Uwezekano wa Barcelona kufungiwa kushiriki Kombe la Mabigwa Ulaya (UEFA)

Uwezekano wa Barcelona kufungiwa kushiriki Kombe la Mabigwa Ulaya (UEFA)

Pamoja na ubora wote lakini Barcelona wamekuwa wakipendelewa kupita maelezo. Ile nusu fainali na Chelsea ni ushahidi tosha
 
Chama cha Mpira barani Ulaya UEFA, inaichunguza timu ya Barcelona juu ya madai ya kuilipa kampuni ya Jose Mara Enriquez Negreira ambaye ni Makamu wa Raisi mstaafu wa chama cha marefa Hispania.

Nyaraka za mahakama zinaonesha kuwa, Barcelona imelipa kiasi cha €7.3m ambayo ni sawa na paundi 6.5m kuanzia mwana 2001 mpaka 2018 kwa kampuni hiyo.

Uchunguzi huu ukikamilika inaweza kupelekea Barcelona kufungiwa kujihusha na mashindano yote yanayoandaliwa na UEFA.

Uchunguzi huu umeombwa na bodi ya uongozi UEFA na mpaka kufikia sasa uchunguzi huu umeshaanza kufanywa na waendesha mashtaka wa nchini Hispania.

Source: Sky Sports

Siwapendi Hawa kenge
 
Sasa kwenye like game walipendelewa NINI ??! Tuanze hapo
Marefa wa Ulaya wanatumia technics za hali ya juu katika kuzibeba timu zao pendwa au walizohongwa. Angalia miaka yote hii mimi na wewe tunajua kuwa ilikuwa ni mpira wa Barcelona wenyewe bila usaidizi wowote toka kwa marefa wa Hispania kumbe kuna hongo zilikuwa zinatembea katika usimamizi wa mechi zao. Ingekuwa bongo tungeshagundua Mara moja maana wakwetu huku wanatoa penati hata pasipo stahili🤣
 
Back
Top Bottom