ZionGate
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 6,362
- 2,991
Wakati wowote Simba itaanza kujifua kwenye uwanja wake ulioko Bunju nje kidogo ya jiji la Dar es salaam baada ya kukamilika kwa uwanja wa nyasi asili
Kwa sasa matengenezo ya vyumba vya kubadilishia nguo wachezaji ndio yanayoichelewesha Simba kuhamia Bunju
Lakini mpaka mwisho wa mwezi huu Simba itaanza rasmi kutumia uwanja wake na kuepukana na gharama za viwanja vya kukodi
Aidha ujenzi wa uwanja wa nyasi bandia unaendelea ambapo baada ya matengenezo ya awali, zoezi la kutandika nyasi ndio linalofuata
Hii ndio Simba ambayo wengi walikuwa wakiisubiri kwa hamu
Kwani lilikuwa jambo la aibu kwa klabu kongwe kama Simba kutokuwa na uwanja hata wa mazoezi
Baada ya kukamilika awamu ya kwanza, awamu ya pili itawashirikisha Wanasimba wote ambapo ujenzi wa majukwaa pamoja na miundombinu mingine utafanyika
Lengo likiwa kuhakikisha uwanja huo unaweza kubeba kuanzia mashabiki 10,000 na kuendelea