Uwepo wa UAE kwenye Mbuga, Bandari, Misitu, Tanesco: Nini kingine hatukijui?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Tatizo sio Kuwakaribisha wawekezaji bali ni aina ya mikataba, mfano hii mikataba ya waarabu kama wa bandari hauvunjiki hadi wao watake uvunjike ndio maana unaitwa wa milele.

1. BANDARI - Na sasa kuna mkataba huu wa bandari ambao ndio unazungumziwa zaidi sababu kipengere cha kuuvunja ni mpaka waarabu nao wakubali kuuvinja, ni kama mkataba wa milele tu.



2. MBUGA YA NGORONGORO - Ilianza na Mbuga mwaka Jana, waandishi wa habari kama Maulid Kitenge hawahawa wanaoshadadia bandari apewe mmwarabu ndio hawa hawa walikuwa mstari wa mbele kutangaza wamaasai wahame ngorongoro.



3. MISITU YA TAIFA - Mwezi February, Serikali ya Tanzania ilisaini hati ya makubaliano na Serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ajili ya kutusaidia kuendeleza misitu yote nchini inayosimamiwa na Wakala wa misitu (TFS). Yani wanaoishi Jangwani wanatusaidia kuendeleza misitu


4. TANESCO - kampuni ya falme za kiarabu ya UAE inayoitwa MASDAR ilisaini mkataba wa ushirikiano na kuzalisha umeme na TANESCO.



Ni kitu gani kingine hatukijui?
 
Urais si nafasi ya kuamka tu asubuhi na kumkabidhi mtu kama kifungua kinywa vile... let's enjoy the consequences!
Mkuu, nilitegemea ungesema Let's face them practically and manly. Wasomi huwa ni marufuku kabisa kukata tamaa. Afadhali kukata kamba ukipigania jambo unaloliamini kuliko kukata tamaa, ndivyo wasemavyo.
 
Atashindwa tu!

Sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, akishupaza, Mungu ataanza naye
 
Bado ccm, bunge na Ikulu...
 
Naomba mtusamehe!

Tulikosea pale tulipoamua Mwenyekiti wa chama awe ndio Rais kazi ya check and balance ilishindwa kufanyika ipasavyo!!

Nadhani wenye mamlaka watalifanyia kazi hilo!

Mungu IBARIKI Tanzania nchi yetu niipendayo SANA!!
 
Alisaini mikataba 32 kwahio ukae Kwa kutulia hahahahahahahaha
 
Nyerere aliwahi kusema kwamba "Uchumi mnao mnaukalia", hivyo wacha tuendeleza uchumi wetu ili nasi tufaidike.
Tatizo hasa si uwekezaji lakini naona tatizo ni aina ya muwekezaji.
 
Alisaini mikataba 32 kwahio ukae Kwa kutulia hahahahahahahaha
Mikataba ya ushirikiano hata na USA alisaini mikataba zaidi ya 15
Na China zaidi ya 11..
Main point ni "ushirikiano"...

Msijitoe ufaham kuongea uzushi
 
Hio namba 2 ndo naelewa Sasa aliposema wanyama hawali madini.
Mwarabu wa jangwani na misitu wapi na wapi.
Hao hata ukiwapangisha nyumba Ina miti wanakata wanataka jangwa wao Wana Imani eti miti inaleta majini ndio wawe wataalamu wa misitu kweli,misitu inahitaji utaalamu upi wa usimamizi.
Hao wanataka kuchimba madini mbugani kumbuka mbuga na hifadhi zote ndipo hifadhi za madini plus malikale za wajerumani ndipo zimejaa.
Hazina ya taifa ipo mbugani achana na takataka zingine
 
Mbona hukuuliza kuhusu project zinazosimamiwa/kumilikiwan a wachina pamoja na wazungu kama vile constructions, migodi na biashara kwa ujumla. Kama Tanzania kuuzwa basi Tanzania basi imeuzwa kwa wachina lakini hilo halilalamikiwi na watanzania kama wewe. Nimefanya google ya haraka haraka na nimesoma kutoka chinese official websites kuwa kuna chinese-state funded projects Tanzania zifikazo 92!!! Kutoka migodi hadi trade! Yupi kati yenu alolalamika hapa? Kuwa mkweli hasa hapa ambapo hujulikani idenditity yako halisi, sababu kubwa ya makelele yote haya sio kuendeshwa miradi mbali mbali na nchi za nje bali ni uendeshwaji wa miradi hiyo na nchi za kiarabu. Huo ndio ukweli. Next!!!!!!
 
Kuwakaribisha wawekezaji ni jambo jema, lakini ni hatari kuweka mayai yote kwenye kapu moja.
 
POSTA
 
Ongezea hapo
 

Attachments

  • F160F7BC-D31C-4D8A-AC91-AABFF60DB6F3.jpeg
    51.3 KB · Views: 3
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…