Naweza jaribu kukujibu kama ifuatavyo, neno pixel ni kifupi cha neno picture elements terminology hii inaonyesha uwezo au ubora wa picha(resolution) katika kamera, computer screen(monitor) au TV. Ubora huu unategemeana na jinsi kifaa hicho kilivyo tengenezwa kiwandani kimsingi uwezo wa jicho la mwanadamu huwezi kulipima kwa mfumo huo kwa sababu jicho lina uwezo mkubwa zaidi ya huu wa camera za kawaida.
Kuhusu uwezo wa ubongo wa mtu nao pia ni vigumu kuupima lakini storage capacity yake yaweza kuwa infinity lakini kumbuka binadamu ameumbwa kusahau hivyo anapo sahau anaupa ubongo nafasi ya kuhifadhi vitu vipya. Pia uwezo wa akili unatofautiana kutoka mtu mmoja kwenda mwingine.