Uwezo wa kuongea na wafu: Elimu Iliyoshindikana duniani

Mwaka 2016 nilifiwa na mama mzazi baada ya kumuuguza sana nyumbani na pale kcmc, nilikuwa karibu sana naye.

Ikatokea jioni moja dada mkubwa akaja kunipokea ili akesha pale, japo mchana nilishinda nampaka dawa maana mwili sehemu sehemu zilianza kuungua.

Muda wote nikiwa naye akiwa ICU (tulipewa kibali maalum cha kukaa mle ndani ICU ) nilikuwa namwimbia nyimbo za kanisani na kumsomea neno la Mungu. Japo hasemi ila nilikuwa nasogea karibu na sikio au moyo wake nakumwambia mama uende na neno la Mungu, nilijua hawezi pona tena.

Muda kidogo niliambiwa mama hayupo tena.

Siku ya kufuata mwili nilikuwa mbele sikutaka sikose kuona process yote .

Walipomtoa kwenye yale makabati aligeuza shingo nikawa natazamana naye uso kwa uso.

Mshana Jr mama alinichekea, naapa alicheka na ile tabasamu iliendelea kosa nililofanya nikamshtua mdogo wangu nikamwambia ona mama hajafa mbona ananichekea, yaani pale pale akabadilika na tabasamu ikaondoka.

Kweli maiti inaongea.
 
Mtani lile tabasamu lilikuwa lako na si la mtu mwingine yeyote
 
Hizi zote ni hisia za mtu mhusika au wahusika katika tendo la kumwandaa marehemu. Hakuna uhalisia wowote hizi zote ni hysteria tu au woga walionao watu husika. Biblia ina sema msihangaike na hoa waliolala katima umauti kwani hakuna chochote wanachoweza kukusaidia wala sisi kuwasaidia huyo alielala katika umaiti.
 
Haya sawa.. Asante kwa kushiriki mjadala
 
Huyu Jamaa vijimambo vyake huwa ni vifupi2 visivyoeleweka ingawa wasiyojua mambo haya humsifia sana! Eleza Jambo kwa ufasaha na mifano ili ueleweke, ujue kuna wataalam humu wanakuangalia tu!
 
Ghafula pale chini sakafuni nikaona noti ya shs 10. Enzi hizo za '70 hiyo ilikuwa hela kubwa sana. Kama laki+ leo. elfu 10 je hii noti tayari ilikuwepo?
 
Ghafula pale chini sakafuni nikaona noti ya shs 10. Enzi hizo za '70 hiyo ilikuwa hela kubwa sana. Kama laki+ leo. elfu 10 je hii noti tayari ilikuwepo?
Itakuwa ni typing error... Most likely alitaka kusema noti ya shilingi mia moja
 
Nikiwa mtu ambaye nilidili na miili ya marehemu kwa miaka mitatu mfululizo nilikutana mara nyingi tu na hizi hali, marehemu hataki dharau ubishi au kufokewa nguo hata iwe inamtosha Siku hiyo itakataa mpaka mumbembeleza
Hii niliisha ishuhudia- jeneza lilkataa kuingia katika gari mpaka wakagundua kuwa marehemu hakupendezwa na baadhi ya mambo waliyopanga ndipo likaingia
 
Inawezekana.Tabu inakuja hapa,hiyo process mnufaika ni nani?
 
Kwa uelewa wangu nakataa kabisa. Ni jambo linalowezekana kwa 100% kuongea na wafu. Nasio tu kuongea nao ndotoni hata moja kwa moja kanakwamba wapo hai.


Nikusaidie kitu Kaka. Hii sio elimu tu hapana ni kipawa ambacho kinakuwa connected kiuteule, nina ushahidi wa watu na tafiti kadhaa wenye kipawa chakuongea na wafu.


Pia inaweza kuwa elimu sababu kuna mtu aliwahi kuniambia nikitaka anaweza kunipa elimu na maarifa yote juu ya kuwa connected na wafu. So Duniani kuna maarifa ya Siri sana na maarifa haya yapo kwa watu wachache sana.
 
Pia inaweza kuwa elimu sababu kuna mtu aliwahi kuniambia nikitaka anaweza kunipa elimu na maarifa yote juu ya kuwa connected na wafu. So Duniani kuna maarifa ya Siri sana na maarifa haya yapo kwa watu wachache sana.[emoji1545]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…