Uwekezaji: Sio Kila Uwekezaji na Kujenga Nchi, Mwingine ni Kuvuna tu, Uwekezaji wa Total Energies kujenga Nchi!

Angalizo zuri sana umelitoa ndg. Paskali kwa Serikali kwa kuzingatia Masilahi ya Tanzania na watanzania.

Ni kweli Serikali ya awamu hii ya 6 imeifungua Tanzania yaani kwa sasa Tanzania imefunguka kabisaaa.

milango na madirisha yote yamefunguka........ .hili ni jambo jema lkn tuchukue tahadhari maana wapo watakao jipenyeza kwa gia ya uwekezaji kumbe ni wanyonyaji.

Uwekezaji unao lengwa na kukusudiwa na Serikali ya Rais Samia ni ule ambao utawainua watanzania kiuchumi na sio kunyonya uchuminwa watanzania.

kwa sasa sioni tatizo kwenye uwekezaji wa uchimbaji wa madini kwasababu Hayati JPM alisha ziba myanya kwa kufanya marekebisho ya Sheria za madini hivyo kama nchi tunanufaika vilivyo.

ila bado ni muhimu sana tukaweka chujio madhubuti na imara ili kuweza kuchuja wawekezaji na wanyonyaji.
Tatizo kila muwekezaji anatafuta faida kubwa ikibidi hata kwa kufanya udanganyifu, hata hiyo kampuni ya Total sio ya kuiamini kwa 100% lazima kuwe na macho makali.
 
Katika uwekezaji cha kuangaliwa kwanza ni ajira. Maendeleo yanakuja pale mwekezaji anapolipa kodi na wafanyakazi wake wanapolipwa mishahara mizuri. Kwa mfano Toyota ikiamua kujenga kiwanda cha magari Marekani, kitu cha kwanza kinachotajwa ni ajira ngapi zitapatikana kwa Wamarekani. Swali la pili ni kodi kiasi gani watalipa. Hawaulizi Toyota itajenga shule ngapi au hospitali ngapi. Hawaulizi Toyota wataleta maendeleo gani maana wanajua watalipa kodi na kodi zitatumika kuleta kujenga shule, hospitali, barabara na maendeleo mengine. Wafanyakazi watalipwa vizuri watatumia mishahara yao kununua nyumba, gari, na vitu vingi kwa hiyo hela itazunguka kwenye uchumi.

Mwekezaji hana wajibu wa kuwaletea maendeleo. Yeye wajibu wake kutafuta faida kubwa (maximize profits) na kama ni kampuni inayouza hisa ni kuwapa faida shareholders wake na kulipa kodi za nchi zao. Vile vile kuwapa ajira watu wa nchi zao. Msitegemee wawekezaji watawajengea nchi, mtasubiri muda mrefu. Nchi mtajenga wenyewe mkitumia mbinu na maarifa na kuacha ufisadi, tamaa, na ubinafsi.
 
January hajakupigia simu?,basi atakua hajausoma,
Tumalize kimoja kwanza, JNHP au hapo total energy hatuweki hata senti moja ya serikali?
 
Nina mashaka na makala yako....
Siku zote umekua uki ipigia chapuo hii kampuni...

Naona hii mada sio kwa maslai ya taifa, bali maslai ya Pascal....
Anaweza kuwa underground Market Manager wa hii kampuni
 
Kaka Pascal Mayalla uwekezaji ni kitu muhimu sana hasa kama tunataka kupige hatua za haraka, kinachohitajika ni uwazi zaidi kwa serikali na wawekezaji. Lakini mbali na kuwajengea ujuzi watanzania tunahijati kutengeneza mazingira ambayo yatawalazimu hawa wawekezaji kuingia katika ushirikiano (Partnership/Joint Venture) na wazawa.

Mimi kabisa leo kwamba wadau kama vyuo vikuu wanaweza wakatengeneza mashirika yao ambayo yangeweza kufanya mkono kwa mkono na wawekezaji, mbali na kuwapa tu ajira. Kwamba mwekezaji awe anamiliki asilimia 70% huku mashirikia ya vyuo vikuu yawe yanamiliki asilimia 30%. Tutaanza kidogo kidogo, lakini haya mashirika yetu yatakuja kujaa wataalamu na kumiliki mali nyingi sana tu huko mbeleni.

Changamoto kubwa ambayo tunayo Tanzania, ni wale wazee wajamaa wa kipindi cha Nyerere ambao binafsi huwa siwaelewi kwanini wanachukia sana wawekezaji na ukiwaambia tufanye njia gani, wao huishia kusema TUJITEGEMEE lakini hawatupi njia sahihi ya Tanzania kufanya hivyo. Kiufupi wao ndiyo waliifikisha nchi hapa na siasa zao mbovu, na bado wao wanadhani kwamba walihujumiwa na mabeberu, nothing is ever their fault....
 
Sasa bwana Samurai unashauri sisi tuwakatae hawa wawekezaji kwasababu ya Chad na Congo ???
 

paragraph ya mwisho: hawa wazee baada ya kuanguka kwa ujamaa walibaki hawana plan B pamoja na mzee mwenzao JKN....wakabaki na siasa zilezile bila kujifunza na kuelewa uelekeo mpya wa dunia, matokeo yake wamebaki na ideology ileile ya kizamani kichwani kama mji uliotekelezwa na kubakia magofu matupu...

Wazee hawa wangenifunza uelekeo mpya wa dunia na kuwekeza kwa kuwapa maarifa vijana na kuandaa succession plan kwa kizazi kipya bila shaka tusingefika huku...lack of plan and jelous wanaona wao ndio pekee wenye akili yakuliokoa hili Taifa ilihali wao ndio waliolizamisha...kifupi wanataka tutumie akili ile ile iliyofeli tujinasue kwenye tope which is very impossible..

Vijana wa sasa wanahitaji kasi ya maendeleo na sio waoga kurisk na kwenda mbele, Vijana hawa wengi huumia sana nchi yao inapoitwa masikini ilihali sio masikini na inaweza kutoka hapa..Mifumo na hawa wazee wasipokuwa makini watalipa deni kubwa ambalo madhara yake ni damu za watu...

Hatujachelewa, zianzishwe forum kila mahala kuanzia vyuoni, mitaani, mitandaoni, hawa wazee na watu wa system watoke huko walikojifungia wakae na hiki kizazi kuona namna bora ya kufanya reform kwenye mifumo na damu mpya yenye kasi, akili na mawazo mapya iweze kuingia kilingeni na kusongesha Taifa mbele, tuachane sasa na hii mifumo ya watoto wastaafu, michepuko, kamlete, UVCCM, watoto wa vigogo, turudishe Taifa kwa watanzania wote ili kila mwenye akili na uwezo atumikie Taifa hili...
 
Hebu nieleweshe sisi hatuna gesi ya kusindikwa kwenye mitungi na kuuzwa badala yake ile gesi yetu ya ntwara ni ya kutoa umeme tu?
Ni kweli kuwa Taifa ges sio ya serikali bali ni Manji na ges ile inatoka nje ya nchi?
Ni kweli kuwa vinatoka halafu ndio hurudi kama ilivyokuwa milingoti ya umeme ya tanesco?
Ni kweli viongozi waliofanya madudu wao na familia zao hawajisikiki vibaya kwa vile hawaandikwi na kusimangwa mabarabarani na magetini na serikali haina mpango wa kuwafirisi walioingia cha kike kwenye mikataba mikubwa kiasi cha Tanzania kupoteza kuwanda cha karatasi Mufindi.
Kufa kwa shirika la bima ambalo magari yoote nchini walikuwa wanatuhudumia.
Kuuwa reli na shirika lake.
Je nnyie wa media mkizileta fulani ni tajiri wa mpaka kufa lakini alifisadi mradi fulani .watu tuwazoomee na kuwananga.
Nafikiri ni njia ya wananchi kupambana na ufisadi.
 
Kama sio umeshakunywa John Walker muda huu ulipoandika hii mada, basi ni dhahiri umeshapoteza uwezo wako wa uandishi. Nimeangalia hiyo mada yako na kujaribu kuona mahusiano ya huo uwekezaji wa bomba la mafuta la Uganda, na ulichoongelea kuhusu uwekezaji wa Total hapa Tanzania kwenye vituo vya mafuta nimekosa uhusiano. Kama ndio umefikia huku kwenye uandishi, nakushauri jikite kwenye siasa za CCM moja kwa moja, maana ujinga wa hivi ndio huwabeba kwa watu wasio na uelewa wowote.
 
Nina mashaka na makala yako.

Siku zote umekua uki ipigia chapuo hii kampuni.

Naona hii mada sio kwa maslai ya taifa, bali maslai ya Pascal.
Kuwa na mashaka si lazima kuambatane na UHALISIA....

Kwanini tuwe na "negativity" katika mada tajwa?!!

Kwanini tutangulize "ARGUMENTUM AD HOMINEM" katika udadavuaji ?!!!
 
Acha ulevi wa kijinga Pasco, kama una matatizo ya kifamilia tafuta namna nzuri ya kuyamaliza. Mada yako umeweka vitu viwili tofauti na kufanya ni kitu kimoja! Kwanza sio kweli kama huo uwekezaji wa Total Tanzania ndio mkubwa kabisa, isitoshe mradi wa Bomba la Mafuta la Uganda sio mradi wa joint venture baina ya Tanzania na Uganda, bali Tanzania tumetoa njia ya kijiografia kupitisha hilo bomba, tukitarajia kupata kodi kwenye mauzo ya hayo mafuta. Na hili litawezekana kama iwapo huo mradi wa Bomba la mafuta utakamilika Kweli, kwani kuna utapeli mwingi kwenye hilo jambo. Inshort kama unaongelea uwekezaji wa Total Tanzania, tenganisha na huo wa bomba la mafuta la Uganda.
 
Naona unamuomba nyoka miguu, yeye mwenyewe kapoteza.
 
Umetoa mifano mingi ya kupanua bongo zetu....

Ila ni makampuni gani nguli na ya kibepari duniani yasiyo na KASHFA tofauti?!!!

Afrika tungekuwa na uwezo wa vitendea kazi na miundombinu ikiambatana na UWIANO SAWA WA KIBIASHARA tungeyachimba wenyewe madini na mafuta yetu......


Kuutafuta huo usawa 💯 p ndiko kuliko wagharimu WATAWALA WENGI WA KWANZA barani humu....

Hoja yangu si kushajiisha KUPIGA MAGOTI kwao bali tulipo ni kuhakikisha angalau TUNAFAIDIKA kwa raslimali zetu zilizopo kwa mintaarafu ya "WIN-WIN SITUATION"!!!

#SIEMPRE JMT
#NCHI KWANZA KABLA YA NAFSI ZETU🙏
 
Uwekezaji ni jambo jema lakini tuwe makini na aina ya wawekezaji na terms zao....vyombo vyetu viwe makini 24/7 kuwajua hawa watu na matokeo yawe positive kwa watanzania...

Ni wakati wa kuwekeza kwenye rasilimari watu ili hawa wawekezaji wakija tayari wakutane na trained workforce iliyotayari kwa kazi...Vyombo vyetu visimamie maslahi ya watu wetu 24/7 kuhakikisha watu wetu wanalipwa vizuri, wanapata international training and exposure, healty and safety zinazingatiwa, standard za kazi zinazingatiwa..

Hawa wawekezaji walazimishwe kutoa scholarships kwa watu wetu kusoma vyuo mbalimbali duniani, Majasusi wapandikizwe kulearn new technologies na kuandika reports zitakazokaa huko dip state na tiss..

Supplies na watoa huduma mbalimbali wawe wazawa kwa 90% na Serikali iwezeshe wawekezaji wa ndani kupata mikopo nafuu kutoka kwenye mabank ili wawe na uwezo wa kuwekeza ( hapa sizungumzii watanzania wahindi na waarabu).. Serikali kupitia vitengo vyake ifanye controlling kwa makampuni ya wazawa kuzingatia standards..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…