Jambo la kwanza ninapenda kukushauri kwamba sio busara kujibu post za kila mtu hapa JF, hii inakufanya kushindwa kupata muda wa kusoma kwa makini na kuelewa kile kinachokusudiwa, matokeo yake unajibu nje kabisa na kile kinachozungumzwa, post zako nyingi zinaonyesha kutokua makini katika majibu yako.
Nani aliyesema kwamba Tanzania tunategemea soko la nchi moja?, sisi tumesema tunauza Cement yetu katika nchi mbalimbali zilizotuzunguka na hata nchi za mbali kama Zimbabwe na South Africa, hii habari ya Marekani kutotegemea Kenya na Tanzania kutegemea Djibouti imekujaje na inahusianaje?, sisi tumetaja nchi ambazo tunaziuzia Cement na zile ambazo tunategemea kuziuzia siku zijazo, sasa huko kutegemea kumeanzia wapi?, wacha kudandia kujibu bila kuelewa mada husika