Uwepo wa UAE kwenye Mbuga, Bandari, Misitu, Tanesco: Nini kingine hatukijui?

Naomba mtusamehe!

Tulikosea pale tulipoamua Mwenyekiti wa chama awe ndio Rais kazi ya check and balance ilishindwa kufanyika ipasavyo!!

Nadhani wenye mamlaka watalifanyia kazi hilo!

Mungu IBARIKI Tanzania nchi yetu niipendayo SANA!!
Hapana mlikosea pale mlipokubali kuwepo kwa serikali mbili badala ya tatu na mkampigia makofi Nyerere, mlikosea pale Aboud Jumbe na ujumbe wake ulipokuja kutaka kuwepo kwa serikali tatu mkamcheka na mkamwambia "toka lini 1+1 = 3"! Unayakumbuka hayo au ulikuwa mdogo sana yalipotokea hayo? Yote hayo yalifanywa na CCM
 
Kwanini wanaogopa serikali moja au tatu?
 
Umesahau na shirika la posta pia.

Soon utaona ya ttcl
Tukumbushe kidogo ya posta yalitokea mwaka gani vile? Chini ya uongozi wa nani? Ukijibu hilo utajuwa kuwa hakusahau ila hailengi malengo yake binafsi. Kwa hiyo hakusahau posta, hakusahau benki na hakusahau wizi wa CAG enzi za Magufuli!
 
Mfalme wa Dubai anatoa zawadi kubwa Zanzibar kujenga barabara za ushindani wa magari Formula One.
Matrilioni yanamwagwa. Ameshaanza kuomba Grand Prix Formula Zanzibar iingie hata kabla ya South Africa. Chenji tu hio🌊👈
 

Attachments

  • Screenshot_20230621_135154_Chrome.jpg
    196.9 KB · Views: 2
Kwanini wanaogopa serikali moja au tatu?
Laiti wangelikuwa wakweli kwa hilo na pia ni kwa nini wanashadidia kuwepo kwa muungano waktii huo huo wanasema zanzibar inawatia hasara na kuwarudisha nyuma kimaendeleo. Wanasema zanzibar ni mzigo kwao lakini wao wao ndio wanaosisitiza kuwepo kwa muungano, Wazanzibari wanalia wanataka muungano uvunjwe lakini bara wanasema No!

Yaani hii ni kama vile una mke hakutaki na anadai talaka lakini wewe unasisitiza kuwa nae ilhali unalia kuwa hana faida nawe anakuzidishia umasikini na hata chakula ya usiku hakupi!
 
Kichwa cha habari nchi inauzwa
Unaingia ndani unakuta mikataba ya "ushirikiano"

Utasema aliendika hakufika hata darasa la tano...kumbe anajua anachofanya
Nakwambiaje ndugu yangu. Afya ya akili ni tatizo kubwa sana hapa nchini.

Hawa wote wana tatizo la Afya ya akili tu
 
Bado waichukue na CCM mazima!!
 
Kichwa cha habari nchi inauzwa
Unaingia ndani unakuta mikataba ya "ushirikiano"

Utasema aliendika hakufika hata darasa la tano...kumbe anajua anachofanya
Ametumia kichwa cha habari chonganishi, ni kwamba anawaachia wachangiaji wa mada kazi ya kutema sumu na nyongo zao kadri uzi utakavyokuwa unasogea.
 
Wanajua kuwa wakiwatukanisha waarabu kwa wachangiaji wa mada zao wataupata mrejesho wanaoutegemea.

Lakini ni maamuzi yasiyo na hekima wala busara, wanavunja nchi kwa kutumia nguvu kubwa badala ya kuja na hoja zisizo na sura za chuki.
 
Mikataba ya ushirikiano hata na USA alisaini mikataba zaidi ya 15
Na China zaidi ya 11..
Main point ni "ushirikiano"...

Msijitoe ufaham kuongea uzushi
Hahahahaha nazungumzia DUBAI sio USA. Asante Kwa taarifa ya US
 
Nakumbuka kuna miaka fulani tuliwasikia wenye akili wakilalamika dharau zimezidi hadi twiga anawekwa kwenye ndege.. Sasa je wakipewa uhuru wa kusimamia misitu itakuwaje... Mvivu kufikiri ataongezewa ujinga tu na anayetafuta maarifa Mungu atambarikia maarifa mengi inategemea focus yetu.. Tusiwaite wezi maana tunakuwa wavivu kufikiri kweli chui anamfundisha mamba kuogelea ili hali anaishi majini.. Kituko.. Hata Adamu hakupewa kila kitu bustan ya Eden bali aibadil akili kuwa teknolojia..
 
Shida yako ni nini? Kote ulikotaja utawakuta UK na Germany na Norway na hata Benki ya Dunia. Bwawa la Mtera lilijengwa na Kuwait, hospitali ya Mkoa ya Singida kwa kina tundulissu ina ufadhili wa Italia.

Kwa nini umechagua UAE? Au wewe ni Mdude CHADEMA au Wakilimsomimatusi Mwambukuzi una ajenda yako dhidi ya bandali ya Waalabu?
 
Mambo ya serikali ndivyo yalivyo, muda utaongea...
 
Masdar ni kampuni 3 kubwa ulimwenguni kwenye miradi ya Solar energy, Zimbabwe wanajenga mradi wa $500m, Wana ujuzi,Pesa na ni watimizaji. ABU DHABI wamejenga eneo linaitwa MASDAR CITY hambapo maturities ya umeme wote ni wa Solar tuu
 
Tusichokijua ni motive behind ya ukwapuaji huu
 
Tuwache ujinga na unafiki, kama hujafika Dubai ama Abu Dhabi au Sharjah, warlike wakiofika, hawa watu wamelibadilisha jangwa kuwa Kijani, tena miji yao iko kijani zaidi ya sie tulio na Mvua na ardhi yenye rotuba. Tunachofanya ni chuki tuu. Angekuwa ngozi nyeupe sote tungekuwa YES SIR.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…