Uwanja wa Mkapa | Kombe la ASFC, Simba SC 2 - 1 Kagera Sugar

Uwanja wa Mkapa | Kombe la ASFC, Simba SC 2 - 1 Kagera Sugar

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) linapigwa leo Mei 1, 2021 kwenye Uwanja wa Mkapa, ambapo Mabingwa Watetezi, Simba SC wanakwaruzana na Kagera Sugar katika mchezo wa hatua ya 16 ya michuano hiyo.

Kwenye mchezo wa leo Mnyama Mkali Mwituni, Simba SC anapewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana rekodi za hivi karibuni na vile vile kuwa na Kikosi bora ambacho kinatanya vizuri kwenye michuano mbalimbali kuliko Kagera Sugar. Je Kagera Sugar wataweza kutibua hiyo rekodi?

Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Gumzo Hapo Ndipo.

========

Naaaam mpira umeanza uwanja wa Mkapa.

15' Mchezo ni mkali Wanaume hawa wanapambana lakini Simba SC wanamiliki mpira huku wakikosa nafasi nyingi zaidi kuliko Kagera Sugar

25' Kagera Sugar hawajaleta hatari zaidi kwa Simba, kama ambavyo Simba SC wanajaribu kutafuta bao

Simba SC 0-0 Kagera Sugar

40' Free Kick kuelekea Kagera Sugar, anapiga Wawaaaaa, golikipa anatema shuti lile.

42' Kagera Sugar wanakosa utulivu wa kuweka wavuni mpira, Mayanga alifanya kazi nzuri ya kumpiga chenga Wawa.

Golikipa wa Kagera Chalamanda anaonyeshwa Kadi ya Njano kutokana na kupoteza muda.

45' Goooooooooooooooooooooal

Erick Mwijage anaipatia Kagera Sugar bao la kwanza akiunganisha krosi ya kichwa

Simba SC 0-1 Kagera Sugar

Vitals Mayanga anaonyeshwa Kadi ya Njano baada kuzuia mpira usipigwe.

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Kagera Sugar wapo mbele kwa bao moja.

HT, ASFC; Simba SC 0-1 Kagera Sugar

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa, na Ametoka Taddeo na ameingia Morrison upande wa Simba SC.

Free Kick kuelekea Kagera Sugar, anapiga Chamaaa loooooo golikipa anatema na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

54' Ametoka Bwalya na ameingia Bocco upande wa Simba SC

55' Morrisoon Gooooooooooooaaal Gooooooaaal

Bernard Morrison anaipatia Simba bao la kusawazisha kazi nzuri ya Miquissone.

Simba SC 1-1 Kagera Sugar

Miquissone anaachia shutiiiiii kali, lakini mpira unatoka nje na kuwa Goal Kick.

67' Kagere Goooooooooooooaaal Gooooooaaal

Maddie Kagere anaipatia Simba SC bao la pili, akipokea pasi safi kutoka kwa Morrison

Simba SC 2-1 Kagera Sugar

Ametoka Mwijage na ameingia Seseme upande wa Kagera Sugar. Na ametoka Maddie Kagere na ameingia Nyoni upande wa Simba SC

80' Ni wakati wa Biriani.. kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi.

Namna gani Bocco, nafasi mbili za wazi anakosa kuandika bao..!

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo wa ASFC uwanja wa Mkapa

Simba SC wanamiliki mpira huku wakipiga pasi za hapa na pale.

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Kagera Sugar na kutinga robo fainali.

FT, ASFC; Simba SC 2-1 Kagera Sugar

Ghazwat
 
10' Kagereeeee loooooo anakosa..Hii ilikuwa nafasi kwa Simba SC na faida kwa Kagera Sugar

Simba SC 0-0 Kagera Sugar
 
bwalyaaaa.. golikipa kaicheza
 
mipira ya kagere haifiki lengo
 
kona ya kwanza dk22 wanapata kagera
 
39' Golikipa wa Kagera Sugar anacheza kazi sana amesaidia kuweka salama lango lake

Simba SC 0-0 Kagera Sugar
 
Back
Top Bottom