Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
- Thread starter
- #261
Japo hii ni mada ya zamani ila kufuatia revelations za kitabu cha EK, kuna watu wanashangaa kwa baadhi ya mambo EK aliyoaandika,Wanabodi,
Hoja ya Udikiteta Tanzania
Kwa wiki kadhaa sasa nimekuwa nikijadili hoja ya Udikiteta Tanzania. mada ya leo ni kuhusu uzalendo wa ajabu wa Watanzania kuunyamazia uongo unaoenezwa kimataifa kuhusu huu udikiteta Tanzania. Jee Sisi Watanzania, Tuna Uzalendo Gani Kunyamazia Huu Uongo Unaonezwa Kimataifa Kuwa Rais wa Tanzania ni Dikiteta na Tunatawaliwa Kidikiteta?. Au Kwa Kunyamaza Huku Ndio Kukubali Kwenyewe Kuwa ni Kweli Taifa Letu Tanzania Tuko Kwenye Udikiteta?
Kama ni Kweli Tanzania Tuna Udikiteta na Sisi Wenyewe Tumeukubali, Kwa Nini Watuingilie?.
Kama ni kweli rais wetu Magufuli anatenda kinyume cha katiba na sheria, na taratibu za kumshughulikia zipo lakini sisi Watanzania wenyewe tumeridhika naye na utendaji wake huo huo, hivyo hivyo anavyotenda iwe kwa kuvunja katiba au kinyume cha sheria, Watanzania wenyewe tumeridhika na kukubali, who the hell is jirani yasiyomhusu, anayekuja kutusemea kwenye media yao kuwa rais wetu amekosea? Kama wenyewe tumekubali na tumeridhika, huyu jirani anamsemea nani? Kwa nini Watanzania tunanyamasia uongo huu?
Paskali
Kwanza naomba kusimama na EK ni mwandishi wa IJ, na kiukweli Tanzania tuna waandishi wachache sana wa IJ na EK is one of the best that we have!.
Hivyo yote aliyoyaandika ni mambo ya kweli aliyohadithiwa, akayafanyia IJ, akajirodhisha akayaandika.
Baadhi ya hayo aliyoaandika, tuko wengi tuu tuliyasikia, lakini hatukuyafuatilia. Mengine yaliripotiwa na yule mdada kichaa wa Marekani kwenye mtandao wake, na hayakuwahi kukanushwa!.
Kazi ya uandishi wa habari duniani kote ni kazi ya kufanya jambo moja tuu, to “tell nothing but the truth”, with truthfullness, objectivity, impatialty and balance, yaani kusema kweli daima, ila unapima maslahi ya jamii, usiegemee upande mmoja na kuibalansi au kuwa na kiasi.
Ila katika kuusema huo ukweli, sio lazima kuusema kila ukweli unaousikia, ukiupata ukweli, unaupima kwa kitu kinachoitwa objectivity test kwa kujiuliza, ukweli huu utasaidia jamii?. Ikikutana na ukweli ambao ukisemwa hauta saidia jamii, then wewe mwandishi mwenyewe unajifanyia self censorship na kuuhifadhi tuu huo ukweli kwenye kifua chako!.
Sisi Waafrika tuna utamaduni wa kuwaheshimu sana marehemu wetu, mtu anapotangulia mbele ya haki, anazikwa na maovu na mabaya yake yote, ila mema ndio anatuachia. Marehemu hasemwi kwa ubaya, anasemwa kwa wema, na kukitokea ubaya mkubwa kumhusu marehemu, ubaya huo hausemwi kwa mtu ambaye hawezi kujitetea!.
Kwa vile kitabu kiko sokoni na nimeona mahali, ni hot cake, kina uza kweli kweli!, hata kama ni kweli, mamlaka zetu zina wajibu wa kumtetea marehemu kwa kupunguza damage controll kuwa sii kweli!.
Kwenye unyago wa kuwafunda mabinti wa baadhi ya makabila, binti anapewa figa moja ainjike chungu, anashindwa, anapewa mafiga mawili, anashindwa, anapewa mafiga matatu ndio yanainjika chungu, somo hapo ni figa moja haliwezi!. Ila binti anafunzwa, ikitokea umefumaniwa, hata kama mtakutwa kama ulivyozaliwa, wewe kataa kata kata kwa kanusha kuwa ilitaka kutokea ila haiku....!. Mwenye mali atakasirika sana, ila akitulia, hasira zitapoa, na kasababu aliambiwa haiku..., atasamehe na maisha yataendelea, kumbe ndio zao watu wa kabila hilo!.
Hivyo kitabu kiko sokoni, mamlaka zetu lazima ziibuke na kusema huo ni uongo mtupu, Watanzania tutaiamini mamlaka kuliko mwandishi!.
Mambo mengine yaliyoripotiwa ni mambo ya maisha binafsi ambayo yana kinga ya kihabari ya the right to privacy, hayakupaswa kuripotiwa!.
Naendelea kusisitiza
uzalendo wa kweli wa Mtanzania kwa kutokusema kila kitu!. Mfano lile tukio la tarehe 17, akina sisi tulipenyezewa tarehe 12, na tukaelezwa ugonjwa. Lakini kwa vile tumetangaziwa rasmi ni tarehe 17 na ugojwa uliotajwa, Mtanzania mzalendo haiwezi kusema tofauti!. Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele ‘Maslahi ya Taifa’?
P