Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Nina girlfriend wangu ambaye amekuwa ni mchumba wangu ila huenda kuanzia sasa uchumba umeisha baada ya kugundua kuwa nimemdanganya.
Nilipokuwa chuo nilizaa na wanawake wawili tofauti si unajua tena mambo ya ushamba.
Baada ya kupata kazi nikapata mchumba ambaye ndiye huyu sasa. Tuna mwaka mmoja na nusu na kwa kipindi hicho chote sikuwahi kumweleza kuwa nina watoto wawili. Yeye alikuwa anajua kuwa ninao wawili. Moto wake si mdogo, kavunja vyombo vyote kabatini, kavunja dressing table, kavunja coffee table yaani ni kasheshe, binti kapandisha majini ya kichaga. Najaribu kumtuliza hatulii, naombeni mnisaidieni kwani nampenda sana na ninamuhitaji maishani na sikupanga kumuumiza moyo
Ishu yako imenikumbusha mbali.
Hao watoto amewakuta asipanic sana. Wangekuwa wamezaliwa wakati mshaanza mahusiano ingekuwa mbaya zaidi.
Mwambie ulimficha ukihofu kuwa atakuacha na wewe unampenda, ukweli umejulikana hujui ufanyaje kwahyo mwamuzi ni yeye ila unajutia kwa ulichofanya.
Uwe mpole wakati unaongea.
Hebu fafanua hapo kwenye rangi Mkuu
pole sana mzee, hapo pazito, ushauri ni kwamba mtafute mtu ambaye ni trustworthy na ambaye gf wako anamweshimu na kumuamini, ajitaidi kumtuliza hasira. N.B tumia njia hii baada ya kuona kuwa njia zote ulizotumia zimeshindwa kufanikiwa kabisa, kwanini? sababu kuu ni kuwa mambo ya mapenzi mara nyingi wahusika ndio uweza kuyamaliza matatizo wenyewe ndani kwa ndani.
daahhh
Je ulimwambia au yeye aligundua kwa njia zake mwenyewe??
bwana weee yeye alijua kuwa nina mtoto mmoja kumbe ninao wawili
bwana weee yeye alijua kuwa nina mtoto mmoja kumbe ninao wawili
Kagundua mwenyewe
Ulipofikia kanivunjia vitu nikahisi tu wa kili mi 1 alivunja kila kitu mpaka tv,deck hadi vitanda na alitaka kuchoma nyumba tena ya kupanga majirani wakamwahi, wanapenda jumla na hawapendi uongo,pole sana kuwa mpole atakusamehe.