Uwepo wa nembo ya Royce Roycee kwenye Engine za Airbus ya Air Tanzania

Uwepo wa nembo ya Royce Roycee kwenye Engine za Airbus ya Air Tanzania

moyafricatz

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2015
Posts
2,904
Reaction score
4,902
Wakuu,

Katika pita pita yangu nilibahatika kuisoma vizuri engine ya kushoto ya ndege yetu Murua kabisa ya "Airbus 220" iliyokua imepaki pale JNIA.

Kitu kilicho-catch attention yangu ni nembo ya Rolls Royce's ambayo imechorwa.

IMG_20200830_205641_872.jpg

Wajuvi naomba mtusaidie kuna kahusiano chochote kati ya Rolls Royce's na Airbus.

Kila la heri wakuu.

Kidumu Chama cha Mapinduzi.

Magufuli tenaaa...
 
Kuhusu uwepo wa engine za Rolce Royce ni kwamba hawa jamaa biashara yao kubwa ni kutengeneza Engine za ndege.

Kuna wakati walijiingiza kwenye biashara ya kutengeneza magari ya kifahari lakini baadae waliuza hii division ya magari kwa kampuni ya BMW.

Kuwepo kwa Engine ya Rolce Royce kwenye ndege sio uamuzi wa mnunuaji bali ni maamuzi ya mtengenezaji.

Ndege mpya inapokuwa inasanifiwa, makampuni mbalimbali ya kutengeneza Engine (Mfano General Electric, Rolce Royce) hutengeneza Engine ambayo mtengenezaji wa ndege atahitaji kutokana na specification alizotaka mtengenezaji.

Kampuni itakayotengeneza Engine bora na yenye kukidhi vigezo ndio itakayoshinda tenda ya kutengeneza Engine kwenye hio model mpya ya ndege.

Mfano wakat airbus wanatangaza ndege mpya Airbus A350-1000 General Eelectric (GE) na Rolce Royce wote walileta proposed Engine zao mwisho wa siku Rolce Royce wakashinda na Engine yao ya TRENT XWB, Kwenye tender ya Model mpya ya Boeing 747 yani Boeing 747-8 General Electric walifanikiwa kushinda na Engine yao ya GE90.

Hivyo suala la engine ni mapendekezo ya mtengenezaji kwa sababu yeye ndie anaejua ndege yake imetengenezwa kwa malengo ya kukidhi mahitaji yapi na kwa viwango gani.
 
Hata ndege ya Trump ina Engine ya Rolls royce,engine za rolls Royce zinasifika kuwa na kelele ndogo na ufanisi mzuri so ni kawaida Airbus kuwa na Engine ya Rolls Royce

Pia ni vizuri kuwa na hiyo Engine kwa sababu nilisikia Trump anasema baadhi ya Airport ni noise restricted so huwezi kuruhusiwa kutua na ndege yenye kerere
 
hata ndege ya Trump ina Engine ya Rolls royce,engine za rolls Royce zinasifika kuwa na kelele ndogo na ufanisi mzuri so ni kawaida Airbus kuwa na Engine ya Rolls Royce
pia ni vizuri kuwa na hiyo Engine kwa sababu nilisikia Trump anasema baadhi ya Airport ni noise restricted so huwezi kuruhusiwa kutua na ndege yenye kerere
Umedadavua vizuri sana ukiwa na mifano hai...

Kongole sana mkuu.
 
niliwahi kusikia ROLLS ROYCE wanahusika pia na utengenezaji wa ENGINE za ndege

upo sahihi, Rolls Royce hutengeneza Engine za ndege,unaweza kununua ndege yenye Engine ya Airbus ukatoa ukaweka ya Rolls Royce kama Trump alivofanya kwenye ndege yake binafsi
so naona Serikali ya Tanzania iliweka specifications kwamba wanataka Ndege hiyo iwekwe Engine ya Rolls Royce au ni Airbus wenyewe waliamua kufanya hivo
 
Fact that unamtumia Trump kwenye mifano yako, utakuwa 'clown' kama yeye
 
Fact that unamtumia Trump kwenye mifano yako, utakuwa 'clown' kama yeye

Mkuu,huo ndio mfano pekee nilionao ,nilikua natizama documentary fulani kuhusu Ndege yake kwahiyo hapo ndipo nilipata majibu ya hiki mleta mada anachouliza hapa,nje ya hapo sina mfano mwingine
 
Na hii 'moyafricatz' n nini na ni avatar yko mleta mada.tupe shule juu ya hili
 
hata ndege ya Trump ina Engine ya Rolls royce,engine za rolls Royce zinasifika kuwa na kelele ndogo na ufanisi mzuri so ni kawaida Airbus kuwa na Engine ya Rolls Royce
pia ni vizuri kuwa na hiyo Engine kwa sababu nilisikia Trump anasema baadhi ya Airport ni noise restricted so huwezi kuruhusiwa kutua na ndege yenye kerere
Chadema bwana, mkuu umepoteza nguvu zako kuwaelezea, walikuwa wanadhani nayo ni kiki!
 
Engine za rolleys royce zimetumika kwenye ndege nyingi tu, kama..
Airbus A330, A340, A350, and A380, Boeing 777, boeing 787 Dreamliner. N.k.
Pia hutengeneza engine kwa ajili ya helicopters, turboprop, (pangaboi) jenerators na magari.
 
Engine za rolleys royce zimetumika kwenye ndege nyingi tu, kama..
Airbus A330, A340, A350, and A380, Boeing 777, boeing 787 Dreamliner. N.k.

Zinasifika sana kwa ubora,huenda ikawa ndio sababu
 
Back
Top Bottom