barafuyamoto
JF-Expert Member
- Jul 26, 2014
- 32,378
- 29,739
Ilikuwa shot on target hivyo ni goli la Kichuya.David Mwasa kajifunga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ilikuwa shot on target hivyo ni goli la Kichuya.David Mwasa kajifunga
Soka la kifaransa hiloSimba wanacheza vizur Sana hadi raha
Bado unawaombea kila la kheri [emoji23] [emoji23]HAHAHA KAWAIDAAA
Soka safi mkuu tunapata goli la3Soka la kifaransa hilo
Angalau tuhamie upande huu maana jukwaa la siasa sio!Leo ni kiputwe cha ligi kuu soka Tanzania Bara ambapo wekundu wa msimbazi Simba inawakaribisha Mbao FC kutoka jijini Mwanza.
Mbao ikiwa kama timu iliyoleta changamoto kwa Timu kubwa za Kariako yaani Simba na Yanga ambapo yanga Tayari kashachezea msimu huu kwa goli 2.
Kwa upande wa Simba, matokeo ya mzunguko wa kwanza ilikuwa 2-2 wakati mbao ikiwa nyumbani. Leo Simba atakuwa nyumbani uwanja wa Taifa, Dar.
Swali linalobakiwa ni hili; Je, Mnyama atafanikiwa kuzichanachana Mbao?
View attachment 7016510' Mechi inaanza
Kikosi cha Simba
View attachment 701643
Kikosi cha Mbao
View attachment 701714
1' Simba wanaanza kwa kupigiana
2' Mbao nao wanapanga mashambulizi kwenye lango la Simba
04' Habibu kyombo anafanya shambulizi kuelekea lango la simba ila anadhibitiwa na James Kotei.
06' Mbao wanafanya shambulizi lingine linadhibitiwa.
07'Mbao wanaonekana kujipanga vizuri japo Simba wanajitahidi kujipenyeza kupitia pembeni.
08' Simba wanafanya shambulizi kwenye lango la mbao na wanapata faul, faul imepigwa ila haijazaa matunda.
10'Simba wanapiga kros kupitia kwa Gyan, na Okwi anaikosakosa.
11'Kipa wa mbao anaonyeshwa kadi ya njano
12'Mbao wanafanya counter attack ila wanadhibitiwa.
14'Ndemla anapiga shuti golini ila kipa anaidaka
15'Mbao wanapigia vizui wenyewe kwa wenyewe
16'Mpira unapigwa kuelekea simba
17'Faul kuelekea simba ni karibu na 18, simba wanadhibiti
20' Free kick kuelekea lango la mbao, ni nje kidogo ya 18. Golikipa anadaka
21'Okwi anafanya shambulizi lakini anadhibitiwa
24' Mbao wanafanya shambulizi hatari golini mwa simba ila mabeki wa simba wanasimama vizuri kudhibiti madhara
Kona imepigwa kwenye lango la simba inapigwa kichwa na kutoka nje.
26' Simba wanapanga tena mashambulizi kwenda lango la Mbao.
28' Mbao wanafika langoni mwa Mbao mara nyingi zaidi, wanaonekana kuwa na kasi sana.
29' Mpira sasa ni kushambuliana kwa zamu
31' Anatoka Ndemla anaingia Mzamiri Yasin
37' Goooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Simba inapata goli la kuongoza kupitia kwa Siza Ramadhani Kichuya, ni baada ya kupokea pasi kutoka kwa Emmanuel Okwi na kuutundika wavuni.
41'Emmanuel Okwi anavutwa na beki wa Mbao David Mwasa na imeamriwa kupigwa penati na David mwasa anaonyeshwa kadi ya njano
Penati inapigwa
41'Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
45'Mbao wanafanya shambulizi kwenye lango la Simba kupitia kwa Habibu Kyombo anatoa pasi lakini inatoka nje
Mpira ni Mapumziko
Kipindi cha pili kinaanza
45'Mbao wanajitahidi kulishambulia lango la Simba ila inakuwa inashindwa kuzaa matunda.
46' Okwi anawekwa chini, faul inapigwa
48' Shomari Kapombe yuko chini na anagangwagangwa na dk wa Simba
50' Simba wanapigiana vizuri huku wakipanga mashambulizi kuelekea Mbao
51' Mzamiru anapata nafasi nzuri ila anapiga shuti hafifu na kipa anaidaka
James Msuva, mdogo wake Simoni Hapigodi Msuva anatoka
52' Faul inapigwa na almanusra afunge japo kipa anaiokoa
54' Faul inapigwa kuelekea Simba, kipa wa Simba Manula anaidaka
55' Emmanuel Mvulukule anaoneshwa kadi ya njano
57' Anatoka Ibrahimu Njohole anaingiaSaid Said kwa upande wa mbao
59' Nicolaus Gyan anafanya shambuuliz matata ndani ya lango la Mbao, lakini anadhibitiwa na Yusuph Ndikumana.
62'Mbao wanafanya shambulizi kupitia kwa Habibu Kyombo lakini anaitoa nje.
63' Free kick kuelekea lango la Simba, inakuwa ni kona
65'Otecha anapiga shuti kali lakini halijalenga vizuri goli
66' Habib Kyombo anaachia shuti moja golini lakini inatoka nje
67'Simba wanaanzisha mashambulizi upya, wanapata kona inapigwa na Kichuya ila haijakuwa na madhara.
69' Gooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo
Emmanuel Okwi anawanyanyua mashabiki wa Simba kwa kutundika goli la tatu baada ya kupokea pasi kutoka kwa James Kotea na kutundika kimiyani.
Kama Moira ulikuwa unaelekea golini mpinzani akiugusa/pangua hauhesabiki Own Goal. Ni pale tu mpinzani anapofanya Moira unaoenda nje kuingia goliniAzam wamempa beki OG
Nani katungua?La 3 bado 2...Leo 5G
Nani kachana mbao?Soka safi mkuu tunapata goli la3
Tatizo hamuweki wafungajiMpaka huu mpira uishe hizi mbao zitabaki toothpick.