Uzalendo wa ajabu wa Watanzania: Nchi inatukanwa, Rais anatukanwa, tumenyamaza. Huu ni Uzalendo gani?


Ndugu. kwa stail ya kujitoa uhamu, wazamini wa makala zako watakuwa makada wa lumumba, labda ionyeshwe TBC ...kwenye TV utafanya wakose wateja kama TBC unless uvae kinyango wasijue ni ww. Kwa hili bandiko napenda niseme toka moyoni umeonyesha undumilakuili wa kutoasha.
Uko tayari kuona watu wanateseka na bado ukasaport mateso ya watu walio wengi ili tu ukombe miguu ya watawala upate cheo cha kuteuliwa.
Mungu sio Juma, Pascal wala Mayala.

Alisema BORA MCHAWI KULIKO MNAFIKI
 
Tabia za dikteta zinafahamika, zipo wazi! Anachofanya Magufuli ndiyo udikteta halisi. Watu hawawezi kupotea yeye asiwe na habari, watu hawawezi kuokotwa mto Ruvu au Coco beach wakiwa wamefungwa kwenye viroba rais asiwe na habari ya nini kinafanyika katika nchi yake! (ingawa Kamishna Lazaro Mambosasa anatuambia inawezekana maiti hizo zimetoka Angola.....Hivi nani kamfundisha Geography?) Tanzania imeshakuwa kama Kenya miaka ya 1980"s wakati walipouawa akina Robert Ouko na wengine au miaka 1960's-1970's walipouawa akina JM Kariuki, Ronald Ngala na Tom Mboya......Tusipopiga kelele na kupaza sauti, watesi wetu hawataogopa na wataendelea kutupiga na kutuua bila sababu.
Wengine wetu tunaweza kuwa na mahaba na rais Magufuli hasa kwenye mambo ambayo tunafikiri ni mazuri anayoyafanya lakini ukweli unabaki pale pale rais wetu njia anayotumia kwenye kuongoza/kutawala siyo nzuri, Mambo yale yale ya Libya aliyokuwa anafanya Ghadaffi ili aonekane ni mwema kwa upande mmoja....Kwa kwetu anasema yeye ni rais wa wanyonge...vipi kuwa rais wa watu wengine wasio wanyonge? Madikteta huwa wana tabia ya kusifiana, Magufuli alimsifia Ghadaffi kuwa Libya ukioa unapewa dola elfu hamsini(sina uhakika kama kuna ukweli, nachojua walikuwa wakipewa welfare ya dola 500 kila mwezi!) lakini alisahau mambo aliyokuwa akifanya Ghadaffi ikiwamo kuhusika na ulipuaji wa mabomu kwenye Night club kule Germany, kuangusha ndege ya Pan Am kule Lockerbie Uskochi, kuua imamu mkuu wa Lebanon(baada ya kubishana kuhusu maandiko ya Quraan), Bado akamsaidia Idi Amin aliyevamia nchi yetu na kuua raia zaidi ya elfu 40 wa Kagera....Leo hii huyu Magufuli anamsifia Ghadaffi???
Rais Nyerere alisema ni nafuu uwe maskini lakini uwe huru, Magufuli anataka tumwabudu kwa kazi ambayo ni wajibu wake kufanya huku akiminya demokrasia kwa nguvu zake zote (Tunafanywa kama watoto wa Kindergarten). Kujenga reli ya kati huo ni wajibu wake (Ingawa alianzisha rais Kikwete) ni moja ya job description yake......hahitaji sifa ya aina yoyote , kwani awali ya yote tutapanda hiyo train free? Kwanini anajipa sifa ambazo hazina msingi? Kila mikutano anasifia kazi zake za ujenzi (ingawa hiyo ni protocol ya waziri wa ujenzi), mbona haongelei ELIMU inayoporomoka siku hadi siku....Iliteracy inapanda kila siku, biashara zinadorora kwa kudaiwa kodi kubwa, watanzania wanaofungwa nje ya nchi anatuambia wanyongwe na wauawe kabisa (Je huyo ni rais wa kawaida ambaye bila kuhakikisha kwamba kuna uonevu au la, yeye anakazia hukumu kuwa watanzania wanyongwe....Kama wameonewa je?...Mbona alimwachia huru babu Seya aliyehukumiwa kwa kubaka?) KIATU CHA URAIS HAKIMTOSHI HUYO DIKTETA, ndiyo maana anapigana na kila mtu, si wanasiasa wa upinzani, wafanyakazi wa umma, viongozi wa dini, wafanyabiashara, na matajiri wenye kumiliki viwanda na makampuni. Kilichomjaa huyu rais ni wivu na visasi hakuna lingine!
Paschal, wanachosema watu wa nje ikiwamo magazeti yao ni ukweli mtupu, Magufuli amechaguliwa kwa bahati mbaya hafai urais labda uwaziri mkuu, ndiyo maana anakotupeleka siko sahihi. Tunaelekea shimoni na kutoka huko ni kazi kubwa.
 
Hivi uzalendo nini, katika kukua kwangu cjawahi ona ama kusikia mzalendo katika nchi hii. Panapostahili pongezi nitapongeza, pale ninapoona giza vile vile sitaacha kupeleka Nuru, uzalendo c kuona watu fulani kwamba ni special sana No. Tutumie huo uzalendo kuelezea mabaya yote na mazuri yote bila kupindishapindisha ukweli, otherwise utakuwa unaleta unafiki.
 
Madictators wote duniani wanaanza kimya kimya kwa kuminya vyama na watu wanaomsubua kiongozi. Tutaamini vipi kama sio dictator wakati sifa za udictor anazo! Kimbuka madictators wanatabia yakuwafanya raia wampende kiongozi hata kama hawamkubali
 
Mkuu hii madam yako na Aina ya uandishi wako unatia ukakasi.
Ukiangalia Kwa mbali wewe ndie unaechochea au unayeuabarisha umma kwamba Raisi wetu ni Dicteta.
Njoo na mada zinazoelezea ni jinsi Gani mkuu ni mwema na uyaelezeee Yale mazurii anayofanya ili watz wajue
 
Mayalla acha kucheza na akili za watu. Huyu MTU anatakiwa kupinduliwa exaggerations zake. Hebu niambie leo unaleta takwimu za inflation kuwa chini ya 3.9 kweli na sisi kiujinga wetu tunapokea wakati chakula sokoni juu, mafuta juu, vifaa vya ujenzi juu, shilingi inadorora lkn anakuja kutudanganya kuwa inflation 3.9 kweli. Kwanini usitukanwe.
 
Watu wamezibwa midomo Habari za kiuchunguzi hakuna tena Waandishi wanapotezwa wengine kutekwa japo kuna Matamshi ya kujiteka wengi wanasema bora liende ama kanyanga twende
 
Hujuma dhidi ya taifa haikubaliki lakini kwanini tumefika hapa?

Nani wametufikisha hapa?
 
Tufanyeje kasha tukanwa sana, sasa tumeanza kuzoea. Hata yeye Alisha sema kwamba kasha zoea, na aliwahi kusema hata kama kuna mapepo apelekewe yeye hatojali. sasa sisi tufanyeje, ingawa unataka tukawatukane wanaomtukana, lakini labda tunawaogopa, maana anayetukanwa naye haonyeshi kukerwa hivyo mi nashauri tutulie tu. Siku akionyesha kukerwa tutajua tu na huwa hawezi kukaa kimya atatuambia tu, sasa hapo nasisi hatutosita kujitutumua, kumuonyesha kwamba tuko nyuma yake na tunaunga mkono kukerwa kwake. Hatutafanya chochote mpaka atupe amri yake yeye anayetukanwa, sasa hivi tutaonekana tunawashwawashwa.
 
Katika pitapita zangu nimekutana na Cambridge Advanced Learner's Dictionary linaandika "dictator noun 1 a leader who has complete power in a country and has not been elected by the people 2 a person who gives orders and behaves as if they have complete powers
 
Pasco usihangaike na waliokata tamaa ya kuishi
Mtu yoyote aliekata tamaa,sifa yake kuu ni kufurahia majanga!
Sampuli ya watu wa aina hii wengi wanapatikana Tanzania
Ugumu wa maisha yao hasira kwa ccm
Wengine wamepandikizwa maalum na vyama vyao kuhamisha ajenda ili chaguzi za ndani na ruzuku zisijadiliwe
Ndio mana siku hizi wapinzani hawana hoja,ni matukio tu,deni likilipwa watasubiri tukio jingine
Sore losers!
 
Neno sisi kwenye makala yako nashindwa kuielewa mayala. Upingaji usingekuwepo Kama tungekubali unachokisema. Msimamo wako usiwe wa watu wote nchini.
 
Sasa atukanwe yeye tujibu sisi.... kwani yeye hana mdomo..., Actions speaks louder than words kwanini maneno ya watu yanamuogopesha mtu, kama jamaa tunapoteza rasilimali na muda kutaka kuwaziba watu midomo..., You can take a Donkey to a river but you can not force it to drink....
 
Ahsante kwa posting zako hizi. Zinatufanya tuendelee kuieleza jamii ya watu wapenda haki juu ya kinacho tokea Tanzania hasa kwa Tabaka LA watawaliwa jinsi wanavyo tendewa na wenyemadaraka, huku wenye madaraka wakifikiri kuwa wanaungwa mkono kwa mauajo na mateso wanayo wafanyia wanyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…