Uwekezaji tunaupenda sana, ila kwanini wawekezaji wanakuja kuwekeza kwenye miradi iliyoiva?

Uwekezaji tunaupenda sana, ila kwanini wawekezaji wanakuja kuwekeza kwenye miradi iliyoiva?

Bwawa la Nyerere limetumia matrilioni ya fedha ambazo kama zingeingizwa kwenye afya kila mtaa sasa Ungekuwa na kituo cha afya na watumishi wa kutosha. Kwanini mwekezaji hakuja kabla ya miundombinu ya bwawa la Nyerere kuanza au kukamilika?

Bandari ya Dar es salaam imemeza mabilioni ya pesa za mkopo na fedha za ruzuku ili ipanuliwe. Upanuzi unaenda kukamilika tu mwekezaji huyo.
Nasikia hasira.

TEMESA kwa miaka 5 iliyopita imemeza mabilioni ya pesa kutengeneza vivuko leo hii vivuko vinatafuta mwekezaji. Hili mbona kituko.

Kuna taasisi nyingi ambazo zinapumulia mipira wawekezaji wakawekeze pesa huko ili kuleta maana halisi ya NENO mwekezaji.

Hii tren iliyokula matrilioni ambayo yangepelekwa yote wizara ya elimu wanafunzi wa msingi na sekondari wangeweza kupata chakula bora cha mchana na walimu wangelipwa overtime allowance kama watumishi wengine.

Soma Pia: Wito: Pamoja na kusainiwa kwa mikataba mitatu ya wawekezaji wa Dubai Serikali ibainishe maudhui yake na mabadiliko yaliyofanywa kwenye mkataba wa IGA

Imagine shule ya serikali ambayo ina miundombinu yote kijana anamaliza form 4 hajui kuwa Songea si mkoa bali ni wilaya tu. Mtafute kijana wa kidato cha tatu shule ya serikali akuelezee ugonjwa wa malaria kinafaubaga aisee utaishia kusikitika.
Unafikiri pesa unazokopa kujengea bwawa kama si wawekezaji wanaokukopesha ni kina nani?

Tana hilo la kukopeshwa ndiyo janga kuliko la PPP.
 
Back
Top Bottom