Uwepo wa VITA duniani ni ishara pekee kuwa binadamu ni kiumbe ambaye ana akili ndogo , unatoka kwako kwenda kupigana kwa ajili ya mwanasiasa fulani!

Mkuu umeongelea vita kwa mlengwa wa kisiasa tuu. Vipi kuhusu ugaid, uvamiz wa mipaka n. K.
Kabla haujabeza mfumo wa ulinz kiinch tafakari kwanza mfumo/askari wa mwili wako wew.
Unadhani antibodies wa mwili wako wanapambana na adui wangap mwilin mwako wanaotokana upuuz, ulafi na ukosefu maarifa wako?. Je, ni halali wangepuuza kukupambania ili ufe kwakuwa ni kosa au uzembe wako?.
 
Binadamu anaweza kuishi bila kupigana.

Sema tu ni tamaa, uchu na kutotosheka ndio kunafanya binadamu kupigania ardhi ambayo kwanza wataiacha wakifa.

Hii dunia ni kubwa sana kila mtu kupata sehemu ya kuishi.

Sema tu tumejiwekea limit na boundaries kwa kubaguana tu.
 
Binadamu anaweza kuishi bila vita.

Tukiondoa tamaa, uchu na wivu binadamu wote ulimwenguni tunaweza kuishi kwa Amani.
 
Binadamu anaweza kuishi bila vita.

Tukiondoa tamaa, uchu na wivu binadamu wote ulimwenguni tunaweza kuishi kwa Amani.
Ni ngumu sababu tupo wengi alafu falme tofautitofauti

Kwa masingira haya hatuwezi kukubaliana wote labda kuwe na serikali moja ya dunia tena itumie mkono wa chuma kutawala
 

Kweli wanafanya ujinga mtupu ,alikuwepo Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu wa Zabanga na ameziacha mali zote.
 
Maisha yenyewe kiujumla ni vita.....vita ya kiroho/kiimani,kiuchumi,kiakili,kisiasa n.k

Yaani dunia ni uwanja wa vita.....jifanye mnyonge uone,na hakuna nabii ambae hakupigana vita


Na penye amani pana ncha ya upanga....
 
Vita si sehemu ya maisha.

Kama vita ni sehemu ya maisha mbona nchi nyingi hazitaki ardhi yao iwe uwanja wa vita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…