Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Uwekezaji wa vyumba vya kupanga, mrejesho wa uwekezaji

Watu watakuja kushtuka too late😂😂
Mji unaendelea kwa spidi kubwa sana ule. Yaani kama hayo maeneo niliyopiga hizi mijengo, mahitaji ni makubwa sana ya makazi.
Wanaouza maeneo makubwa makubwa sasa hivi ni wale ambao walikamata maeneo kipindi hicho, sasa hivi wameyagawanya, wanayapiga bei tu kwa raha zao (wengi ni wazee wazee- wastaafu).
Mkuu usiniambie hivyo natamani nizitapike zile bia na nyama nilizokuwa nafakamia badala ya kuweza😬😬😬😬😀
 
Miembeni huko ngoja nitafute weekend moja nije kupaona.

📌📌Mkuu usisite kutuwekea fursa za wauzaji wa viwanja kama watakuwepo hiyo bei ni ya kizalendo kabisa😄😄😄 hapo unaunga viwili au vitatu unamaliza kazi🤝💪
Karibuni sanaaa...!! Kama ukiwa tayari, unaweza kunicheki tu PM, mimi naweza kukupa namba ya simu ya mzee ambae ana maeneo makubwa hapo Kibaha-Kongowe anauza, na hana tamaa yule mzee. Hiyo ni pande direct, hakuna udalali.
 
Kabisa, yale maeneo kujenga huwa ni gharama hatari😂😂😂... Hata hivyo waliojenga kule wapewe maua yao, maana kwanza ule msingi pale chini tu unaweza ukasimamisha nyumba yako huko vikindu🤣🤣
Wekeza hela kwenye kiwanja kizuri kwanza, architect akuchorea plan nzuri,hela zikibaki ndio uanze ujenzi. Nyumba ni investment ya ghali naya muda mrefu,epuka kukurupuka.
 
Wekeza hela kwenye kiwanja kizuri kwanza, architect akuchorea plan nzuri,hela zikibaki ndio uanze ujenzi. Nyumba ni investment ya ghali naya muda mrefu,epuka kukurupuka.
Yale ni maeneo ya kujenga nyumba za kukaa labda(kwa maana ni rahisi kwenda nayo taratibu kama usemavyo) ila kwa nyumba za biashara utatumia gharama kubwa sana thou Kodi ya maeneo yale nayo sio mbaya sana
 
Duuuuhh!! Hapo si inabidi investiment iwe kubwa sana? Na pia iwe yale maeneo ya kishua sana ya kitalii. Na in terms of accessories inabidi ziwepo za kutosha (eg swimming pool, etc). Mtu atalipia laki 5 per night bila swimming pool kwa mfano?
ukiwa na 300M unawezza kutoa kitu kidogo matata sana. ila inatakiwa vitu vingi ubane matumizi.
kusimamisha kitu kama hicho hapo chini milioni 3 na point hadi bati unaweka ishu iko kwenye finishing. ila kuna namna nawaza jinsi ya kufanya.
1740164992612.png
 
Yaani nikipitaga Goba najisemeaa hiii mimi bora nikakae huko kibaha au Mapinga aridhi imenyooka.

Ni mara kumi nikae huko pembezoni alafu ninunue kivits 1KR engine cc990.Nikifanye kibodaboda changu cha kujia mjini kati.

Maeneo hayo ya muinuko yana ujenzi wake sio hivyo vichuguu watz walivyootesha, chakukera kabisa ni ukosefu wa mitaa na mpangilio😬😬😬😬
Unaongelea Goba gani chief?
 
Mimi naamini kwenye kuwa na multiple sources of income mkuu.Hata huko UTT ninayo account ambayo natupia huko vijisenti,hiyo haimaanishi nisifanye harakati zingine. Haiwezekani hela yote niiweke tu UTT.
Plus, kinachotakiwa kwenye hii biashara kwanza ni usimamizi wa karibu na kuweka mikataba mikali, ambayo ndicho nilichofanya. Wakati nakabidhi funguo mpangaji, tunakabidhiana kwa picha kabisa hali ya ndani ya vyumba ilivyo (milango, rangi, holder za mapazia, etc), na hizo picha zimehifadhiwa pamoja na mkataba, anapoondoka tunalinganisha, kama kuna uharibifu anarekebisha kabisa.
Mkuu, nakuelewa sana ila ogopa kizazi cha wabongo. Wakati wa kuondoka huo ukali wa mikataba hautakuwa na maana yoyote. Nasema kwa uzoefu.
 
Mimi naamini kwenye kuwa na multiple sources of income mkuu.Hata huko UTT ninayo account ambayo natupia huko vijisenti,hiyo haimaanishi nisifanye harakati zingine. Haiwezekani hela yote niiweke tu UTT.
Plus, kinachotakiwa kwenye hii biashara kwanza ni usimamizi wa karibu na kuweka mikataba mikali, ambayo ndicho nilichofanya. Wakati nakabidhi funguo mpangaji, tunakabidhiana kwa picha kabisa hali ya ndani ya vyumba ilivyo (milango, rangi, holder za mapazia, etc), na hizo picha zimehifadhiwa pamoja na mkataba, anapoondoka tunalinganisha, kama kuna uharibifu anarekebisha kabisa.
Achana nao hao. Yaani hio UTT wanavyoipaisha utafikiri sijui nibuwekezaji gani wa maana wakati inatofauti ndogo sana na FDR account. Uwekezaji wako una ROI 19% haya UTT inatoa 19% kwa mwaka?
Halafu naona wameshikilia ukarabati, hivi nani lawadanganya kila mtu akitoka lazima ufanye ukarabati wa gharama? Sana sana rangi tu ambayo ukipiga mtu anaona nyumba mpya. Sasa rangi bei gani? Halafu nyumba zako zikiwa nzuri location nzuri watu wanakaa muda mrefu na wenhi wa aina hii wanakarabati wenyewe vitu vidogo. Naongea kwa experience sio hisia.
 
Hongera mkuu mimi mwenyewe natamani sana japo sina uwezo huo ndoto zangu nipate vyumba hata viwili kwavigwaza tutakuwa na uhaba wavyumba watakaotokea kwenye viwanda
 
Sisi kama binadamu kuheshimiana ni muhimu sana mkuu, bila kujali status zetu au tuna nyumba, ah hatuna, au tuna hela au hatuna.Tuheshimiane kwa ubinadamu wetu!
Aaaah naamini watu wapo wenye roho safi na wenye mioyo ya jiwe zilizokunjamana roho zao
 
Mimi nahitaji fundi wako huyo. Na hizi gharama zako. Kama itakupendeza.
 
Ukiweka pesa utt usisahau na inflation rate ya mwaka ni bora awekeze kwa real estate ambapo thaman yake inaongezeka kila mwaka. Utt unaweka pesa kwa muda ukisubir cha kufanya.
Sidhani Tz kuna mtu mwenye kipato kinachoendana na inflation. Kama wapo ni wachache sana.
 
Wakuu mko vizuri?

Kuna kipindi nilileta thread humu ya kujaribu kupata ideas ya namna ya kuiwekeza shs milioni 64 niliyokua nimei save, kwenye link hii hapa.

Nimekuja hapa kuleta mrejesho wa namna nilivyotumia ile pesa.

Ule mzigo wote niliuchimbia kwenye ujenzi wa vyumba vya kupanga wakuu. Vyumba hivi nimejenga maeneo ya Kibaha hapo (karibu na Miembe 7), na nimejenga kwa style ya chumba chenye choo ndani (self-contained) + sebule yake. Nimejenga jumla ya units 8 (zikiwa zimeunganika).

Maeneo hayo niliyojenga uhitaji wa makazi ni mkubwa sana.

Nimezijenga katika style ya unit nne nne (majengo mawili, kila moja unit nne). Jumla ya gharama nimetumia sio chini ya shilingi milioni 76 kukamilisha kila kitu hapo (hii ni kabla ya kuweka fence).

Tangia wakati nanyanyua boma, watu wengi sana walikua wanaulizia kila mara. Sasa hivi nimemaliza, nimeweka na fence pia (ujenzi wa fence unaendelea-bado mageti).

Tayari nimeanza kula kodi wakuu, hadi sasa unit zote 8 zimeshaingia wapangaji, nimeanza kula kodi kuanzia mwezi huu wa pili.

Napangisha kwa gharama ya 150,000 kwa mwezi kwa kila unit.

Nawashukuru wote ambao mlinipa ideas na mawazo mbalimbali wakuu. Mbarikiwe sana!

Nimeweka picha chache hapa chini kwa uelewa zaidi.

View attachment 3241776View attachment 3241777
Hongera sana mkuu hapo umefanya kitu chenye akili sana.
Ni biashara isiyo na stress na hainaga hasara popote ulipo unatumiwa muhamala wako kila mwezi kuliko ukurupuke kununua fuso kila siku safari za gereji ni presha tupu.
Yaani hadi nimetamani na mimi nyumba yangu ningeijenga kwa muundo kama huu
 
Back
Top Bottom