Aliyeharibu ni huyu afisa wa TFF. Badala ya kusubiri mechi ziishe, yeye akaanza kutoa ufafanuzi hadharani kwa kutaja majina na takwimu za Mayele na Mpole. Kimaadili, afisa anayehusika na maamuzi hakutakiwa kutanguliza maelezo kama hayo kabla ya mechi kuisha. Ni sawa na mjumbe wa Kamati ya Nidhamu kutaja hadharani adhabu atakayopewa mchezaji fulani hata kabla ya vikao vya kupitia kosa husika havijakaa, hata kama anajua
Bodi ya Ligi Tanzania Bara βTPLBβ imetoa ufafanuzi wa tuzo ya Mfungaji Bora kwa msimu wa 2021/22, ambao utafikia tamati leo Jumatano (Juni 29) katika viwanja vinane tofauti.
Afisa Habari wa TPLB Karim Boimanda, amesema endapo wawili hao watamaliza msimu wakiwa na mabao sawa ya kufunga, wataangalia kanuni ambazo zinatoa ufafanuzi nani anapaswa kuwa mfungaji bora.
Boimanda amesema: Ikitokea Fiston Mayele na George Mpole watamaliza msimu na magoli kama yalivyo sasa (16), kikanuni Mayele ndiye atakuwa mfungaji bora kwa kuwa hana goli la penati wakati Mpole ana penati mbili.β