Uwanja wa Mpira Dodoma Utagharimu Bilioni 310. Utabeba Watazamaji 32000

..BILLIONI 310?

..sio sahihi hata kidogo.

..tulitaka nani wajenge? Hata CCM wana viwanja vya mpira, ikiwemo Kirumba.
Wewe utajenga kwa shilling ngapi? weka kiasi unachodhani ni sahihi tujadili. Kama wewe ndio mkandarasi utaweka kiasi gani tupe hapa tujuwe.
 
Faida ipi kwa taifa bora wangenunulia matrekta wagawieni vijana
-Watanzania wanapenda soka.
-Asilimia zaidi ya 70 ya maongezi ya watanzania wanajadili mpira.
-Media karibu zote zinauza zaidi habari zinazojadili mpira kuliko chochote.

-Hakuna event yeyote inayoweza kuwaleta watu pamoja 60,000+ wakiwa wamejilipia wenyewe zaidi ya soka..sio siasa, sio muziki, sio dini, nk

Acha wapewe wanachokitaka.
 

..katika nchi zilizoendelea na zinazojitambua viwanja vya michezo humilikiwa na makampuni binafsi.
 
Wewe utajenga kwa shilling ngapi? weka kiasi unachodhani ni sahihi tujadili. Kama wewe ndio mkandarasi utaweka kiasi gani tupe hapa tujuwe.

..hoja yangu ni kwamba tungeweza kutumia BILLIONI 310 kwa mambo na vipaumbele vya maana zaidi.
 
..hoja yangu ni kwamba tungeweza kutumia BILLIONI 310 kwa mambo na vipaumbele vya maana zaidi.
Nchi ina watu Mil 68 hatuwezi kuwa na vipaumbele vilivyofanana, miundo mbinu ni muhimu sana katika nchi yoyote na viwanja vya mpira ni muhimu sana tu kama yalivyokuwa mambo mengine muhimu. Michezo ni ajira na assets huu uwanja utaingiza mapato japo kuwa sio malengo kuwa biashara lakini unaingiza. Hatuwezi kuwa na nchi tuna viwanja vibovu, sisemi kama hakuna mambo mingine muhimu lakini tukianza hivi basi kesho nitasema SGR haina umuhimu bora tufanye vitu vingine siku nyingine tutasema ndege sio muhimu na haitaisha.

Kikubwa kila jambo linatengewa budget yake sasa kama kuna la muhimu lilitakiwa lisemwe litafutiwe budget. miundo mbinu kwa nchi yoyote muhimu na uwanja wa michezo ni muhimu ndio maana huwezi kwenda mkoa wowote Tanzania hii ukakosa uwanja wa michezo.
 

..hata kama tunataka kuinua michezo sio busara kutumia BILLIONI 310 kujenga kiwanja kimoja cha mpira.
 

..bajeti ya kilimo ni Billion 970.

..ujenzi uwanja wa mpira Billion 310

..(310÷970) × 100 = 31.96%.

..sidhani kama ni busara kutumia fedha sawa na 32% ya bajeti ya kilimo kujenga uwanja wa mpira.

Cc Nguruvi3
 
Lazima mzubaishwe

Ova
 
..bajeti ya kilimo ni Billion 970.

..ujenzi uwanja wa mpira Billion 310

..(310÷970) × 100 = 31.96%.

..sidhani kama ni busara kutumia fedha sawa na 32% ya bajeti ya kilimo kujenga uwanja wa mpira.

Cc Nguruvi3
Mkuu, Waafrika tuna namna zetu za kufikiri. Sad!
 
Huwa sielewi kwa nini hatufikirii miaka 30 ijayo population ya Tanzania itakuwa na watu millioni 150 huo uwanja utakuwa mdogo sana
 
Watanzania tunazidisha sifuri kwenye Mali zetu ni kama tumerogwa wenzetu washatoka kujenga viwanja vyenye ubora huu wamehamia kujenga kama kiwanja cha Bernabeu Estadio sisi hivyo hivyo vya zamanj bado tunaibiana kweli...
 
..bajeti ya kilimo ni Billion 970.

..ujenzi uwanja wa mpira Billion 310

..(310÷970) × 100 = 31.96%.

..sidhani kama ni busara kutumia fedha sawa na 32% ya bajeti ya kilimo kujenga uwanja wa mpira.

Cc Nguruvi3
Kilimo hiyo ndio budget yake imepangwa kutokana na mahitaji yake kwa mwaka haijapunguzwa kutokana na ujenzi huu pia hiyo 970 Bill ni kwa mwaka kwa miaka miwili almost 2 Trillion hiyo 310 ya kiwanja ni total cost 310 Billion ujenzi wa miaka miwili kwa maana hiyo mwaka inatoka 155 Billion so hesabu zako sio sawa.
 

..OK.

..ngoja niweke mahesabu vile unavyotaka.

..Je, ni busara gharama za ujenzi wa uwanja wa mpira kuwa sawa na asilimia 15% ya bajeti ya kilimo?

..Zingatia kwamba kilimo ndio sekta inayogusa watu wengi zaidi hapa nchini.
 
..OK.

..ngoja niweke mahesabu vile unavyotaka.

..Je, ni busara gharama za ujenzi wa uwanja wa mpira kuwa sawa na asilimia 15% ya bajeti ya kilimo?

..Zingatia kwamba kilimo ndio sekta inayogusa watu wengi zaidi hapa nchini.
Sio kila mtu mkulima kuna gari bei kubwa kuliko nyumba utasema gari muhimu kuliko nyumba. wizara ya kilimo ina budget yake pesa ya uwanja haijatoka kwenye budget ya kilimo shida iko wapi? mchezaji mpira analipwa kuliko Dr au Eng sio issue kawaida tu. Hatuwezi sote kuwa wakulima tu sasa kwa wewe mkulima umepunjwa nini? wewe kila mwaka una budget 970 billion uwanja ni miaka miwili tu sasa chukuwa life span ya uwanja chukuwa pesa hiyo gawa ndio thamani yake.
 

..mradi wa kilimo cha umwagiliaji ungekuwa na faida kuliko uwanja wa mpira wa billioni 310.

..nchi hii ina wacheza mpira wangapi, na wakulima wangapi, mpaka tutumie fedha zote hizo kujenga uwanja wa mpira badala ya kuwainua wakulima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…