Uwekezaji wa DP-World ni USD 250 milioni ni mdogo kuliko "kishika uchumba" cha Barrick USD 300 milioni

Uwekezaji wa DP-World ni USD 250 milioni ni mdogo kuliko "kishika uchumba" cha Barrick USD 300 milioni

..Watanzania sijui akili zetu zikoje.

..Kwanini hatujui thamani halisi ya rasilimali zetu?

..Dpw wameahidi kuwekeza usd 250 mil na kuchukua bandari yetu.

..Na fedha hizo sio kama wanawekeza kwa mkupuo, bali ni kwa miaka kadhaa.

..Tanzania kama nchi hatushindwi kupata kiasi hicho cha fedha.

..Hata kishika uchumba cha Barrick tulichokuwa tunakidharau ni usd 300 mil.

..Pia sisi wenyewe tulishafanya uwekezaji mkubwa wa kuboresha bandari ambao ni zaidi ya fedha alizoahidi Dpw.

..kwa habari zaidi fuatilia link hapo chini.

CCM hawafai kabisa.
 
Hawa ccm wabinafsi wanaolindana usitegemee wanaweza fanya chochote, bora tuuze nchi yote kila mtu apewe chake tutahamia kenya au burundi
 
Soma vizuri link,hawaekezi bandari yote,bandari ya Dar,ina berth 12,wanawekeza 4 berths,tofautisha na kuwekeza na kuchukuwa.Kwa mfano aliyekodisha frem ya duka,amewekeza kwa mwenye nyumba,sio amechukua frem ni mali yake.Watanzania sio kila kitu tunapinga bila kutumia akili.
Hii ni mihemko Jazz Band !!
Watu wengi hudhani kila kinachoandikwa mitandaoni ni cha kweli !!
Habari nyingi kwenye mitandao hata hiyo mitandao ya habari ya nje ni uongo tu ndio unatawala !!
Habari ni Silaha ! Kwahiyo kila mtoa habari huwa anaangalia maslahi yake katika hiyo habari anayotaka kuitoa !!

Vita vya Uchumi ! Kila muamba ngozi huvutia upande wake !! 🙏🙏
 
Inasikitisha sana kuna watu walikua beneficiary wa scholarship za serikali 1960's-1990's ambao wengi wao ndio walitumiwa kufanya negotiation.

Serikali laiti ingejua hawa watu isingewasomesha miaka hiyo maana nadhani kwa vitu tunavyoviona kwenye mikataba ya kimataifa ni fedheha hawa watu wangeachwa tu vijijini miaka hiyo ya giza maana elimu waliyopewa bure kabisa ughaibuni na exposure waliyoipata haijawasaidia kabisa bora wangeachwa tu vijijini kwao.
 
..Watanzania sijui akili zetu zikoje.

..Kwanini hatujui thamani halisi ya rasilimali zetu?

..Dpw wameahidi kuwekeza usd 250 mil na kuchukua bandari yetu.

..Na fedha hizo sio kama wanawekeza kwa mkupuo, bali ni kwa miaka kadhaa.

..Tanzania kama nchi hatushindwi kupata kiasi hicho cha fedha.

..Hata kishika uchumba cha Barrick tulichokuwa tunakidharau ni usd 300 mil.

..Pia sisi wenyewe tulishafanya uwekezaji mkubwa wa kuboresha bandari ambao ni zaidi ya fedha alizoahidi Dpw.

..kwa habari zaidi fuatilia link hapo chini.

Hoja ile ya kusema kuwa tunawapa DPW bandari zetu kwa sababu wanakuja na mtaji wa dola milioni 250 na wataboresha huduma za bandari, ilikuwa ni hoja ya wezi kuwadanganya punguani.

Miaka michache kabla, nchi imekopa na kuwekeza dola bilioni 1 kwenye bandari, halafu eti unamleta mwekezaji wa dola 0.25 bilioni, yaani robo ya pesa uliyowekeza mwishoni. Na huku, kabla yake ulishawekeza mabilioni ya dola mpaka kufikia hapo.

Mtu mwenye akili hawezi kupoteza muda kusikiliza huo upuuzi. Hapa kilichofanyika ni wizi tu, ndiyo maana huoni chochote kilichoboreka wala kubadilika tangu hao DPW wagawiwe bandari mama ya Dar.
 
..vurugu zote walizosababisha Dpw kumbe wanawekeza usd 250 mil tu.
Tena hiyo imetajwa kwa kujikakamua tu ili kuwadanganya wajinga. Kiuhalisia, hawekezi chochote, maana DPW hii ya hapa kwetu, ni ya wajanja wa pwani.
 
Usiwe na wasiwasi, hicho ni kianzio tuu!, umuhimu wa DPW na Bandari zetu sio just capital injection, ni technical know how za how to operate more efficiently and more profitably ambapo sisi wenyewe hatuwezi hata kama hizo fedha tunazo.
P
Kwahiyo huo upuuzi ndo iwe USD 250mil? Dah
 
Shida kubwa la taifa letu ni rushwa,ambayo imefanya watawala kuwa vipofu wasio ona mbele bali kutanguliza maslahi binafsi mbele kwa kupiga 10%.

Na sio ajabu siku akistaafu atakuja na unafiki wa kuandika kitabu,kusikitika kwa kuuza bandari kwa wajomba zake kama mzee Mwinyi.
 
Usiwe na wasiwasi, hicho ni kianzio tuu!, umuhimu wa DPW na Bandari zetu sio just capital injection, ni technical know how za how to operate more efficiently and more profitably ambapo sisi wenyewe hatuwezi hata kama hizo fedha tunazo.
P

Hiyo technical know how hawa DPW ya Bongo, wataipata wapi?

Trust me, DPW inayofahamika, haitaendesha bandari ya Dar. Endelea kufuatilia kama utaona chochote katika ubora wa huduma kitakachokaribia huduma zile za bandari ya Dubai, ambapo watu walienda kutembezwa.
 
Sisi hatuwezi kitu cho chote. Kama unabisha nitajie kitu kimoja tu ambacho unaweza kusema kweli hapa tumeweza. Na tatizo letu kuu ni ufisadi. So sad!
In short tumeaajiri DPW kunamage baadhi ya magati yetu…. Not the whole port

Na kazi yao ni beyond clearance ya mizigo, but inbound logistics and outbound

We need tpa watupe details za business model
 
Hakuna jambo serikali ya mboga mboga imewahi kufanya kwa usahihi wake hata siku moja na haitawahi kutokea, ukipata kanafasi kwenye serikali kwapua kwa kadri utakavyo weza kwa sababu wezi wakubwa hua hawafungwi hata siku moja
 
Usiwe na wasiwasi, hicho ni kianzio tuu!, umuhimu wa DPW na Bandari zetu sio just capital injection, ni technical know how za how to operate more efficiently and more profitably ambapo sisi wenyewe hatuwezi hata kama hizo fedha tunazo.
P
Wakati Mkapa ameleta watu wa kuchimba dhahabu tukapewa hadithi kama hizi.... miaka 15-20 baadae, hao hao wakatuambia tulikuwa tunachezewa.

In 2040's huko, you are going to eat your words.
 
Back
Top Bottom