Uwanja wa Simba Bunju Wanoga

Uwanja wa Simba Bunju Wanoga

ZionGate

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
6,362
Reaction score
2,991
Wakati wowote Simba itaanza kujifua kwenye uwanja wake ulioko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam baada ya kukamilika kwa uwanja wa nyasi asili

Kwa sasa matengenezo ya vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji ndio yanayoichelewesha Simba kuhamia Bunju
Lakini mpaka mwisho wa mwezi huu Simba itaanza rasmi kutumia uwanja wake na kuepukana na gharama za viwanja vya kukodi

Aidha ujenzi wa uwanja wa nyasi bandia unaendelea ambapo baada ya matengenezo ya awali, zoezi la kutandika nyasi ndio linalofuata

Hii ndio Simba ambayo wengi walikuwa wakiisubiri kwa hamu

Kwani lilikuwa jambo la aibu kwa klabu kongwe kama Simba kutokuwa na uwanja hata wa mazoezi

Baada ya kukamilika awamu ya kwanza, awamu ya pili itawashirikisha Wanasimba wote ambapo ujenzi wa majukwaa pamoja na miundombinu mingine utafanyika
Lengo likiwa kuhakikisha uwanja huo unaweza kubeba kuanzia mashabiki 10,000 na kuendelea

bunju_simba.jpeg
 
Kwahiyo huu uwanja utakuwa wa mazoezi tu au hadi match zitapigwa
 
Hongera kwa Mo kufanikisha ili maana wengine huu uwanja walishaanzisha michakato ya kupiga pesa kwa kisingizio cha uwanja wa bunju
 
Hapa ndio inaonekana tofauti ya mjinga na muelevu.Wakati huyu anawaza maendeleo ya timu huku WAPUUZI FC wanawaza kurogana.
 
Tanzania bado kuna safari ndefu sana ktk suala zima LA maendeleo endelevu.
Timu za Simba NA Yanga kama zingekuwa kwenye nchi zingine hadi Leo hii ndio zingekuwa timu "bilionea" KWA ukwasi WA pesa. Kununua tu kiwanja basi Watz wameona kama timu imeendelea sana kumbe Ni majanga tupu.Kutokana NA ukongwe WA timu hizi, mpaka sasa ingekuwa hata NA viwili kikubwa vya kuweza kuchukua watazamaji angalau 45,000 kwenye kila mji mkubwa hapa nchini Tz.
 
Tanzania bado kuna safari ndefu sana ktk suala zima LA maendeleo endelevu.
Timu za Simba NA Yanga kama zingekuwa kwenye nchi zingine hadi Leo hii ndio zingekuwa timu "bilionea" KWA ukwasi WA pesa. Kununua tu kiwanja basi Watz wameona kama timu imeendelea sana kumbe Ni majanga tupu.Kutokana NA ukongwe WA timu hizi, mpaka sasa ingekuwa hata NA viwanja viwili vikubwa vya kuweza kuchukua watazamaji angalau 45,000 kwenye kila mji mkubwa hapa nchini Tz. KWA kuwa vichwani KWA Watu weusi wengi hakuna kitu matokeo yake ndio hivi tena
 
Back
Top Bottom