Uwanja wa Sokoine | Vodacom Premier League (VPL) Tanzania Prisons Vs Simba SC

Uwanja wa Sokoine | Vodacom Premier League (VPL) Tanzania Prisons Vs Simba SC

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kuvurumishwa leo Jumapili ya Juni 28, 2020 kwenye Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya, ambapo wenyeji Tanzania Prisons wanawakabili vinara wa ligi hiyo Wekundu wa Msimbazi, Simba SC.

Mchezo wa leo unatarajia kuwa mkali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku Tanzania Prisons wakisema hawatakubali kuwa ngazi ya Simba SC kutangazia ubingwa kwao ambapo Simba SC ikihitaji alama moja tu kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga wala Azam FC ili aweze kuchukua ubingwa wa VPL kwa mara ya tatu mfululizo.

Kwa upande wa Kocha wa Prisons Mohammed Adolph Richard amesema;

" Tunajua wakitufunga watakuwa mabingwa na hatutaki litokee hilo kwetu, hivyo tutapambana kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi ili kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi kwani hata sisi hatuko salama" amesema Adolph.

Naye Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck amesema;

" Nina uhakika kesho (leo) tutacheza mchezo mzuri, kila mchezaji yupo tayari kwa mchezo na hilo ni jambo nzuri kwa kocha kuchagua mchezaji yeyote. Tutacheza kushinda na kama matokeo yakiwa chanya tutapata kitu cha ziada na hilo ndo lengo letu" amesema Sven.

Nani kuibuka mbabe? Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 10: 00 jioni, Usikose Ukaambiwa..!

....Ghazwat.. Ghazwat ....Nikiwa na Team Mnyama Mkali OKW BOBAN SUNZU sembo mmteule Viol King Ngwaba Shunie Van pebles Raynavero Troisième Ceil kenge 10 NAWATAFUNA Mtoto halali na hela Kinyungu mozila firefox Dam55
Screenshot_20200628-092229.jpg
Screenshot_20200628-081147.jpg


View attachment 1491102[/B]

00' Naaaam Mpira umeanza uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya VPL

Tanzania Prisons 0-0 Simba SC


25' za kipindi cha kwanza hakuna bao kwa pande zote mbili huku kila timu ikijaribu kupenga lango la mpinzani wake bila mafaniko

Tanzania Prisons 0-0 Simba SC

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko VPL uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya

Naaaam mpira ni mapumziko huku kila timu zikitoka bila kufungana kipindi hiki cha kwanza licha kila timu kujaribu kujenga mashambulizi ambayo hayakuzaa mabao.

HT, VPL; Tanzania Prisons 0-0 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza vema uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya VPL

Huku Simba wakifanya mabadiliko na ametoka Ajibu, ameingia Cloutis Chama

Mchezo ni mashambulizi kwa pande zote mbili, Tanzania Prisons wakikosa umakini wanapofikia lango la Simba na Simba SC wajaribu kupenya lango la Tanzania Prisons bila mafaniko

67' Mabadiliko upande wa Simba SC, ametoka Hassan Dilunga, ameingia Luis Miquissone

70' Tanzania Prisons 0-0 Simba SC,

Bado Simba SC wajaribu kujenga mashambulizi eneo la Prisons huku Prisons katikati wakiimarika

Kichwa cha Maddie Kagere linashindwa kulenga lango la Prisons, oooooh ilikuwa hatariiiii lango la Prisons na nafasi kwa Simba kuandika bao

80' Ametoka Miraji Athumani na ameingia John Bocco upande wa Simba SC

90+6' Kuelekea kumalizika kwa mtanange huu wa VPL uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.

Naaaam Mpira umekwishaaaaaaa ambapo Simba SC, wanatangaza ubingwa kwani walihitaji alama moja tu kufikisha alama 79 ambazo haziwezi kufikiwa na Yanga wala Azam FC

Tanzania Prisons wanashindwa kuwazuia Simba kutangazia ubingwa hapa, kinachoelekea ni kugawana pointi moja kwa moja hii ni faida kwa Simba SC

FT, VPL Tanzania Prisons 0-0 Simba SC

.... Msimulizi wako Ghazwat....
 
Naaaaaaaam ni Mabingwa wa nchi Mnyama mkali Simba sc atakapo ungurumaa kule Mbeyaaaaa na kutwaa Ubingwa kwa mara ya tatu mtawaliaaaaa.

Tunawakaribisha De Mkunungu na wengine wote kwenye sherehe zetu za ubingwa.
Simba nguvu moja
Simba bingwa 2019/2020
 
Back
Top Bottom