Uzalendo ndio huu, Dar-New York kwa B787-8 gharama ya mafuta ni TZS 267M

Ni kweli nakubaliana na mtoa hoja kwamba iwapo angetumia ndege ya serikali gharama zingekuwa kubwa zaidi . Hivyo kutumia ndege ya usafiri wa uma gharama zimekuwa nafuu. Hongera kwa kuliona jambo hili
 
Yote siyo muhimu hayo...

Tunachokitaka sisi kwa sasa kama taifa ni MARIDHIANO YA KITAIFA...

Maridhiano ya kitaifa yachagizwe na demokrasia ya kweli, haki kwa wote na uhuru wa watu...

Hata hivyo, tukirudi kwake Rais Samia, hivi ni sababu gani ilimfanya aambatane na msururu wa watu 50 au 25 au hata 10...?

Wote wa nini hawa kwa sababu alikuwa anakwenda kwenye kikao tu na wala haikuwa ziara ya kiserikali?

Ni kwanini asimwige mwenzake Haikainde Hichilema aliyekwenda na maafisa wengine wasaidizi wake watatu tu; walinzi 2 na mbeba mkoba 1 na bado kaupiga mwingi kuliko madikteta kadhaa wa Afrika kama Rais Samia, Museven, Kagame...???
 
Unapofikiri unasifia kumbe unaharibu...., Bure hizi hoja ungeachana nazo kuliko kuwakumbusha watu.... ?

Unajua uzalendo zaidi na kupunguza gharama ? Kwenda na delegation ya watu wachache.
mpiga picha wa Nyerere anasema Nyerere alikuwa anaenda na mkewe tu
 

kulikuwa na upotoshaji kweli
 
Hakuna cha gharama, hiyo bora isingetumika hata senti kwa uongo was wazi alioenda kuongea juu yetu huko Duniani.
 
Mbona linapoondolewa kwenye ramani ya dunia hawakutwambia nani aliyefanya hivo na tulipata hasara gani au hasara ndo kutegemea ajira ya machinga kila mahali maana tulipoteza wawekezaji.
 
Ebu acheni kutuletea ujinga wenu hapa. Mtahangaika naye sana huyo mtu wenu.
Tunataka kichwa kama cha JPM ambaye alitumia akili zake kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeshea miradi, na alifaulu sana.
Hatutaki mtu anayetumia akili zake kuzurura huku na huko kutafuta misaada, mwisho wa hiyo misaada ni kuuza Nchi.
"There is no free lunch in the World"
RIP, JPM Baba yetu. Tunakukumbuka sana. Mungu akupe heri ya milele. Amina.
 
Hivi yule mkulima tulishamalizana nae?
Kama hatukumalizana nae vp kuhusu usalama wa njiwa wetu akiruka mbali?
Sawa, Ila aliiache uchumi unakua kwa 2.1% toka 6.8% Leo Samia kaurudisha 5 8%,Usiwe kama zezeta,
 
Duuuuh,

Naona vijana mnakaza kwelikweli, hatupumui,
Nikweli alichofanya Rais nikupunguza gharama sana,
kwenda na ndege binafsi gharama ni kubwa,

Hongera rais Samia, Karibu nyumbani
Kwa hiyo na huku nchini atakua anapanda magari ya abiria kupunguza gharama? Pamoja na delegate yake?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Kwani nani alisema kuwa aende na Boeing? Kwani Kikwete alikuwa anakwenda Boeing ambazo hazikuwapo wakati huo? si angeenda na Gulfstream ambayo ndiyo ndege rasmi ya rais? Kwanza Gulfstream ina range kubwa sana na haili mafuta kama Boeing; akienda na Gulfstream hawezi kubeba delegation ya watu 40!
 
Niwazo zuri pia
 
Kumbe mafuta ya ndege lita moja ni cheap kuliko petroli! Lita moja TZS 1,162/=!! Aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…