Uwezo wangu wa kununua mzigo na kupeleka sokoni unapungua

Uwezo wangu wa kununua mzigo na kupeleka sokoni unapungua

mwanyaluke

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2015
Posts
704
Reaction score
2,435
Uwezo wangu wa kununua nafaka kutoka kwa wakulima na kupeleka sokoni kwa ajili ya walaji unazidi kupungua, mzigo niliookuwa nakusanya kwa milioni kumi nahitaji kupata kwa milioni 13, 14.

Nipo Ikungi Singida muda huu nilikuwa napita kwa wakulima natafuta alizeti na mahindi, ni kweli mashambani mazao yapo changamoto ni bei zake, sielewi kwa bei hizi nikinunua nitauza kwa bei ipi.

Hii hali ipo pia dukani mzigo wa duka uliokuwa unachukuliwa siku za nyuma na unaochukuliwa sasa ni tofauti na kila ninapouza ni lawama kwa wateja, faida ipo kiduchu sana.

Najiona naenda kufirisika kabisa otherwise nibadili biashara tu.

Maombi yenu.
 
Jitulize, ndiyo hatua ya kwanza. Ondoa cash zote, zihifadhi kwa siku 3 hadi wiki uangalie eneo lipi lenye unafuu.
Kama njia ina utelezi na miba, ukakomaa kupita, utakosa wa kumlaumu mbele ya safari.
 
Kuna vitu vinaendelea kwenye uchumi ukichanganya na siasa za CCM vinazorotesha sana maendeleo ya wafanyabiashara wadogo.
 
Back
Top Bottom