KwetuKwanza
Member
- Mar 13, 2023
- 82
- 150
Uwanja wa michezo Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, ambao utumiwa na wanamichezo mbalimbali, Sasa unatumika kuhifadhi mifugo kama ngo'mbe, mbuzi, na kondoo pia.
Taarifa zinasema kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo Simon Simalenga, ameufanya uwanja huo kuwa zizi, baada ya kuamua kuhifadhi mifugo ambayo inakamatwa ikichungiwa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa katikati ya mji wa Bariadi.
Nimeshuhudia Leo ndani ya uwanja huo, huku ukiwa umefungwa mageiti yote, kundi kubwa la ngo'mbe likiwa linazurura uwanja mzima, wakiwemo na vijana wawili ambao ni walinzi wakiwa wamelala.
Eneo la kuchezea, nalo limejaa kinyesi Cha ngo'mbe, huku baadhi ya maeneo kikiwa kimekusanywa.
Inaelezwa kuwa Mkuu huyo wa Wilaya ameanzisha opereisheni ya kukamata mifugo inayochungiwa kwenye maeneo yasiyoruhusiwa katikati ya Mji wa Bariadi, na mifugo yote inayokamatwa inapelekwa kwenye uwanja huo.
Ikifika wakati wa Jioni, hao vijana wawili wanaolinda mifugo hiyo, uwafungulia wanamichezo kwa ajili ya kufanya mazoezi, huku mifugo hiyo ikiendelea kuzagaa huku na kule.
Wachezaji kuendelea kufanya mazoezi huku mifugo ikiendelea kuwa ndani na ikizagaa kila sehemu, haileti Afya kwao lakini pia uwanja mzima umejaa kinyesi.