Nawasalimu nyote mtakaosoma story hii!
Awali ya yote nipende kusema kwamba yote nitakayoandika kwenye story hii ni maelezo yangu ya kweli na nimeyaishi.
Hivyo basi story yangu ni ya kweli na ilikuwa mapito yenye ukweli ndani yake:
Nimezaliwa kijiji kimoja wapo wilayani Rufiji mkoani Pwani.
Tulizaliwa watoto watatu tukiwa wote wa kiume nikiwa wa kwanza kuzaliwa. Baba alikuwa mfanyabiashara wa biashara ndogondogo na kumfanya kuwa tegemeo kubwa ndani ya ukoo.
Alikuwa wa kwanza kuzaliwa ambapo baba yake alifariki akiwa tayari ameshaanza kujitegemea kimaisha. Mara baada ya kifo cha babu kilimfanya baba kuwa tegemeo kuu hususan kwa wadogo zake.
Mnamo mwaka 1980 dada yake mmoja aliolewa na mwanaume wa kijiji kimoja kutoka Mkuranga. Huyo mwanaume alikuwa mkulima wa mazao ya chakula. Shangazi yangu huyu alibahatika kupata mtoto wa kike mwaka 1982 lakini kwa bahati mbaya mwaka uliofuata mtoto huyo alifariki dunia kwa ugonjwa wa surua. Tangu wakati huo shangazi hakubahatika tena kupata mtoto .
Nikiwa na umri wa miaka mitatu shangazi alikuja kuwaomba wazazi wangu ili anichukue na kunilea,ambapo ombi lake lilikubaliwa. Wakati huo wazazi wangu walihamia Dar es salaam na baba aliendelea na biashara zake ndogondogo sokoni Buguruni. Alibahatika pia kujenga kajibanda eneo la vingunguti.
Ilifika mwaka wa kuanza shule ambapo shangazi alinianzisha shule darasa la kwanza. Nilipofika darasa la nne baba alifariki dunia kwa kuugua ghafla tuu! Nakumbuka siku ya kuumwa kwake tulipokea taarifa na haraka shangazi alinichukua na kwenda pamoja hadi kwa baba Vingunguti. Kwa bahati mbaya nilimkuta ameshakata kauli na Baadae akaaga dunia.
Mazishi yalifanyika na baadae tukarudi Mkuranga mimi na shangazi yangu. Mdogo wangu wa kwanza alichukuliwa na mama mkubwa na mdogo wangu wa mwisho alichukuliwa na baba mdogo. Mama naye alichukuliwa na dada yake kwa kujipumzisha.
Wakati nikiishi na shangazi nilipatiwa mbinu mbalimbali za kujitegemea kama usafi wa nguo zangu, kilimo pamoja uuzaji wa bidhaa ndogondogo kwa kutembeza mara baada ya kutoka shuleni na siku za mwisho za juma.
Kikao cha ukoo kilikaa na kuamua kile kibanda pale vingunguti kiuzwe ili kulipa deni la sh elfu arobaini aliloliacha marehemu. Pia walikubaliana wanaukoo kwamba pesa itakayobaki tununuliwe eneo nje ya jiji kwa ajili ya mama na sisi watoto. Nje ya deni lakini pia nyumba ilionekana ina mikosi na nuksi hivyo haifai tena. Cha kushangaza pesa iliyobaki ililiwa yote na kutoambulia chochote.
Mama alishindwa kuishi kwa dada yake kutokana kutoweka kwa maelewano baina ya mama na dada yake. Alihamia kwa kaka yake na kwa bahati mbaya naye aliugua kwa muda mfupi mwishowe akafariki. Alifariki nikiwa darasa la sita ikiwa ni miaka miwili baada ya kifo cha baba.
Shangazi alizidi kunilea na kuninyoosha hasa kwani Alikuwa mkali kama nilivyosema hapo awali. Nilianza kujitegemea kwa kuanza kuuza biashara kuuza ndizi mbivu kwa kuzitembeza kwenye kituo cha mabasi.
Nilimaliza elimu yangu ya msingi na kuchaguliwa kwenda sekondari. Kabla ya kuanza sekondari baada ya kumaliza shule ya msingi nilijiingiza kuuza mayai ya kuchemsha kwa kutembeza mitaani na kituo cha mabasi. Niliweza kupata fedha zilizoniwezesha kupata mahitaji muhimu ya shule.
Ilikuwa ni shule ya kutwa hivyo ilinilazimu kujitegemea kwa kila kitu kama kupanga chumba na kujiandalia chakula. Shangazi yangu pekee ndiye aliyehakikisha ananitimizia mahitaji yangu. Kipato chake kilikuwa duni mnoo kwani alikuwa akitegemea vibarua na biashara ndogondogo. Hakuna mtu yeyote aliyetoa msaada juu ya kusoma kwangu.
Hakuweza kulipa ada na kusabishwa kufukuzwa shule kwa hatua za awali. Ilinibini niende kwa afisa elimu nikiambatana mwenye nyumba ambaye alinishauri kwenda kwa ajili ya kupata msaada.
Tulifika na kumuelezea tatizo letu ambapo aliandika kimemo cha kwenda kwa mkuu wa shule. Tulikipeleka kile kimemo ambapo mkuu wa shule alikisoma na kuniruhusu kuendelea na masomo.
Shangazi alizidi kupambana ili anisaidie kwenye chakula,nami pia kipindi cha likizo nilikuwa nikiendelea na uuzaji wa mayai ya kuchemsha.
Wadogo zangu walimaliza darasa la saba lakini hawakubahatika kuendelea na masomo. Hivyo nawo walikuja kuishi kwa shangazi.
Nilimaliza kidato cha nne na nilibahatika kupata division two. Nilipangiwa shule ya advance mkoani Iringa.
Nilipohitimu kidato cha nne niliendelea kufanya biashara ambapo ilifikia wakati niliweza kusafirisha mihogo na kuiuza soko la Buguruni. Nilipata pesa ambayo ilinisaidia kupata mahitaji ya msingi ya shule pamoja na nauli.
Nilifika shuleni ila sikuwa na ada ya shule, pia sikubakiwa hata na shilingi mfukoni. Kila mara nilitolewa darasani hivyo ilinilazimu kumdanganya mkuu wa shule kwamba nafadhiliwa na shirika linalosaidia watoto ya kutoka Mkuranga. Niliishi kwa uongo huwa japo niliendelea kusumbuliwa kila wakati.
Nilivyofika kidato cha sita mdogo wangu wa pili alitoka kwa shangazi na kwenda kujitegemea Dsm ambapo alijishughulisha na kazi ya upasuaji mawe na kuyauza.
Aliweza nisaidia kwa pesa za matumizi pamoja na nauli. Wakati huo mdogo wangu wa mwsho alikuwa akifanya biashara ya kuuza mayai ya kuchemsha ambayo biashara niliyoiasisi.
Nilimaliza kidato cha sita na kurudi kukaa kwa mdogo wangu ambaye alikuwa amepanga chumba na kujitegemea. Nilitaka kujiunga na kazi yake ila alikataa kabisa. Alinisaidia sana kwa kunipa hela ya matumizi na hata fedha ya mtihani wa kidato cha sita alilipa yeye.
Nilibahatika kupata division one na kujiunga na chuo kikuu cha DSM. Nilipata mkopo asilimia mia moja hivyo niliweza kutoa kiasi cha pesa ya boom na kumlipia ada ya mafunzo ya udereva mdogo wangu wa kwanza.
Alihitimu na baadae alipata kazi ya udereva wa daladala. Alifanikiwa kuoa na kujenga nyumba ya kisasa nje kidogo ya jiji la Dsm.
Nilivyoingia mwaka wa pili nilimpa pesa ya mtaji mdogo wangu wa mwisho aliyekuwa Mkuranga na kuanzisha duka la vyakula ambalo aliweza kulianzisha na kuliendeleza likawa kubwa hadi kufikia duka la jumla. Aliwekeza pia kwenye kilimo cha mihogo,ununuzi wa mashamba na viwanja. Pia alifanikiwa kujenga nyumba ya kisasa.
Nami nilimaliza chuo ila sikuweza kupata kazi hivyo nilijishikiza kwenye kufundisha tuition kwa miaka miwili. Niliamua kwenda kusoma postgraduate kwa ufadhili wa wadogo zangu.
Nilimaliza na baadae nikapata kazi Serikalini ambapo nilioa na kupata watoto. Nilifanikiwa kujenga nyumba pia.
#Mungu mbariki shangazi
#Mungu wabariki wadogo zangu

Upvote
8