RAMAKISIMA
New Member
- Jun 29, 2023
- 2
- 4
ANDIKO LA MAONI
Maendeleo ni mchakato unaohusisha ushirikiano baina ya wananchi, haiwezekani wananchi wote wakafanya kazi zote kwa pamoja katika eneo moja .Ni lazima kuwe na mgawanyiko wa kazi ili kuleta tija katika utendaji na kuzia mwingiliano wa majukumu. Mgawanyiko wa majukumu huainisha kila jukumu la muhusika na vipi atawajibika na nani ataulizwa nini.Mgawanyiko huu wa majukumu huibua dhana ya utawala bora inayoainisha utekelezwaji wa majukumu kwa njia jumuishi na shirikishi kwa kuzingatia haki na wajibu wa kila muhusika katika jamii ili kuleta maendeleo endelevu.
Tanzania tunatumia elimu kutengeneza rasilimali watu na sehemu ya kuanzia ni shule za msingi na sekondari katika mfumo rasmi wa elimu, ni muhimu saana wanafunzi kuanzia ngazi ya chini kutambua taratibu za uendeshwaji wa elimu ili kuhakikisha dhana ya utawala bora inatambulika na kuchochea maendeleo endelevu.
Kwa sehemu kubwa wazazi ,walezi pamoja na wanafunzi hawaelewi taratibu za uendeshwaji wa shule hali inayochangia kukwama kwa maendeleo ya elimu.Walimu na wazazi na walezi wamekuwa maaduii wa chinichini hivyo kushindwa kushirikiana na kubaki kutupiana lawama hali inayochangia wanafunzi kuacha shule,mimba kwa wanafunzi wa kike kuongezeka,ukiuwaji wa haki za wanafunzi ,utoro kukithiri,rushwa ya fedha na ngono baina ya walimu na wanafunzi kuongezeka
Kwa kuwa kutokujua hujaza hofu ,wazazi na walezi wengi huwa na hofu na kushindwa kujua nani wa kumpelekea tatizo la mwananfunzi pindi inapotokea changamoto za shule.
✓Mfano wa baadhi ya matukio yanayotokea katika mashule ambayo huchangiwa na kutojua taratibu
I.Mzazi au mlezi anaweza kwenda shule kufuatilia mwenendo wa taaluma ya mwananfunzi na akaenda moja kwa moja katika ofisi ya mkuu wa shule au mwalimu mkuu badala ya kuanza na mwalimu wa darasa kisha ofisi za taaluma,hali inayochangia upotevu wa muda kwa mzazi au mlezi kusubiri amuone mkuu wa shule na Kisha swala lake litashushwa ngazi za chini ofisi alizoziruka.
II.Wanafunzi wamekuwa wakifukuzwa shule,kusimamishwa masomo bila kufuata utaratibu sahihi na wamepoteza haki ya kuendelea na elimu kwa hila za viongozi wa shule na walimu.Kutokana na ufinyu wa uelewa wa taratibu za uendeshwaji wa makosa ya kinidhamu kwa wanafunzi na adhabu zake hutokea mwananfunzi akasimamishwa masomo kwa kuambiwa aende nyumbani mpaka bodi ikae na wazazi huamini tayari kafukuzwa moja Kwa moja Kwani hawajui waanzie wapi na walimu hawawaweki wazi wazazi au walezi juu ya taratibu za kufuata.
III.katika shule za serikali wanafunzi husumbuka kupata uhamisho na kufikia hatua ya wazazi kutoa fedha kwa walimu ili wawasaidie wakati uhamisho ni jambo la bure na ni haki ya mwananfunzi.
Kwakuwa sehemu kubwa ya wananchi wanafuata huduma kwa kukariri na si kwa kuzijua taratibu halisi hali ambayo wateja wengi hukalili mwalimu mmoja wa kuwahudumia katika shule na inapotokea mwalimu wanaemfahamu hayupo hushindwa namna ya kupata huduma na hujiingiza katika rushwa ili kupata wepesi wa huduma wakihisi wanaokoa muda kumbe wanakuza rushwa .Njia zifuatazo zitachangia kukuza uelewa Kwa wazazi,walezi na walimu juu ya haki na wajibu katika shule.
SHUGHULI ZA KUFANYIKA
✓Kufanya semina zitakazoongozwa na wanasheria na afisa elimu.Semina itahusu kutoa ufafanuzi juu ya sheria za uendeshwaji wa elimu kwa kuainisha haki na wajibu wa mwalimu, mwanafunzi na mzazi au mlezi.Pia wanasheria watatoa ufafanuzi wa taratibu za kuzifuata kudai haki na kanuni zinazoongoza utoaji wa elimu katika shule.
✓Kufanya kampeni Kwa kutengeneza matangazo mafupi yatakayorushaa kwenye vituo vya redio na runinga.Pia kutumia vipindi vya redio na runinga kutoa ufafanuzi Kwa wananchi juu ya taratibu za uendeshwaji wa huduma za elimu katika shule.
✓Kuweka chati katika katika mbao za matangazo za shule kwa Lugha ya kiswahili inayoainisha mgawanyo wa majukumu na wahusika katika shule ili kuwarahisishia wateja kujua wahusika kulingana na mahitaji yao.
✓Kutengeneza majarida yanayoainisha majukumu ya kila idara katika shule,ukomo wa mamlaka ya shule,haki na wajibu wa mzazi , mwanafunzi na mwalimu na kuyagawa kwa wanafunzi na wazazi.
✓Kushirikiana na asasi za kiraia kutoa eimu ya utambuzi wa wajibu na haki za Kila mdau wa elimu.
✓Shule kuwa na katibu mahususi atakaehusika kusaidia wazazi na wanafunzi kuwapa maelekezo kulingana na huduma hitajika.
HITIMISHO
Wanafunzi wengi hutumia udhaifu wa uelewa wa wazazi au walezi kuhusu maswala ya taaluma kufanya udanganyifu juu ya gharama za mahitaji ya shule, pia baadhi ya walimu wamekuwa hawatoi taarifaa sahihi na rahisi za upatikanaji wa huduma ili waendelee kunufaika na uelewa mdogo wa wateja kwa kuminya haki za wanafunzi ,kufanya uonevu na kudai rushwa ya ngono baina ya walimu na wanafunzi,rushwa ya fedha baina ya walimu na wazazi au walezi.
Hali ya uelewa mdogo wa taratibu za uendeshwaji wa shule ikiendelea kuwa chini itapelekea kuzalisha kizazi kibovu kimaadili kisichofuata utaratibu katika utekelezwaji wa majukumu hivyo Kuongeza idadi ya wananchi wazembe wasiofuata utaratibu katika utekelezaji wamajukumu na wasiokuwa na nia ya kutambua mambo kwa kina. Ni lazima viongozi wa elimu kutambua utawala bora Kwani maendeleo sio jambo la kiongozi bali jamii nzima.Kufanya kazi na watu Wasiojua taratibu huchangia upotevu wa muda na kuzalisha migogoro isiyo ya lazima.

Upvote
3