Uzalo Special Thread

Ninaposema nimekufa nimeoza kina Vera ginger wananiona kama nimedata aseeh [emoji23][emoji23]

Halafu manzuza ni mlokole wa mchongo tu sababu anajudge wengine na kisirani plus sio mwepesi kusamehe.
Hahahahaaa[emoji23][emoji23][emoji23]endelea kupambania mzigo huo
 
Ila sba ni bonge Moja la duuh na kanajua kuact ,naona Amos kapata demu wa kumuuza mwingine
 
Sba maovu yake yakija kujulikana sjui ataweka wapi suraa... bora ya Ayanda ye tushamzoea😅
 
My g mabuza anapigilia misumari hatari wamefanya la maana sana kuniletea jembe langu anakwambia kaokoka
 
Kwa ufupi uzalo Thursday..
Asbuhi na mapema thobile akipiga tizi, anawaona pastor nkosi na Esther wakipigana makiss. Anashtuka na kwenda kumwambia gc.

Anamwambia kwamba gc alikosea kusema fikile ndo chakula ya pastor, yeye (thobile) amewaona Esther na nkosi sio fikile, muda huo fikile anafika saloon hapo wote wawili wanafunga madomo yao japo fikile alishawaskia..

Kule kwa manzuza ayanda anatoka tizi na kumkuta manzuza mezani akichagua magauni ya bibi harusi mtarajiwa ambaye ni sma, ayanda anamaindi kidogo na kudai bado mapema, lakini maza anamkazia kudai ayanda amekuwa baba na aachane na side Chicks (anamaanisha kina sibahle).
Mara ayanda anaona gauni moja zuri anasema size ya sibahle, Mama yake anamkatisha na kudai sibahle ndio amechangia ayanda kuwepo matatizoni hivyo amsahau, ayanda anadai kammiss sibahle ila maza anakaza bado..

Kule kwa mangcobo wapo jikoni na nosipho wanabishana , nosi anadai kuwa mama yake anaenda kumuuza kwa yule jamaa muuwaji (govender au prevender kitu kama hicho).

Mama yake anadai nosi afanye hivyo kwa sjili ya mxo na sio kingine ila nosi anagoma kata kata na kwenda chumbani kwake..

Gerezani thobile anaenda kumtembelea zweli, anadai bado anampenda zweli na amemmiss pia anaahidi kumsubiri zweli mpaka atapotopoka kwani anaamini zweli hana hatia kabisa ,wanaongea mengine kisha zweli ananyooshs ngumi kwenye kioo kinachowatengenisha na thobile anakutanisha mkono..

Saloon tena gc akiwa na mteja huku pembeni fikile anamuangalia gc vibaya naye gc anashtuka kisha fikile anamuomba gc waongee, wanasogea pembeni, lakini kabla kila mtu hajaanzs kujitetea anafika Esther na gc anafunga mdomo kisha Esther anamuulizia thobile kwani ana miadi naye atengenezwe kucha , gc anajibu thobile ametoka..

Polisi pale ayanda anaenda kufuatilia kesi ya msichana yule yatima aliyefariki baada ya kunajisiwa na pastor lakini mondil anamjibu kuwa amefunga file la kesi kwani ameona nkosi hausiki kwa namna yoyote , ayanda anamaindi lakini hakuna jinsi..

Gerezani tena mxo yupo na shown na zweli shown anawaambia rufaa yao imetupiliwa mbali hivyo tarehe 3 wajiandae kwenda mahakamani kusikiliza kesi yao ya mauwaji hukumu itatoka,

Mxo anamaindi na kudai shown ameshindwa kazi kabisa na wao hawawezi kukaa hapo kwani wanamuogopa sana yule gangster mindlos, kisha mxo anamuomba shown akatoe pesa rand 100000 ili wahonge kwa mkuu wa jela ili mindlos ahamishwe.

Mabuza akiwa home kwa mangcobo wanajadili kuhusu kukataa kwa nosi kujilengesha kwa yule muhindi mangcobo anamuuliza Mabuza kwanni anafanya yote haya ikiwa kaokoka,
Mabuza anadai anafanya haya kumsaidia mxo kwani hajaua..
Ghafla nosi anatokea na kukubali kufanya kazi aliyopewa.

Jela tena mxo akiwa na zweli wanajadili kuhusu kulipa hela na mindlos ahamishwe kuna jamaa pembeni mfungwa anasikiliza kijanja ,huku zweli kama ameshtukia hivi,kisha jamaa anaondoka kwenda kutoa taarifa kwa mindlos na jamaa anamaindi na kuamuru vijana wake wakawafunze adabu kina mxo,

Hapo hapo afande yule mdada ambaye ni demu wa zweli anapita na kusikia hayo kisha anaondoka haraka sana.

Noxi anaenda gateway kumtega muhindi yule na wanaparamiana, kisha muhindi anajipendekeza kuomba lunch nosi anagoma na pia date nosi anagoma mwisho muhindi anaomba namba ya nosi na anaipata wanaagana..

Sma pia aliletewa nguo za mtoto wske ajaye na thobile anauliza thobi kajuaje haya , thobile anadai ameambiwa na zweli kule jela na kusema zweli aliomba sma aksnunue nguo za mtoto.. thobile anauliza mimba ya nani sma anaomba thobile asiseme kwa mtu, anamtaja ayanda na thobile anashtuka..

Nkosi akiwa church ametegesha camera anaanza kurekodi mahubiri yake kitini ghafla akaingia fikile, nkosi anadai ana kazi lakini fikile anadai kafata upako.

Anasema kafunga milango ya kanisa yote kisha anamfata nkosi kitini wanapakatana na nkosi anatoa mafuta..

Sma anaenda hospitali for checkup ghafla anaambiwa na dr kuwa hana mimba kwani alikosea vipimo vya mwanzo ,sma anababaika sana


Mimi sio mwandishi mzuri vile vile nimeishia darasa la pili b..

NB: sma acha uteseke mbwa wewe si uliniringia 🤣🤣🤣
Jagiya Vera ginger Mafian cartel na wengineo
 
swafi sana umeniokoa pakubwa leo
Mabuza nampa hongera sana... sio mvivu kwenye mambo ya uchunguz kama huyu dinangwe.
Kama namuona nosi vile kwenye hiyo game anayoenda kuplay maana si mzembe sekta hizo..
Sasa apo kwa sma iyo mimba mbona nae pia alijipima ama hivyo vipimo vyake vilimletea majibu gani mbali na hospitali maana sielewi...
😅😅Sma anaonja joto la jiwe yani n full misukosuko
 
siyo tu kupima hata mamlambo alimwambia kabla hiyo scene wameikosea kuipangilia
 

asante sana, jana sikuangalia ila kwa maelezo haya leo nitaelewa muendelezo
 
Unajua baba sma
 
Yaani cha moto anakiona mbwa huyu hajui wengine kwa mashu wananifata fata?🤣🤣🤣

Sema hapa kwenye hii mimba wametupiga sana hawaeleweki..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…