Toka nje ya jumba la kioo ambalo unaona kila kitu kinachotokea nje lakini huna jinsi ya kufanya mawasiliano yoyote ya moja kwa moja
Mrembo by Nature nipe muda kwenye hili nisikurupukemshana jr
Naomba kujua haya
1. Nina ndugu yangu alinilea na kunipenda Sana toka nikiwa mtoto. ninamuota tunaongea marakwamaramarakwamara. Tunaongea mengi ila linalonisumbua aliwahi kusema bila mumewe asingekufa. Na mumewe toka arobaini ya marehemu hajawahi kujua waatoto wanaishije huu mwaka Wa 10.
2.kuna siku aliniambia ndotoni kwamba yeye hajafa ila mwanae ambaye (huyu mwanae yuko hai ndio mama yake alikufa wakati anamzaa. Alijifungua pre mature vizuri then wakamuover dose akafa. Swali why aseme alokufa sio yeye Bali mwanae ambaye ni hai? Why mumewe amlalamikie?
Mrembo by Nature nipe muda kwenye hili nisikurupuke
Nimelitafakari nimemeditate Kwa muda hili ni kubwa kwangu Ila kw ufupi tu n kwamba huyu nduguyo bado roho yake inaishi na hajawa radhi kupumzika kaburini anasubiri kisasi au anasubiri ukweli ujulikane
Huyo mumewe ana Siri kubwa sana moyoni ila hana amani na anatumia sana nguvu Za giza kulizima hili. Ila lina mwisho wake na wakati utalakapotimia na akalitema wewe ndio utakuwa shuhuda, na huu ndio ukweli
Kwenye hicho kifo cha huyo mama na huo mkangangiko wote kuna kitu kisicho cha kawaida kilitokea na bado mumewe akihusika kwa Karibu.....lakini ni suala la muda tuu
Dunia ina mengi yaliyo kizani na mwanadamu amenyimwa ufahamu WA kuyajua yote
Duh asante Sana. Nasikia Alafu alinitafuta sana anione ila nilikuwa shule by then (coz walihamia kwingine) . Nilipanga kumtembelea wakati wa likizo (bila kujua kwamba hata yeye alikuwa ananitafuta). sikumaliza hata wiki akafa. Tumekuja kuonana yeye ni marehemu.
Nilimpenda alinipenda .... haipiti muda mrefu namuota tunaongea Kama mtu hai. Story kabisa nikistuka ni ndoto. Ila ninakosa raha sana. sasa najiuliza why yeye tu wakati waliokufa ni wengi kwenye tumbo lao?
natamani siku nijue sababu haswa ya kifo chake.
Nimekuwa nikiwajali wanae, wanalelewa na mama yangu... au labda ni vile nawapenda na kuwahudumia ndo maana haishi kunijia?
Hapo ataongea na pepo tu hakuna mawasiliano baina ya mfu na binadamuKuna strong bound kati yenu tangu akiwa hai, kwa maana ya kuvaa huu mwili wa kibinadamu, na kukutafuta kule alibeba siri nzito ambayo alitaka kukwambia wewe wetu, ikashindikana lakini ile WILL POWER ilikuwa ni kubwa kiasi kwamba alijiapiza kuwa atakwambia hata atakapokuwa hana mawasiliano ya moja kwa moja ya kibinadamu nawe
Ishu ya kuwaangalia wanae vizuri imezidisha ile strong bound iliyokuwepo kabla na usingefanya hivyo ama angekutokea na kukwambia au angekaa kimya na kusononeka ila ungejua tuu
Fanya hivi tafuta siku moja unuie kuonana naye ama la kukwambia kile kilichofichika....siku hiyo funga tangu asubuhi sanasana kunywa maji tuu, ukiweza jifungie chumbani ukikata mawasiliano yote na ulimwengu wa nje, fanya hivyo mpaka usiku
Hii inaitwa unveiling secrets meditation, muda muda wote akuambie, kwa upole na unyenyekevu ukimuahidi kuwa utamsaida UTAKAPOWEZA kama akikwambia
Fanya hivyo mpaka usiku, unaweza kuja kupata majibu usiku wa manane lakini pia ujiandae kwakuwa anaweza kukutokea...hakikisha chumba ni kisafi kabisa na haingii mtu yeyote yule halafu weka kitu alichokuwa anakipenda sana mfano nguo marashi uturi nk
Roho ni uhai nafsi ni utambulisho
Nafsi haifi kwakuwa haina uhai bali nafsi hubaki kama utambulisho kinachokufa ni mwili kwa maana ya roho kuuacha mwili milele
Je hii roho ambayo ipo na nafsi huko kwenye ulimwengu mwingine inajitambua, kama inajitambua inamaana inaweza kupenda au kuchukia na kwa hili ukamilifu unapatikanaje huko kwa Mungu
Kila kitu hufanyika ndani ya jumba la mwili uharibikao baada ya hapo roho hugeuka kuwa pepo
Mkuu #mshana jr nisaidie kitu. Mimi huwa nahisi jambo kabla halijatokea muda mfupi. Ingawa si mara zote ila mara nyingi huwa hivyo. Kwa mfano siku moja nilikuwa chini ya mwembe nikahisi nadondokewa na embe ile kutoka tu pale embe likaanguka. Kuna siku nilikuwa namdai jamaa nikahisi kapata hela na atanipigia na kweli sekunde ileile akapiga. Pia ipo siku nilihisi umeme utakatika usiku so nikawaambia wawashe mishumaa kabla ya kuanza kula na kweli umeme ukakatika. Mifano ni mingi ila ukweli ndio huo. Nina nini mimi?
Ni sixth sense ambayo wengi huitafuta kwa njia ngumu ya meditation lakini tayari wewe unaimiliki kiswahili cha kawaida ni machale
mshana jr: Naomba kujua jambo hili hapa
Mimi mama yangu mzazi alishafariki tangu mwaka 2013, ila ninamuota mara kwa mara naweze nikahisi nipo naye tunaongea lakini nikishituka najikuta nipo kitandani nimelala. wakati mwingine namuota ananipa vitu na mimi napokea. Wakati mwingne hunioji kama naweza kusamamia baadhi ya vitu hapa home n.k
je hii ina maana gani? Mana nimejaribu kusali na kuikataa hii hali lakini inajirudia
Mshana mbona majibu yanatofaitiana... awali ulisema kila kitu hufanyika ktk mwili baada ya hapo rpho inakua pepo na hapo juu anaesema anaongea na ***** unasema Guardian angel... im confused
Na kuna mtu alifiwa na nduguye akawa anamtokea na kumwambia wabaya wake na mambo yanayoendelea nyuma ya pazia i mean wanaoifanyia ushirikina familia hiyo na kilichoshutua zaid akamwambia muwe mnasali juu ya kaburi langu mtapata baraka nyingi... hii sijui unaiongeleaje Mr. Mshana...