Uwanja wa ndege kukodishwa Wachina

Uwanja wa ndege kukodishwa Wachina

Hii nchi imeoza sana, mkapa aliuza kila kitu kwa bei rahisi ili apate 10% yake, sasa naona mkuu wa kaya anataka kumalizia vitu vichache vilivyobakia.

Hii hatari kabisa kwa nchi yetu, management zetu ni nzuri tatizo ni kuingiza ufisadi ndani yake bila kufuata ethic za biashara ndo maana kila sehemu ni hovyo.
 
Mkuu GT,
Labda mimi niko outdated kidogo lakini swala comoro tulidicuss na tukapata clarification kutoka serikalini kuwa gharama ni AU na sio serikali ya Tanzania, samahani naomba clarification kama kuna habari mpya, maana itakuwa hajabu kama serikali yetu inagharamia vita wakati madara ni issue kujenga.
 
It seems this has now become a common thing for Tanzania nowadays.

Why do we need mbia? Did they ask local investors for participation au ndio kule kutoa zabuni na miradi dizaini ya Kiwira na Richmond?

Mpaka lini Serikali yetu na watendaji wake wataendelea kufanya mambo kama vibaraka kwa manufaa ya hawa wabia na wawekezaji?

Je hatujajifunza kutokana na TRL?
 
Guys i think this is quite right, kwakweli ni aibu mno kuona viwanja vya ndege vingi ulimwenguni kwa sasa vikiwa vya kisasa zaidi, kuanzia na ASIA,America,Europe na mwishowe ni huku kwetu!

Kwa afrika ya mashariki, Entebbe waliufanyia marekebisho wa kwao na kujenga termina nyingine mpya ambayo walau kidogo inapendeza na ni mwaka jana alipokuja malkia wa Uingereza na Brown kwenye commonwealth head of states meeting lakini pia nenda kaangalie Jomo Kenyatta sio sawa na wakwetu kabisa kinachosikitisha wakati mwingine ukiwa umekaa kwenye lounge umeme unakatika na ni adha kubwa kweli.
Nimetoka jana Lagos - Mohamed Mutalla airport na kwakweli jamaa wameubadilisha pia, nilikuwa huko last year!
Ninachojaribu kusema ni kuwa, there are alot of changes that our african airports are trying to do at the moment including having new premises and runways! Tanzania tunahitaji kwa hali na mali, moja kwa utalii wa nje na ndani, biashara na mengineyo yatakayo ajiri watanzania wengi mno.
Si mbaya kupata mwekezaji ambaye ataufanya uwe wa kisasa zaidi, airport nyingi tu zimefanyiwa ubinafsishaji tunachohitaji kutoka kwa viongozi wetu ni kuhakikisha mageuzi haya yanafanyika yakituacha na kitu badala ya hohehahe.
I trust JF, tuseme ubinafsishaji upite ila ufisadi kwenye hii project usiwepo kwa level yoyote ile!
Aviation industry is a driving force to boosting our tourism industry if is managed with professionals and honesty!

I am not sure if I follow your line of thinking here, but let me ask you, kudorora kwa uwanja wetu wa ndege unafikiri chimbuko lake ni nini?
 
Ni mfanyabiashara gani anaanza na kujenga VIP? kupenda dezo kutatutokea puani!

Fundi,

Utashangaa wakijengewa hiyo VIP lounge wakaambiwa walipie vinywaji, chakula na huduma nyingine wataanza kulalamika!

There is no VIP lounge anywhere in international airports I have been that is free of charge.

Labda jingine la kuuliza, what do they mean by VIP lounge? Maana huku kwenye VIP lounge utakutana na Wabunge na hata mawaziri kama hawatumii ndege za Serikali.

Sasa sisi VIP lounge ni ya vigogo au iendane na wale ambao wanasafiri kwa daraja la juu na wenye uwezo wa kulipia huduma za gharama za VIP lounge?

This whole thing of privatisation and even the focus on VIP lounge it seems like bs.

What we need is competitive management, that is free of vi-memo na kuingiliwa na Serikali. Let the damn airport run as an airport and business center!

Wanataka kujenga VIP lounge ya watu 300, wakati haitatumika kwa capacity ya watu 300, ila mara 5 kwa mwaka! what wastage of time and resources!
 
Tutasalimika ? Hawa jamaa si waaminifu kabisa .Kwa wakiuchukua huo uwanja wataurudisha lini ? Mbona nimeanza kuogopa ? Kama kweli issue ni kuiga what others does mbona hatuigi kwa haraka kuwapeleka mahakamani akina Chenge na watu wa EPA ?Jamani nisaidieni .

Lunyungu,

Hivi umesikia lini Heathrow, Gatwick, JFK, LAX, Ohare, Schippol, Chang Kai Shek na viwanja vingine vya ndege vinakuwa ni ubia?

Leo hii na woga wa ugaidi wa kuteka ndege na kusambaa kwa biashara haramu za madawa na mambo mengine tunataka kutoa ubia na kumpa mwekezaji?

Tumewapa wahindi TRL wameshindwa, Makontena bandarini yametushinda, sasa tunataka toa uwanja wa ndege!

Tubinafsishe hata Ikulu basi, maana tumeshindwa kuwa makini na proffesionals!
 
Rev,
I am with you on this one! Wachina wana track record gani katika uendeshaji wa viwanja vya ndege? Worse still, utasikia wamekodishwa kwa miaka 25 au hamsini ( kama walivyofany Mlimani Project na KIA!) na hakuna chochote bali kujenga VIP kwa ajili ya waheshimiwa wabunge. Hili ni bomu lingine tunaloingia kichwa kichwa.
 
Kuna mambo mengine nchi hii ukiyasikia tu tangu mwanzo unaanza kuhisi harufu ya rushwa, ufisadi na "inefficiency".

Hao wachina wamejenga barabara ya Sam Nujoma chini ya kiwango kinachotakiwa, na pia wameshindwa kuikamilisha ndani ya muda unatakiwa.

Haya Wahindi wa TRL wamepewa shirila la reli huku proposal yao ikiwa inatakiwa iwe "backed up" na serikali kwa dola milioni karibu 10. Yaani nilisilia Pinda akielezea kwamba Serikali inatakiwa kutoa dola milioni 10 katika uendeshaji wa shirika (kwa kuanzia), ili hao wahindi wapewe mkopo wa dola milioni 35 toka IFC!!! Kwa kifupi wamekuja mikono mitupu, na makaratasi tu mikononi, wakapewa tenda. Wameshaleta vichwa 9 vya treni toka India ambavyo ni vichakavu na mabehewa machakavu kadhaaa.

Wana mpango wa kuing'a reli yetu tuliyoachiwa na Mjerumani yenye chuma halisi, halafu wafunge nyingine ambayo naambiwa na wataalamu kwamba itakuwa ya 'aluminium'...inaweza kudumu kwa miaka 25 tu kisha wataondoka watuachie makapi!! Vyuma vya reli watayoing'oa watavipeleka kwenye viwanda vya kuyeyushia vyma chakavu na kujipatia mamilioni ya dola.

ATC wamekodi Air Bus 320 kwa dola 350,000 kwa mwezi "dry lease"...... Wakati Precision Air wamekodi Boieng 737 -300 kwa dola 100,000 kwa mwezi!!!

Kwa hesabu za haraka haraka, ATC watashindwa kulipa hiyo bili.....! Na kuna harufu ya ufisadi hapo!!!!

Tusubiri na tuone!!! Ila ndio nchi yetu hii , tutakwenda wapi?
 
Back
Top Bottom