Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?

Kwa maneno rahisi, dikteta ni yule anaekiuka katiba ya nchi ambayo aliapa kuilinda...! Mengineo ni nyongeza tu!..alichopanda ndo anakivuna.. nyerere, mwinyi..mkapa..jk walipita hakuna hata mmoja alieambiwa dikteta sababu tu waliheshimu katiba..huyu mwe!!
 
Paskali nadhani swali lingekuwa fupi tu..kwa nini msemaji wa serikali anakaa kimya pale media za nje zinapotoa taarifa za kukashifu au kupotosha..wako watu wameajiriwa kwa kazi hii na wanalipwa, sidhani inaleta maana sana raia kujibu kila upotoshaji unapotokea ilihali wanaotakiwa kujibu wako kimya..labda hawaoni sababu ya kujibu, wakumbushe mara moja Paskali siyo na wewe sasa ndio umeona cha kuongelea na kuandika kila siku..leave them, they r comfortable!
 
Paskali nadhani swali lingekuwa fupi tu..kwa nini msemaji wa serikali anakaa kimya pale media za nje zinapotoa taarifa za kukashifu au kupotosha..wako watu wameajiriwa kwa kazi hii na wanalipwa, sidhani inaleta maana sana raia kujibu kila upotoshaji unapotokea ilihali wanaotakiwa kujibu wako kimya..labda hawaoni sababu ya kujibu, wakumbushe mara moja Paskali siyo na wewe sasa ndio umeona cha kuongelea na kuandika kila siku..leave them, they r comfortable!
 
Yaani nayajutia maisha yangu kuja kuishi kwenye utawala wa huyu jamaa. Mtu asie na vision, kapewa tu mamlaka juu ya nchi , hata msaada wowote. Ntaunga jitihada yeyote ya kumuondoa huyu jamaa
 
Kwanza kaingilia dirishani, unavuna ulichopanda.
Ukitaka usiitwe mwizi acha wizi, vinginevyo unaendelea kuitwa mwizi.

Lucifer ni mtawala wa dunia hii ila kwa vile kaingilia dirishani na matendo yake na ndio anapewa majina mabaya ya kila aina, devil, mwizi, muasi muuaji malizia na mengine.

Kwa hiyo utapewa sifa kutokana na matendo yako, ukiwa muuaji utaitwa muaji, ukiwa mwizi utaitwa mwizi, regardless ya title uliyonayo, hakuna cheo hapa duniani kitasafisha matendo yako, njia rahisi ni kuachana tu maovu.
 
Baba gani watoto wanakufa njaa anawaambia mwafa,hela za rambirambi unakunywa pombe hela tunazoleta nyumbani hatuoni zinatumikaje. Baba anatishia kuua ukihoji huyo ni baba au jambazi
 
Watanzania na waafrika kwa ujumla ni madishi mpaka leo hatujui kwa tu masikini je tutajua umuhimu wa kujithamini na kukubari vyetu
 
Mara nyingi nawaonaga wakimbiaji wa Kenya kwenye mbio za marathon hasa Golden league, wapo wale wanaoanza mbio kwa kasi ya ajabu halafu mwishowe anajitoa.. Ni sawa na huyu Pascal manake umeandika mengi ambayo mwishowe inaonyesha umepoteza muda mwingi kwa kuandika upupu!! Haya yote uliyoandika ni kama unamdhalilisha rais wetu maana alishasema akiwa rais watu watalimia meno sasa unapoaminisha watu kuwa rais hakumaanisha haya yanayotokea chiniya utawala wake basi wewe unawaza kupitia tumboni, yaani huna tofauti na yule Jenny mulo.
 
Sasa pascle why cant u file an application letter to ur fellow sukuma man so that u may substitute with msigwa of iringa? Ur real boring so much for the sake of ur personal gain. Unejitaidi kuomba kaz kutipitia uzi wa JF mshikaji kakubania. Tumia formula mbadala
 
Magufuli angekuwa Rais wa Marekani au Ufaransa ndiyo angekuwa dikteta kwa hapa kwetu Tanzania ni HERO Period hakuna kulemba.
 
Pascal kwa makala yako hii inaonyesha ulivyoanza kuyumba. Vizuri vyote anavyofanya Rais wetu kwa sasa vinafunikwa na mabaya mengi anayoyafanya!! Haiwezekani mambo mengi ya ajabu (kutekwa, watu kupigwa risasi, polisi kuonea raia, wakuu wa mikoa kulewa madaraka, hasara kwa Taifa kupitia ununuzi w ndege "Bombardier", kuminya demokrasia na uhuru wa maoni, uonevu wa TRA, viongozi wa upinzani kunyanyaswa) yatokee chini ya uongozi wake. Haiwezekani mambo yote haya yaibuke ghafla awamu hii ya 5. Lazima kuna hitilafu mahali!!
 
Kwanza Raisi sio baba kwenye familia yangu labda yako, ndio maana alikuita 'njaa'. Uzalendo ni kutetea maslahi ya taifa na sio kiongozi. Alipochaguliwa kuwa raisi alitakiwa kufuata katiba na maslahi ya waliomchagua. Anapogeuka na kuwa muuaji wa wananchi wake na kutunyima haki za kujieleza na kukusanyika ambazo zipo kikatiba anapoteza haki ya kutuwakilisha.

Na hayo majarida ya nje hayajatukana taifa wala kusema uongo kama unavyodanganya hapa, yanausema uongozi mbovu wa Pombe ambao magazeti ya ndani yakiandika yanaishia kutishiwa na kufungiwa na sisi wananchi tukisema tunaishia kupigwa risasi. Ukweli siku zote haujibiwi na risasi ndio maana hawana majibu unapotoka nje.

Na kwa taarifa yako walengwa wa haya magazeti sio watanzania bali ni wawekezaji wa nje na serikali zao zinazomwaga pesa za misaada kila wakati kwenye nchi zetu. Na hivyo basi wana sababu ya kuandika uovu wa Pombe na kuzishauri serikali zao kuhusu upelekwaji wa kodi zao kwenye nchi ambazo hazifuati misingi ya kidemocrasia na haki za binadamu ambazo wao wanazisimamia.

Kwa kumalizia, hivyo vyombo vya habari ulivyovi 'quote' vinaheshimika na kuaminika sana huko kwa walengwa, sasa badala ya wewe kuja hapa na propaganda za kumtetea Pombe kwa sababu ya 'njaa' na kutafuta teuzi. Kwa maslahi ya taifa, ulipaswa kuja na majibu ya haya ambayo yamekuwa yakisemwa na hayo majarida: matukio halisi ya utekaji, utesaji, kupotea kwa watu, mashambulizi ya silaha dhidi ya viongozi wa kisiasa, mauaji yenye mwelekeo wa kiitikadi, matumizi mabaya ya vyombo vya dola dhidi ya wananchi, uminywaji wa uhuru wa kujieleza, uminywaji wa shughuli za kisiasa kwa vyama vya upinzani na mahakama na bunge kuingiliwa na 'eti' muhimili uliojichimbia chini (ujinga mtupu).
 
Kwanza aombe radhi yeye sisi tutafatia. Alitutukania wadogo zetu pale Udom kwa kuwaita vilaza. Ilituuma sana.
 
  1. Tatizo waandishi wetu mnamajina makuuubwa lakini uwezo so mkubwa na uwezo haukuwi! Yaani siku zinavyokwenda ahamuongezi umahiri bali ndopumba zinazidi. Andika vitu straight sio kukoroga koroga na kujizungusha chyaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…