Uwiano sahihi kati ya mchanga na cement mfuko mmoja kwa ajili ya kuchapia nyumba

Uwiano sahihi kati ya mchanga na cement mfuko mmoja kwa ajili ya kuchapia nyumba

Kuna sehemu nilikuwa nafanya kazi za saidia fundi tulikuwa tunaweka ndoo ndogo (zile za lita 10) 30 za mchanga kwa mfuko mmoja wa cement
Ahahahahahaah huko itakua mbagala au chanika huko ndani ndani
 
1.nje: kama mazingira magumu mfano unyevunyevu tumia 1:3 ila kawaida kabisa ni 1:4
2: ndani tumia 1:5 kwa mchanga mnene au 1:6 kama mchanga ni laini
hizo ratio ni ujazo (volume) na sio uzito
Unaposema 1:3 unamaanisha mfumo mmoja wa cement, je hiyo 3 nini, ndoo za mchanga, dololi au ndoo kubwa?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
 
Unaposema 1:3 unamaanisha mfumo mmoja wa cement, je hiyo 3 nini, ndoo za mchanga, dololi au ndoo kubwa?

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Kwanza tuelewe hiyo ni ratio ya ujazo.
Sasa kama utapima cement kikombe 1 cha chai then tumia kikombe hicho hicho kupima mchanga vikombe 3.
Mfuko wa cement unakisiwa kua na ndoo 2 kubwa zile za 20lts japo sio sahihi, then tumia ndoo hiyo hiyo kupima mchanga mara 3 ya cement utapata mchanga ndoo 6.
I like teaching!!!!
 
1.nje: kama mazingira magumu mfano unyevunyevu tumia 1:3 ila kawaida kabisa ni 1:4
2: ndani tumia 1:5 kwa mchanga mnene au 1:6 kama mchanga ni laini
hizo ratio ni ujazo (volume) na sio uzito
Mkuu mimi mchanga wangu ni mlaini na natumia cement ya 42.5 sehemu hiyo Ina unyevu nyevu. Pia kama unajua dawa ya fungus kuchanganya na udongo wakati wa plaster naomba uniambie inaitwaje.
Naomba msaada wako tafadhali.
 
Back
Top Bottom