Twende kitaalamu kidogo kabla ya kutuhumiana. Maeneo ya Sam Nujoma, je ardhi imefikia kiasi gani kwa meta mraba?
Acha nibunie. Labda haitazidi 250,000/=. Ikiwa ndivyo, basi eneo la ekari (acre) 1 hapo S'joma litazidi kdg 1bn/=. Bilioni si ndogo jamani.
Kwa hizo 16bn/17bn/=, basi eneo litakua ekari 16 hivi. Zaidi ya meta za mraba 64,000!!
Wenye kujua, je eneo linafikia ekari 16? Maana yake ni kuwa kwa upana wa meta 63, urefu uwe kilometa 1. Kutoka hapo Kobil labda hadi karibia na Mwenge!!
Au eneo linalowiana na hilo.
Hiyo ni km meta mraba moja ya ardhi iuzwe kwa 250k/=. Na hiyo ni kadirio la juu kwa Sam Nujoma. Unless mwenye taarifa za mauzo ya ardhi maeneo hayo siku za karibuni aje kuthibitisha tofauti.