Ni eneo la kibinafsi ambalo limeunganishwa na nyumba ambapo unaweza kukuza mimea, hivyo ni nafasi yote ya wazi inayozunguka nyumba ya makazi ya familia huska. Eneo hili hujumuisha sehemu ya mbele na nyuma ya nyumba ya makazi. Eneo hilo linafaa kupandwa kilimo mseto ikijumuisha mazao ya mda mfupi na mrefu na miti bila kujalisha ukubwa wa eneo lenyewe, upandaji huu unaweza kuhusisha vipande vya bustani za kuliwa kama vile matunda, mboga na bustani za viungo. Kwa ujumla yadi inaweza kupandwa mimea ya matunda, mazao ya mboga, mimea ya viungo, mimea ya dawa, mazao ya wanga, mimea ya viwanda, malisho, kuni na malighafi za ufundi wa kawaida.
Uwanja wa mbele na nyuma ya nyumba unaweza kutumika kwa kilimo mseto na kufanyika kuwa sehemu ya kipande cha ardhi cha uhifadhi kilimo-bioanuwai kutoka mbali na eneo lake la asili kupitia kilimo pamoja na misitu na kilimo pamoja na ufugaji samaki. Hivyo mfumo huu unaweza kutimiza kazi ya kiikolojia zenye tabaka nyingi la muundo wa mimea, inayofanana na misitu ya asili na kutoa makazi na fursa kwa ajili ya anuwai jamii ya mimea ya porini na wanyama.
(Picha no,1 sehemu ya nyuma ya nyumba ya makazi iliyopandwa mhogo, na mipapai. Chanzo, mwandishi)
(Picha no,2 sehemu ya nyuma ya nyumba ya makazi iliyopandwa mhogo, na pilipili kichaa. Chanzo, mwandishi)
View attachment 3.JPG
(Picha no,3 sehemu ya nyumba ya makazi iliyopandwa mauwa, uoto wa majani, miti mifupi na mpapai . Chanzo, mwandishi).
Miongoni mwa faida za uwanja wa mbele na nyuma ya nyumba kwenye makazi ni pamoja na;
Kupendezesha na kulinda mazingira
Eneo hili linaweza kuwa sehemu ya ufugaji mdogo kama vile kuku, bata, kanga, mbuzi, pia kupanda mazao ya mimea, mauwa, matunda, mimea tiba na mimea mbalimbali na katika maumbo mbalimbali kama mstatili, pembe tatu na hivyo kupendezesha mazingira ya nyumbani lakini na kulinda mazingira pia.
Kuchangia usalama wa chakula na kuinua kipato cha kaya/familia
Mazao ya chakula na mifugo ikiwemo mazao kama mboga, nafaka, matunda, nyama na mayai kutoka uwanja wa mbele na nyuma ya nyumba ya makazi vianaweza kusaidia usalama wa chakula, kutoa virutubisha na pia kuuza ziada kujipatia kipato kwa ajili ya kukidhi mahitaji mengineyo ya familia.
Kuboresha afya za wanafamilia na jamii kwa ujumla
Mazao yanayolimwa katika eneo hilo yaweza kuoteshwa kwa kutumia samadi na mbolea zingine asilia na pia kukinga wadudu waharibifu kwa njia za asili au za kibiologia hivyo mazao ya chakula yanayoopatikana kutokea maeneo hayo ni salama kwa afya ya mlaji na hutoa virutubisho visivyokuwa na vimelea vya sumu za viwandani. Hivyo vyakula hivyo huimalisha afya na kuimalisha kinga ya mwili.
Nguzo kuu ya hekima ya jadi /familia/jamii
Sehemu ya utamaduni wa familia ambapo kupitia shughuri za kilimo na ufugaji zinazofanyika katika eneo hilo huwa mhimili wa hekima ya jadi na hekima hii huweza kupitishwa kutoka kizazi hadi kizazi cha familia au jamii kupitia mdomo na mimea na wanyama vinazopatikana nyumbani
Nyenzo ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi
Mabadiliko ya tabia ya nchi yanachangia kuongeza kwa joto , kuleta athari za ki afya, lakini pia kupunguwa kwa uwezo wa uzalishaji chakula. Hivyo eneo hilo likioteshwa jamii ya mimea na mazao mseto inawaeza kuunda hali ya hewa ndogo ambayo ni hali ya hewa ya kawaida ya eneo la kawaida katika eneo dogo au makazi huska.
Chanzo cha ajira na kuboresha kipato kwa familia/kaya
Katika wakati huu ambao idadi ya watu inaongezeka na ajira zinakuwa finyu hivyo eneo hilo linaweza kuwa chanzo cha ajira kwa wanafamilia na kupitia kuuza ziada ya mazao yaliyopandwa au kufugwa inaweza kuinua kipato cha familia na kumudu gharama za maisha.
Kuimarisha mzunguko wa hidrologia ya maji na kutunza udongo
Mabadiliko ya tabia ya nchi yamechangia mabadiliko katika mzunguko wa hidrologia ya maji ambapo moja kwa moja imechangia katika mvua zisizokuwa za uhakika na mtawanyiko usio sawia. hivyo kwa kukubali mfumo wa upandaji mimea na mazao asilia katika eneo hilo la makazi inaweza kuchangia kuboresha mvua na kutunza udongo katika hali yake ya asili.
Uwezekano wa wazo hili;
Ili kufikia manufaa endelevu, serikali za mitaa, za majiji na miji midogo kwa kushilikiana na wadau wa maendeleo wanapashwa kuendesha kampeni ya elimu zaidi miongoni mwa jamii juu ya mfumo/kitendo hicho kuelekea maendeleo endelevu. Pia serikali kuu kuja na sera elekezi.

- Uwezo wa serikali za mitaa na mamlaka za miji na majiji kupitisha sheria ndogo na kuweka utaratibu juu ya jamii kupokea mfumo huu
- Vyombo vya habari kutoa elimu kwa jamii juu ya matumizi ya maeneo hayo kama bustani asili katika makazi.
- Serikali kuu pamoja na wadau mbalimbali kutoa ruzuku kwa kila mwaka kwa familia itakayopokea na kuendeleza mfuo huo kwa viwanjo stahiki.
- Tayari jamii imeshudia na kuonja madhara ya mabadiliko ya tabia ya nchi kama vile kuongezeka kwa joto, ukame, upungufu wa mvua na uzalishaji hafifu wa chakula mashabani hivyo kuwa tayari kupokea mfumo huo rafiki.
- Uwepo na ushilikishwaji wa taasisi za elimu

Upvote
8