Uwepo wa VITA duniani ni ishara pekee kuwa binadamu ni kiumbe ambaye ana akili ndogo , unatoka kwako kwenda kupigana kwa ajili ya mwanasiasa fulani!

Uwepo wa VITA duniani ni ishara pekee kuwa binadamu ni kiumbe ambaye ana akili ndogo , unatoka kwako kwenda kupigana kwa ajili ya mwanasiasa fulani!

War is madness.

Vita ni upumbavu.

Uanajeshi na Uaskari ni kazi za kipumbavu kuwahi kutokea ulimwengu.

Yani unapoteza uhai wako kisa wanasiasa wanaoketi ikulu wakila, kunywa na kushiba wakipata mamilioni ya fedha.

Halafu wewe unapiga mazoezi makali, mshahara unapata kiduchu, unaacha familia yako ikiteseka unaenda maporini kumiminiana risasi na wajinga wenzako.

Mnauana na kupata vilema vya maisha.

Ndio maana wanajeshi wengi wakitoka vitani wanapata ile Post-Traumatic Stress Disorder(PTSD) wakikaa chini na kujitafakari wanaona jinsi walivyokuwa wapumbavu.

Uhai wako ni kitu muhimu sana usiweke rehani maisha yako kwa kupambania wanasiasa wawili walioshindwa kukaa chini kutatua bifu zao.
View attachment 3222462
Mkuu umeongelea vita kwa mlengwa wa kisiasa tuu. Vipi kuhusu ugaid, uvamiz wa mipaka n. K.
Kabla haujabeza mfumo wa ulinz kiinch tafakari kwanza mfumo/askari wa mwili wako wew.
Unadhani antibodies wa mwili wako wanapambana na adui wangap mwilin mwako wanaotokana upuuz, ulafi na ukosefu maarifa wako?. Je, ni halali wangepuuza kukupambania ili ufe kwakuwa ni kosa au uzembe wako?.
 
Binadamu anaweza kuishi bila kupigana.

Sema tu ni tamaa, uchu na kutotosheka ndio kunafanya binadamu kupigania ardhi ambayo kwanza wataiacha wakifa.

Hii dunia ni kubwa sana kila mtu kupata sehemu ya kuishi.

Sema tu tumejiwekea limit na boundaries kwa kubaguana tu.
 
Vita ni sehemu ya maisha!
Jamii inayofurahi leo ujue huko nyuma walipigana kisha wakajiimarisha ndipo wanafurahia amani na utajiri walioupambania kwa jasho na damu.
Unaweza kuogopa vita ukaletewa vita, hivyo ni bora ujiandae kwa nyakati zote nzuri na mbaya
Binadamu anaweza kuishi bila vita.

Tukiondoa tamaa, uchu na wivu binadamu wote ulimwenguni tunaweza kuishi kwa Amani.
 
Binadamu anaweza kuishi bila vita.

Tukiondoa tamaa, uchu na wivu binadamu wote ulimwenguni tunaweza kuishi kwa Amani.
Ni ngumu sababu tupo wengi alafu falme tofautitofauti

Kwa masingira haya hatuwezi kukubaliana wote labda kuwe na serikali moja ya dunia tena itumie mkono wa chuma kutawala
 
Huwa nawaambia binadamu ndo kiumbe ambaye hakupewa akili Ila baadhi ya watu wanabisha.

Ebu jiulize hao M23 wanapambania nini ? Au vita ya Russia ma Ukraine ilisababishwa na nini.

Mtu unakubali kwenda kuuliwa na hao M23 kisa umetumwa na hawa wanasiasa Vilaza na wajinga ambao wanapambania matumbo yao.

Kijana jitfakari sana

Kweli wanafanya ujinga mtupu ,alikuwepo Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga na ameziacha mali zote.
 
Maisha yenyewe kiujumla ni vita.....vita ya kiroho/kiimani,kiuchumi,kiakili,kisiasa n.k

Yaani dunia ni uwanja wa vita.....jifanye mnyonge uone,na hakuna nabii ambae hakupigana vita

Na penye amani pana ncha ya upanga....
 
Vita ni sehemu ya maisha!
Jamii inayofurahi leo ujue huko nyuma walipigana kisha wakajiimarisha ndipo wanafurahia amani na utajiri walioupambania kwa jasho na damu.
Unaweza kuogopa vita ukaletewa vita, hivyo ni bora ujiandae kwa nyakati zote nzuri na mbaya
Vita si sehemu ya maisha.

Kama vita ni sehemu ya maisha mbona nchi nyingi hazitaki ardhi yao iwe uwanja wa vita?
 
Back
Top Bottom