Uzalendo kitu gani?

Uzalendo kitu gani?

Mtambwe

JF-Expert Member
Joined
Apr 14, 2014
Posts
758
Reaction score
926
Aandika Mohammed Ghassani

Uzalendo gani!?

Mpendwa muheshimiwa, anapanda jukwaani huku mbweu anatowa, anukia biriani tutakaohutubiwa, hatuna kitu tumboni

Muheshimiwa ajuwa kwamba watu wana njaa lakini kalewa pawa.

Basi anatuhimiza: “uzalendo ndu’ zanguni!” “uzalendo!” “nchi yetu!”, hii misamiati gani mzalendo hapa petu, hugezwa kwa jambo gani. Ni mtu asiye kitu, fukara na masikini?

- ama ni ule mjitu

- ada uliofurutu

Wenye nyumba tatu tatu?

Kama ndiye mzalendo, akina miye tu nani?

Uzalendo kuridhia, bwana analobaini?

Isiwe kuulizia, ‘utavuruga’ amani hata akikuibia, umwambiye: ‘shukurani!’ maishaye yamwendea ya kwako yadidimia bali ‘sijekumbushia! Ndio huu uzalendo, tutakwao tuamini? Geukia kwa mkubwa, uzalendowe ni nini:

Kujenga kasri kubwa, magari kwa dizaini fedha nchini kuiba, kupeleka ugenini kukuza yake nasaba kwetu kuleta misiba na sisi tuko “twayiba” huyu ndiye mzalendo, nchi inotumaini?

Yeye aponda maraha, mimi kijua kichwani wakati mimi nahaha, yeye yuko shereheni kila sikuye furaha, kila ya kwangu huzuni

Wallahi hii karaha ninacheka sina jiha kicheko kisicho siha kama yeye mzalendo, mimi siye nijuweni!

Kutoka diwani ya andamo: msafiri safarini

215367115_10159468670979655_8884452533818256317_n.jpg
 
Back
Top Bottom