Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
UWEKEZAJI BANDARI YA MTWARA WALETA MATOKEO CHANYA
Naibu waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ( Sekta ya Uchukuzi) Mhe. Atupele Mwakibete, amesema uwekezaji wa zaidi ya shillings bilioni 157.8 uliowekwa katika maboresho ya Bandari ya mtwara umeanza kuleta matokeo kwani kumekua na ongezeko la shehena na meli zinazohudumiwa katika Bandari hiyo.
Akizungumza Katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa kuhudumia Shehena ya Makasha itakayosafirishwa (transshipment) kwenda Moroni na Mutsamudu Katika Visiwa vya Comoro kwa kutumia bandari ya Mtwara, Mhe. Mwakibete amesema lengo la Serikali ni kupata mapato zaidi kupitia Bandari na kutumia feddha hizo kuboresha Miundombinu mingine.
“Ni wakati sasa kuhakikisha mnasimamia vizuri ongezeko hili la meli na mzigo ili kuvutia wateja wengi zaidi kutumia Bandari sababu Kama Serikali hatutegemei wasafirishaji wake na Malalamiko ya kupata huduma zisizo na viwango”amesema Naibu Waziri Mwakibete.
Naibu Waziri Mwakibete ametumia fursa kuwataka wasafirishaji zanaosafirisha mizigo kanda ya kusini kuitumia vizuri bandari hiyo kwani watapunguza gharama za kushushia mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam hali itakayorahisha kufikisha bidhaa kwa walaji mapema na gharama Nafuu.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amesema kuzinduliwa kwa mradi huu kutachangia kukuza uchumi wa Mkoa wa Mtwara na kusisitiza kuwa Mkoa huo utaendelea kujenga na kuweka mazingira mazuri kwa Bandari ya Mtwara kufanya kazi.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Mrisho Selemani Mrisho amesema, TPA inaendelea kumshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya Bandari ya Mtwara ambayo sasa imeongeza ufanisi na mapato yake kwa kiasi kikubwa.
Bw Mrisho ameishukuru Kampuni ya Meli ya CMA- CGM kwa ushirikiano mkubwa Katika kukuza Biashara kwenye Bandari ikiwemo Bandari ya Mtwara ni kusisitiza kuwa ni Jambo la Furaha kubwa kwa Bandari ya Mtwara kuhudumia Shehena ya aina hii.
Aidha, Meneja Mkuu wa Kampuni ya CMA-CMG Bw. Benjamin Coston amesema kampuni yao ina dhamira ya dhati kufanya kazi na Biashara hapa nchini kutokana na mazingira wezeshi ya kufanya biashara.