Uwezekano wa Magufuli kuongoza nchi kwa kipindi cha pili haupo

Uwezekano wa Magufuli kuongoza nchi kwa kipindi cha pili haupo

Da,unajua siasa brother,endelea kuelimisha watu wa taifa lako.nakubaliana na wewe asilimia mia.endelea kusema kweli.NA KWELI WANANCHI HATUMUELEWI JIWE,CCM WENZAKE HAWAMUELEWI,WAFANYABIASHARA HAWAMUELEWI,VIONGOZI WA DINI PIAka HAWAMUELEWI.WE WANT HIM OUT.
Mpaka wananchi hawataki hata kumsikia😂😂😂
 
Wananchi kwa 100% wanamtaka Dkt Magufuli atawale mpaka 2040. Tena kwa taarifa mleta mada, wananchi wako tayari kuingia mtaani kumtetea Dkt Magufuli ili aendelee kuwa rais, hao mafisadi na walafi wa madaraka waliokabidhi nchi kwenye mikono ya wezi na familia zao hawana nafasi!
Sema wewe na wenzako mnaofaidika na huu utawala wenye mambo ya hovyo kabisa!!
 
Mtoa hoja hebu wache EL apambane na afya yake....mnyukano huu uendelee tu hadi kieleweke, wakongwe wa siasa dhidi ya wageni.

CCM imewatesa sana watanzania hawa; mabillioni yakapotea katiba watu wachache wameizuia mwenye kabati...laahh

Ni wakati muafaka wa wana ccm kugawana mbao....chama kishaisha.
 
Wananchi kwa 100% wanamtaka Dkt Magufuli atawale mpaka 2040. Tena kwa taarifa mleta mada, wananchi wako tayari kuingia mtaani kumtetea Dkt Magufuli ili aendelee kuwa rais, hao mafisadi na walafi wa madaraka waliokabidhi nchi kwenye mikono ya wezi na familia zao hawana nafasi!
Una ushahidi wa kiutafiti??
 
Mtoa hoja hebu wache EL apambane na afya yake....mnyukano huu uendelee tu hadi kieleweke, wakongwe wa siasa dhidi ya wageni.

CCM imewatesa sana watanzania hawa; mabillioni yakapotea katiba watu wachache wameizuia mwenye kabati...laahh

Ni wakati muafaka wa wana ccm kugawana mbao....chama kishaisha.
Wanashindana mshindi atachukua nchi 2020. Hawawezi kugawana mbao kiasi wapinzani wakachukua 2020. Ni kwa sababu wapinzani bado hawajawa serious maana kama kuchoka watu washachoka.
 
If Tanzanians were smart enough , they wouldnt agree to be under CCM rule up to this point. What CCM has done so far to this poor country was enough to remove them from power but thanks to our education system for keeping on producing foolish people of all walks of life who cant say a word on whatever wreakless CCM does.

Ccm is a trash.
 
Na Anderson Ndambo.

Kuna mambo yanahitaji jicho la Tatu kuyaona na pengine kuyaamini. Tabia mojawapo ya siasa ni kubadilika badilika kulingana na majira na wakati kutokana na sababu za wakati husika, lakini kwa Tanzania mabadiliko haya yamekuwa na kasi kubwa mno, hicho si kitu cha kawaida, kama ambavyo Magufuli mwenyewe hakutegemea kuukwaa Urais wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa mgombea wa ccm, vilevile mazingira kama yale yanaweza kubadilisha hali ya mambo na matokeo yakawa tofauti na tunavyodhani kuelekea 2020.

Rais Jakaya Kikwete aliingia madarakani kutokana na kuimarika kwa kundi lenye nguvu lililokuwa likiongozwa na Lowassa ndani ya ccm, na kwa wakati huo ndio lilikuwa kundi lenye nguvu ndani ya chama hicho (ccm) lililoweza kudhihirika na kuweza kutoa ushawishi na kulazimisha Kikwete kuingia madarakani na kundi hilo likamkaanga vikali, Salim na kumtowesha kabisa kwenye ulingo wa siasa za kitaifa ndani ya ccm na nchi kwa ujumla. Kundi hili lilianza kujijenga tangu wakati Nyerere akiwa madarakani na kimsingi lilikomaa sana wakati wa Mkapa kiasi kwamba Mkapa akashindwa kulidhibiti.

Mwaka 2015, kundi hili lilifikia hatua ya mwisho na ya juu kabisa ya kupasuka kwakwe, baada ya Kikwete ambae ni sehemu ya zao la kundi hilo kujichomoa na kumsaliti king mwenzie (Lowassa) na kutengeneza kundi jipya ndani ya ccm. Kutokana na nguvu ya Lowassa wakati ule ccm ambayo ilitokana na kundi lake la asili, kundi la Kikwete lilikuwa na wakati mgumu sana, kwasababu lilikuwa halina ukubwa na ushawishi mkubwa kama kundi ambalo kikwete amelisaliti isipokuwa tu kutokana na Ushawishi wake Kikwete kama Rais na mjumbe mzoefu alie asi na baadhi ya wajumbe wake na wote tunafahamu shughuli waliokuwa nayo walipo mkata Lowassa.

Sasa Magufuli amezaliwa kutokana na Kundi kubwa ndani ya ccm kuvunjika kwa kusalitiana na kwa bahati mbaya sana, makundi haya yote yalijikuta yako tena kwenye uwanja mmoja (ulingo wa siasa (ccm), na katikati yupo Magufuli. Kundi la Kikwete kwa sasa lina nguvu kubwa kutokana uwekezaji mkubwa wa kikwete ndani ya serikali na ccm, lakini kundi la Lowassa ni kubwa kutokana na uzito wa wajumbe wake ndani ya ccm na ushawishi wao kwa Rais magufuli. Vita inapamba moto. Na makundi yote haya mawili kwanza hayakubaliani, lakini kubwa zaidi haya mkubali Magufuli kwasababu mwenendo wa magufjli una athari zinazo fanana kwa makundi yote na timu yake. Kundi la lowassa linatumia fursa tu, na tusisahau Ndoto ya Lowassa kuongoza nchi haijafa.

Rais magufuli anadhani yuko salama, kwasababu kuna vita ya ziada kwa makundi haya mawili, anadhani kuliimarisha kundi la Lowassa kutamsaidia yeye kupita kiulaini 2020 kwasababu ya mvutano mkali utakaozidi kuimarika baina ya makundi haya mawili ambayo tayari vita hiyo imeanza kujidhihirisha hadharani baada ya matamshi ya Bashe yenye dhana ya kisasi dhidi ya watu wa kundi la Kikwete. Kitendo hiki kimemshawishi sana magufuli kwamba ataweza kuvuka kiulaini sana. Na hili linaonesha kupata mafanikio kwasababu kundi la lowassa sio tu linapewa nyadhifa sasa na magufuli bali, limeanza kuinunua vita ya magufuli na wakina musiba wanaanza kutoweka kiana.

Kinachokwenda kutokea..

1. Kwanza tuelewe, makundi haya yote yana ushawishi mkubwa ndani ya ccm kuliko magufuli mwenyewe.

2. Makundi haya yana ushawishi mkubwa ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kuliko magufuli mwenyewe.

3. Magufuli sio tu, hana ushawishi mkubwa kwenye vyombo vya usalama kuliko mahasimu wake, Bali hata ndani ya ccm na hata kwenye nchi (Taifa) maana watu wamemchoka kabisa, kweli Raia tumemchoka kabisa.

4. Magufuli amenza kuunda chama chake kipya ndani ya ccm (ccm mpya), inayobebwa na kundi la watu ambao hawana ushawishi wowote ndani ya ccm, hawana uzoefu wa kutosha wa kuongoza nchi, hawana mizizi mirefu ndani ya siasa za ccm, kimsingi watu hawa ni wanasiasa kwenye taswira ya magufuli (magufulisim).

Sasa, mwisho wa kukomaa kwa vita hii kubwa ya mafahari wawili, itapelekea nchi kuwa kwenye hali mbaya zaidi kiuchumi, kisiasa na kijamii. Jamii itazidi kuyajua maovu mengi yaliofichwa dhidi ya ccm, bila kujali ni ccm asilia au mpya au nani, na kimsingi jamii itakuwa imejaa chuki kubwa dhidi ya ccm yote, bila kujali huyu anatoka kundi gani, kwasababu wote hawa nje ya ccm wanajulakana kama ni ccm tu. Magufuli hatokuwa kwenye nafasi ya kufanya mambo mapya, kwasababu ya mtifuano huu na mtifuano huu ndio utakao chukua nafasi kubwa zaidi kuelekea 2020 kwenye masikio ya watu na si magfuli, kimsingi magufuli atakpjikuta anafika 2020 akiwa anachukiwa kuliko mwanzo.

Itakapofikia hapo, wakati wa kufanya maamuzi ya nani anapaswa kuivusha ccm, itategemea mshindi wa kati ya makundi haya mawili, lile la Kikwete na lile la Lowassa, na kimsingi, vyombo vya dola na usalama vitakuwa kwenye nafasi kubwa ya ushawishi ndani ya nchi na ccm yenyewe kuliko wakati wowote ule, na jamii itakuwa ikiamini zaidi kwa wapinzani, hapa ndipo maamuzi ya ama magufuli au mwingine ndani ya ccm atapaswa kuwekwa kama mgombea yanaweza sio tu kufanyika na ccm wenyewe, pengine Jeshi la nchi, na kwa vyovyote vile, jeshi la nchii kwa sisi wachambuzi wa mambo haliwezi kumruhusu magufuli kuendelea na awamu ya pili. Chakuzingatia tu, wakati huo (2020) kuna uwezekano baadhi ya watu hatutakuwa nao, kimwili au kisiasa, akiwemo Magufuli mwenyewe. Hapa ndipo namuona Lowassa akiibuka tena.

Watu wanaosema, ccm imekuwa ikifikia hatua kubwa ya mpasuko, na huweza kujinasua upya, wanasahau wakati huo, kulikuwa na kundi moja, na baadae likaongezeka hili la pili ambalo limejengeka kwenye msingi wa visasi, na sasa tuna makundi mawili yenye nguvu yasiokuwa tayari kupatana na kukaa meza moja, kitu ambacho hakijawai kutokea huko nyuma.

Hichi kinacho onekana Lowassa na Rostam kumuunga mkono Magufuli si kitu cha kufuraia sana, usishangae 2020 mgombe wa ccm akawa Edward Lowassa na sio Magufuli tunae dhani ndie. Mwelekeo wa mambo wa sasa unabadilika kwa kasi kubwa sana, na kuna kila dalili za ccm kufikia tamati, ijapokuwa kweye mazingira tata sana. Lowassa ni mzuri sana kwenye kuficha na kulinda hadhi yake yeye binafsi. Mwaka 2015 kuna utafiti ulionesha ndie amgombea pekee aliekuwa na ushawishi mkubwa kuliko wanasiasa wengine kwa tofauti ya asilimia 11 akifuatiwa na Dr. Slaa. Huu ni ushawishi binafsi bila chama. Na kimsingi anajua jinsi ya kuwatumia wengine, na ana watu wenye weledi mkubwa kwenye kumlinda tofauti na magufuli anaetetewa na vichaa kama musiba.

Naendelea kutoa ushauri kwa vijana wa ccm, kujaribu kuchagua upande sahihi mapema na sio kukesha kupyauka, leo unamtukana huyu, kesho unamtukana yule, mwisho unajikuta unatakiwa kumsifia mtu uliemtukana jana, utasimamaje? Vijana muwe wenye hekima sana, na pengine mjitaidi kunyamaza kimya, unaedhani ana nguvu leo, kesho unaweza kumkuta ni laini kama siagi......kuni zinawaka moto sana....

A. Ndambo
Kwani ninyi mnawashwawashwa na nini si muache wauane tu?Ninavyoichukia cvm basi tu
 
E. L akaombewe kwa T. B. Joshua
Na atarudia afya yake njema na nguvu
 
Yeye hana kundi mpaka ajipeleke kumdi la Lowassa?
Hakuwa nalo. Sema hawaamini watu. Hata wa kabila lake nao anawahisi watamsaliti.

Kuunda kundi ni trust na interest zaidi. Sasa mtu anataka kuunda kundi lake chini ya DAB unafikiri atafanikiwa?
 
E.L. Aende kwa T. B. Joshua akajue kinachomtatiza huenda hako Kaugonjwa ni kisingizio tu.

Aende jamaa akiwa kutulia anaweza kumueleza mengi ya kinabii
 
Wabongo wengi hawajifunzi kuwa na akiba ya maneno.
Tuna mifano mingi tu ya wachangiaji huko nyuma ambapo leo wanaona aibu wengine wameacha kbs kuwa memba wengine wamebadili IDs.

Tujifunze kuchangia hoja na sio kuleta vioja kwa mtoa mada. Dhihaka sio kitu chema,kama hukubaliani na jambo kutokuwa na sababu,onesha hivyo tu itoshe sio kutoa lawama na pengine matusi.

Kuna watu humu walitoa hoja zao zikawa,tukawapongeza kama manabii, GT,wabobezi n.k. isije fika siku huu uzi ukaibuliwa kama kaburi na kuanza kuzikimbia comments zenu.

Tuijadili hoja kwa kuweka hoja zetu hata kama ni mfia dini kundi fulani,chama,ama mtu.
 
IUkiachilia mbali hoja yako hafifu ya ushawishi, naomba sana usisahau kuwa Magufuli ndiye anayeshikilia dola, na ndiye atakuwa anashikilia dola mpaka wakati huo. Sasa niambie nani mwenye nguvu zaidi kati ya ANAYESHIKILIA DOLA na MWENYE USHAWISHI WA DOLA. Kumbuka pia kule kwa wenzetu wenye ushawishi dunia nzima, aliyetakiwa kuwa Rais siyo yule ambaye ni Rais muda huu. Unajua ni kwa nini? Do not do under-estimate the powers of the President of URT. Rais ni Rais!
Ndiyo maana kwa muda sasa hatujawahi kuwekewa rais mpya aliyefungamana na rais aliyetoka. Hapo tujiulize nini hutokea pamoja na kuwa na hizo 'powers'.
 
Uzi wako umeharibiwa na story za low wa saa.
Unaweza vipi kuizungumzia CCM bila kumzungumzia lowassa,kikwete mwenyewe alimtegemea lowassa kuwa rais.Bila nyerere mkapa asingekuwa rais bad boys lowassa&kikwete walikuwa wanachukua nchi ile 1995.by the way toka kuumbwa kwa CCM mtu aliyependwa na watu wote wana CCM na wasio CCM ukimtoa nyerere ni lowassa,sijui historia ya siasa ya nchi hii huijui au unajifanyisha
 
Anza tuition ili umuelewe, maana jamaa yupo yupo sana tu !


Wakati wanaume tukiongea mustakabali wa nchi yetu na vizazi vyetu wewe mtoto wa kike usichangie mada,nenda ukachambane na wanawake wenzako.hatufanyi mipasho hapa.UMESIKIA WEWE MARIAMU?
 
Hata hivyo E. L. Anapaswa kuwaomba msamaha wote alowakosea kwa kujua au kutokujua kama binadamu wengine tunavyopaswa kuzingatia !

Mungu atuhurumie siasa hususa za bongo zinamambo mengi sana maana mmnh!
 
Back
Top Bottom